Barua Rasmi kwa Viongozi wa Tanzania kuhusu Mgomo wa Madereva
Anwani:
Kwa:
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu, Dodoma
Nakala kwa:
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba – Waziri Mkuu
Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa – Waziri wa Uchukuzi
Mheshimiwa Deogratius Ndejembi – Makamu wa Rais
Na viongozi wengine wote wa Serikali na Bunge.
Tarehe: 29 Septemba 2026
Kichwa: Ombi la Haraka la Kutatua Malalamiko ya Madereva na Kusimamisha Mgomo wa Kuendesha Magari
Mheshimiwa Rais na Viongozi Wote,
Tunawaandikia barua hii kwa heshima kubwa kama wananchi na wadau wa sekta ya usafiri nchini Tanzania. Tarehe 29 Septemba 2026, madereva wote nchini wameamua kuadhimisha siku yao kwa kuacha kuendesha magari kwa muda ili kuonyesha wasiwasi wao mkubwa juu ya sheria na kanuni mpya zinazowekwa kila siku.
Sababu kuu zilizotolewa ni:
• Mfumo wa pointi 15 kwenye leseni za madereva ni mzigo mkubwa na unaosababisha hofu ya kupoteza riziki.
• Sheria mpya hazizingatii hali halisi ya maisha na kazi za madereva.
• Adhabu, faini na kusimamishwa leseni kwa makosa madogo madogo kunawafanya waishi kwa hofu na kuteseka kisaikolojia.
• Serikali inapaswa kusikiliza sauti zao na kuwapatia mazingira bora ya kazi.
Mgomo huu si wa ajali wala vurugu, bali ni haki yao ya kuomba usikilizwe. Madereva wanasema “Umoja ni Nguvu” na “Pamoja Tunaweza” – wakiungana wataweza kupata haki zao.
Tunaomba Serikali, hasa Wizara ya Uchukuzi na viongozi wakuu, waangalie suala hili kwa haraka sana. Tafadhali fanyeni mazungumzo na wawakilishi wa madereva ili kurekebisha kanuni zinazosababisha mzigo huu, ili usafiri wa watu na bidhaa usiathirike na uchumi wa nchi usiingie kwenye matatizo.
Tunategemea jibu na hatua za haraka.
Ahsanteni sana.
Watia saini:
Wananchi na Madereva wa Tanzania
(Pamoja Tunaweza)
Handles za ku-tag kwenye X (Twitter)
• Rais: @SuluhuSamia
• Waziri Mkuu: @mwigulunchemba1
• Waziri wa Uchukuzi: @MbarawaM
• Msemaji Mkuu wa Serikali: @TZMsemajiMkuu
Unaweza kuongeza hashtag kama #MaderevaTanzania #SikilizeniSautiYetu #TanzaniaTransport ili ieneze haraka.
HONGERA SANA Sr. Dkt. Sarah Kahumbya Deogratius, Mkurugenzi wa Hospitali ya Cardinal Rugambwa kushinda Tuzo ya Else Kröner Fresenius ya Ushirikiano wa Maendeleo katika Tiba kwa mwaka 2026, kwa kutambua kazi yako ya kuimarisha utambuzi na matibabu ya kifafa pamoja na huduma kwa watoto wenye ulemavu.
Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kila mwaka na Else Kröner-Fresenius-Stiftung (EKFS), hutambua miradi bora pamoja na watu wanaoiongoza katika kuboresha huduma za afya katika nchi zenye rasilimali chache.
Kwa mwaka 2026, tuzo hiyo ililenga huduma kwa watu wenye ulemavu na iliambatana na zawadi ya Euro 250,000, sawa na takribani Dola za Marekani 286,975.
Taasisi hiyo ilimtangaza Sr. Dkt. Deogratius kuwa mshindi wa mwaka huu kutokana na mradi unaoitwa “Kuimarisha Utambuzi na Huduma za Kifafa kwa Watoto Wenye Ulemavu nchini Tanzania” (Strengthening Epilepsy Diagnosis and Care for Children with Disabilities in Tanzania). Aliteuliwa kuwania tuzo hiyo na Evangelisches Krankenhaus Alsterdorf (EKA), taasisi ya huduma za afya nchini Ujerumani.
Sr. Dkt. Deogratius ni Sista wa Kanisa Katoliki kutoka Tanzania, daktari wa tiba na mtaalamu wa afya ya umma, ambaye ameunganisha wito wake wa kitawa na taaluma ya udaktari pamoja na uongozi katika sekta ya afya.
Sista ni mwanachama wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu la Jimbo Katoliki la Bukoba. Ana shahada ya Udaktari wa Tiba na amefanya masomo ya uzamili katika afya ya umma na tiba ya magonjwa ya ndani. Pia amesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
Tangu alipokuwa Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Cardinal Rugambwa, Dar es Salaam, mwaka 2016, Sr. Dkt. Deogratius ameripotiwa kusimamia juhudi mbalimbali za kuimarisha utoaji wa huduma katika hospitali hiyo ya Kanisa Katoliki. Juhudi hizo zimejumuisha kupanua huduma za uchunguzi wa magonjwa, kuboresha huduma za famasia na kuendeleza huduma maalumu za kitabibu.
Chini ya uongozi wake, hospitali hiyo inasemekana kuwa imeongeza uwezo wake wa kutoa huduma kama hospitali ya rufaa ya kikanda. Kazi yake pia imewafikia watu wanaoishi na ulemavu, hususan watoto na watu wazima wenye kifafa.
Ushirikiano kati ya Hospitali ya Cardinal Rugambwa na Evangelisches Krankenhaus Alsterdorf, iliyoko Hamburg, Ujerumani, umejikita katika kuboresha utambuzi na matibabu ya kifafa pamoja na kuongeza uwezo wa wahudumu wa afya katika kuwahudumia watu wenye ulemavu.
Kwa mujibu wa taarifa ya hospitali kuhusu tuzo hiyo, kitengo cha urekebishaji na utengamao (rehabilitation) cha hospitali kinatumika kama kituo cha rasilimali na huduma kwa watoto wenye ulemavu, wakiwemo watoto wenye ugonjwa wa kupooza kwa ubongo (cerebral palsy), ucheleweshaji wa ukuaji na maendeleo, pamoja na Down syndrome.
Kutunukiwa kwa Sr. Dkt. Sarah Kahumbya Deogratius ni utambuzi muhimu wa juhudi zake katika kuboresha huduma za afya kwa watu wenye ulemavu, hususan watoto wenye kifafa, na mchango wake katika kuimarisha huduma za afya nchini Tanzania.
MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISSU
*LISSU:* Sasa naomba nimalizie.
*JAJI NDUNGURU:* Je, ni sehemu ya submission?
*LISSU:* Ni sehemu ya submission, wala si maneno mabaya.
Ni hivi, Waheshimiwa Majaji, kesi ya uhaini ni kesi ngumu sana.
Ukiachilia mbali siasa zake, ambazo pressure zake ndizo zinafanya kesi kuwa ngumu.
Pamoja na kesi kuwa ngumu, nyinyi Majaji mmefanya kazi nzuri sana.
Mmetusikiliza, mmetupa nafasi ya kujitetea.
Hamjanikwaza.
Mmekuwa wavumilivu sana.
Mmefanya kazi kubwa sana na mmefanya kazi nzuri sana.
Nilitaka nisimalize bila kusema haya, pengine hatutakutana tena.
Nilitaka mjue kuwa moyoni mwangu mmefanya kazi nzuri.
Hawa mawakili wangu wa Serikali na wao wamefanya kazi nzuri.
Wamepambana sana mpaka kufika hapa. Pamoja wamekuwa na kesi ya ovyo sana.
Ila wamepambana sana bila kujali nini kitatokea, wamepambana sana.
Nafikiri nawatakieni heri sana.
Asanteni sana.
Haya ndiyo nilitaka yaingie katika rekodi.
Nafikiri msipoyaingiza katika rekodi, mtanikwaza.
Kuna jinsi ambavyo huyu jamaa amejitoa kwa ajili ya Tanzania na Watanzania….
Na ni kweli matatizo yote ya haki tuliyonayo TZ yanatokana na kundi dogo la watu………. Watu milioni 70 tunabagazwa na kuuawa na kundi halizidi watu 100.