Usiku kama saiv mlishazoea mnachat WhatsApp na normal text kwa wakati mmoja, ukituma text moja anajibu tatu. Tena akichelewa hata dakika mbili kujibu text anasema SORRY.
Mara kakutumia vikopa kopa, mara akupe umbea.
Saiv hana muda tena na wewe, ukituma text hajibu 😃💔
Ninatazama kwa makini nguvu ya AI na mitandao ya kijamii, hasa reels za Instagram na namna algorithimu zake zinavyofanya kazi. Ni kweli teknolojia imeleta manufaa makubwa, maarifa yanapatikana kwa urahisi, mawasiliano ni mepesi, na watu wanaweza kujifunza mambo mengi kwa muda mfupi. Hata hivyo, pamoja na faida hizo, kuna athari ambazo hazionekani kirahisi lakini ni za kina sana katika familia na ndoa. Leo hii, watu wengi wanategemea mitandao ya kijamii kama chanzo kikuu cha ushauri kuhusu malezi, mahusiano na ndoa. Tatizo ni kwamba algorithimu hazilengi kukuza hekima, zinakusukumia zaidi kile unachopenda kusikia au kile kinachochochea hisia zako. Ukianza kutazama maudhui ya kulaumu au kujitetea, utaendelea kuonyeshwa hayo hayo. Polepole, mtu anajikuta akiishi ndani ya mtazamo mmoja tu, bila kujitathmini au kusikiliza upande mwingine.
Kwa namna hii, maadili muhimu kama uvumilivu, heshima, adabu na mazungumzo ya ana kwa ana vinaanza kufifia katika maisha halisi. Migogoro midogo inakuwa mikubwa kwa sababu kila mmoja anapata uthibitisho wa mtazamo wake mtandaoni badala ya kutafuta suluhu ndani ya familia. Hili ni tatizo kubwa, lakini si rahisi kuliona isipokuwa uwe na mazoea ya kufikiri kwa kina na kuhoji unachokula kila siku kupitia skrini. Teknolojia si adui , tatizo ni pale inapochukua nafasi ya busara, maadili na mwongozo wa kweli katika maisha na familia.