Taarifa kwa umma .
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Bukoba Manispaa na Meya Mstaafu wa Manispaa ya Bukoba Chief Karumuna amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku huu akiwa nyumbani kwake. Tunafatilia kujua sababu za kukamatwa.
Zacharia Obad
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria.
1. Anaitwa Jerison Keraliyo
2. Umri miaka 18
3. Mkazi wa Kata ya Kishiri
4. Mtaa Kishiri B
5. Wilaya Nyamaba
6. Alitekwa tarehe 9.10.2025 saa 6:30 jioni.
7. Gari iliyombeba Land Cruise
Mwanzo 4:1-16 kuna hadithi ya Caini na Abel. Hawa ni watoto wa Adam na Eva.Kaini alimiumua nduguye Abel. Bwana akamuuliza Kaini yuko wapi ndugu yako? Kaini akajibu sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu? Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
Kila mtanzania leo analala na wenge la kama kesho ataamka.
HOFU YA KUTEKWA imetanda kwenye taifa.
Leo hii watanzania anaejua kesho yetu sio MUNGU tena, ni SAMIA NA WAKINA MAFWELE. Hawa ndio wanaamua nani aishi leo na nani wampoteze kesho.
Angalau tumepata mwanga baada ya kumsikia “Capteni TESHA” kwamba jeshi letu sisi wananchi lipo Upande wetu wananchi. Kwamba ndugu zetu huko mipakani wanakolinda nchi isivamiwe na maadui kutoka nje wapo na sisi.
Mioyo ya wazazi wetu sisi ambao tufanya HARAKATI imejawa na presha, wakiamka simu ya kwanza ni kujua kama tumeamka salama watoto wao. Wanatushawishi kila njia tuachane na hizi harakati za UKOMBOZI ila wanashindwa kwasababu ya misimamo yetu iliyopo ndani mwetu kuwa “LAZIMA TULIKOMBOE HILI TAIFA”.
Haya mambo yanaumiza sana, ila Mungu anasikia vilio vyetu, na Mungu ni MUNGU wa HAKI—TUTASHINDA. Jipe moyo haya yote yanapita na mwisho wake ni USHINDI.
Usiku mwema kila mpambanaji.🙏🏿🇹🇿
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
“Kulinda uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maana yake ni kulinda wananchi”
Kwa wasioijua historia ya JWTZ - jeshi letu lilisukwa upya 1964 na kuitwa Jeshi la Wananchi kwa sababu mahsusi kabisa
Na hii mjue ndo sababu kubwa itabaki kuwa la wananchi! Na si kulinda ofisi moja au kikundi kidogo cha watawala wanaotuteka 😓
Kwa hiyo makatili madhulmat msitutishe na jeshi letu! Kiapo cha JWTZ ni kwa wananchi na wao ni watoto wa wananchi si watoto wenu!
Na #WenyeNchiWananchi
#TutaelewanaTu
Ni aibu kwa vijana kufoleni kupokea rushwa ya T.shirt
KUTOKA KWA MTUMISHI WA MUNGU APOSTLE Mtalemwa Dionis Rweyemamu
NI AIBU KIJANA KUUZA HAKI ZA MABILIONI KWA TSHIRT, BAISKELI AU PIKIPIKI, KULISHWA NYAMA.
Naona Balozi Polepole jana kaongea mengi ila kamwambia @SuluhuSamia kuwa anamweleza ukweli wala si chuki au fitna!
Ukweli ni kuwa hakubaliki kabisaaa 💯 hata ndani ya CCM ila hawamwambii waliomzunguka!
Na kila kiongozi wa umma anayeishi kwa kodi za wananchi awe HUMBLE na aache kutumia dola kuumiza mtu kisa kukosolewa!
#TutaelewanaTu
Sweta lake alilovaa limeandikwa gari la Mungu. Mungu atamlipia kisasi kikubwa sana. Look at this guy !! Jamani , alikuwa ana hatari gani huyu mtoto kwa usalama wa Nchi ? Why ? Halafu mnauliza hasira za wananchi zinatoka wapi ?
Kutoka kwa @MalisaGJ_ 👇
Habari za leo? Naomba utusaidie kupaza sauti kuhusu huyu mtoto. Jana amepigwa kisha baadaye akachomwa moto na kufariki kwa kudaiwa kuiba parachichi. Ni mtoto wa jirani yangu hapa Don Bosco Iringa, ana umri wa miaka 14 tu. Mama yao alifariki akaacha watoto watatu. Huyo aliyeuawa, amemaliza darasa la 7 mwaka jana na ana ndugu zake wawili.
Wana maisha magumu sana toka mama yao alipofariki. Kupata chakula tu ni mtihani. Hata hizo parachichi hakwenda kuuza, alikua anatafuta chakula chake na ndugu zake. Lakini nimesikitika akina mama wanaozaa kwa uchungu wamempiga marungu na kumchoma moto hadi kufa. Inauma sana. Tuombe Mungu atusaidie tusife tukawaacha watoto wetu wakiwa bado wadogo, wakapitia changamoto kama hizi.!
Kigoma Mjini, CCM ina wagombea wawili, Samia ameshindwa kumuombea Kura baba Levo amesema Mgombea wa mwingine naye mwanaye , ila vyovyote vili itakuwa CCM HOYEEEEE
Kuna mtu hajaelewa hiyo KODI ya Samia kusema wagombea wote wanaye ila kikubwa CCM HOYEE
Inaweza kuwa CCM OYEE kama mwanae mmoja sio wa CCM ?
Hongereni sana wananchi kwa kuonyesha rangi zenu na kusimama upande wa HAKI. Mlichokifanya ni faraja kubwa kwa Tundu Lissu ambaye yupo gerezani kwa sababu ya kusimama upande wa HAKI. Hii ni chachu ya ukombozi. Tusirudi nyuma. Tukatae kuwa nyumbu na wajinga.
Tundu Antipas Mugway Lissu siyo wakili tuu anayejua kuongea na kupanga hoja.
Kwasanaa ya sheria watu wa namna hii huwa tunawaita "Legal Maneac" ni watu wenye ueledi wa kina na ubobevu ambao huwezi kuupata Darasani... NI CHUO KIKUU CHA HIYARI CHA TAFAKURI ZA KISHERIA.
BAK Mwabukusi.
Mimi na wezangu tukiwa kanisa la Kirumba Mwanza tulikamatwa na @tanpol na kupelekwa kituo cha Polisi Kirumba. Tuhuma : KUFANYA FUJO.
Serikali ya CCM haitaki tuwaombee ndugu na jamaa zetu. Inatuumiza lakini haitaki tulie na kusali.
Hali ya nchi yetu ni dhoofu sana.