Karibu Mirror Online TV, kwa Habari za Burudani, Michezo na Siasa.
🤏 Twitter : Facebook : YouTube : Mirror TV
✍Ukweli Uliothibitishwa
[email protected]
TANZANIA MAFUTA BEI RAHISI, KULIKO MAREKANI
"Watu wanalalamika kuhusu bei ya mafuta ya hapa Tanzania, juzi nimetoka Marekani bei ya mafuta yako juu kuliko Tanzania" - Rais @SuluhuSamia
BREAKING NEWS : Aliyewahi Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Camilius Membe Amefariki Dunia Leo Asubuhi Katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni Jijini Dar es salaam.
SHEIKH MUSSA AONDOLEWA
Baraza la Ulamaa la BAKWATA lililokutana kwa siku mbili DSM, limetengua uteuzi wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum kuanzia leo Alhamisi, Februari 2, 2023.
Aliyeteuliwa Sheikh Walid Alhad Omar kukaimu.
"Wakati wa Rais Magufuli,Dkt.Bashiru huyu alikuwa anatupa maelekezo rasmi wabunge wa CCM kumsifia Rais, ndio maana mlikuwa mnatuona Bungeni tunasifia sana,leo anachukia Rais @SuluhuSamia kusifiwa? kama hana agenda ya siri kwanini achukizwe na sisi kumsifia Rais?" Mbunge Lusinde
IKULU CHAMWINO IMEKAMILIKA
Ujenzi wa Ikulu ya Tanzania wilayani Chamwino, Dodoma umekamilika kwa 100%, ikiwa ni miaka 2.9 tangu ulipoanza. Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema ni fahari kwa vijana wake kujenga jengo hilo na ni jambo zuri kiusalama.
WAZIRI MKUU NA MAWAZIRI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 08, 2022 ameongoza kikao kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na baadhi ya watendaji wa Serikali kwenye ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE WAAGWA
Wafanyakazi wanne wa MDH na mmoja wa taasisi ya chakula la Lishe, waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege Bukoba waagwa Dar
AZIZ KI, CHAMA WAFUNGIWA
Mchezají wa timu ya Yanga, Stephan Aziz Ki na clatous Chama wa Simba wamefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faíni ya Sh. 500,000 kwa kosa la kukwepa kusalimíana na wachezaji wa timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo wa dabi ya Kariakoo.
SITA WAFARIKI DUNIA
Watu sita wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa wilayani Kiteto, Manyara baada ya gari la wagonjwa la Kituo cha Afya Sunya kugongana na Prado usiku wa kuamkia leo eneo la Pori Namba Moja. Wote waliofariki walikuwemo ndani ya gari la kubeba wagonjwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumapili Novemba 6, 2022 amewasili Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia Ndege ya Precision Air kupata ajali ilipokuwa ikikaribia kutua uwanja wa ndege wa Bukoba.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewajulia hali wahanga wa ajali.
AJALI YA NDEGE BUKOBA
Ndege ya Precision Air imepata dhoruba wakati ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba, hivyo kutua ndani ya Ziwa Victoria.
Taarifa kutoka mkoani Kagera zinaeleza kuwa kuna kuna mvua na ukungu.
KESI YA WABUNGE 19
"Vyama vinaua ndoto nashangaa sana niliahidiwa kuwa Mbunge nilikuwa na Mwenyekiti na Katibu mkuu wa Chama, hata mipango yote ya kutoka gerezani ilipangwa na Mwenyekiti @freemanmbowetz na Katibu mkuu wa Chama @jjmnyika sasa leo inakuwaje? - Hanje
NENO 'WALA MIHOGO' LAMUIBUA RAIS WA YANGA
"Kuna watu wanaitumia kauli yangu niliyoitoa Mwanza (Wala Mihogo) kuwakejeli WanaYanga, naombeni WanaYanga muwapuuze wanaotumia kauli yangu kuwa kejeli, niliitoa ili kujenga mshikamano ndani ya Klabu Yetu" - @Caamil8 Rais wa Yanga
RAIS SAMIA CHINA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Peking, Beijing nchini China kwa ajili ya ziara ya Kiserikali tarehe 02 Novemba, 2022
WAZIRI MKUU NA BALOZI WA QATAR
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 2, 2022 amezungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania, Hussein Bin Ahmad Al Homaid, Ofisini kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam
BREAKING NEWS : Rais @SuluhuSamia ametangaza Tanzania kuna Jumla ya wananchi Milioni 61.7
"Ninawatangazia rasmi kuwa Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120."
RAIS SAMIA KWENDA CHINA
Rais @SuluhuSamia anatarajiwa kufanya ziara ya kitaifa nchini China kuanzia Novemba 2 hadi 4 mwaka huu kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping, Ubalozi wa Tanzania nchini China umeeleza.
MKUU WA MKOA AUTAFUTA URAIS
"Leo unaweza kumkuta Mkuu wa Mkoa anahangaika kutengeneza njia na makundi ya kampeni ya uchaguzi wa mwaka 2025 kwa ajili ya kumtoa aliyekuteua, huu ni ujinga ambao haupo katika kundi lolote" Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Kagera
PONGEZI KWA RAIS WA CHINA
"Pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa China Xi Jinping, kwa kuchaguliwa tena kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP)." - Rais @SuluhuSamia