Professional Journalist- ITV /Radio One 2002-2015/To date 2025-2030 MP ( special seat ) Morogoro Region l ChairPerson PAC | Vice Chairperson- CHAUMMA .
Tunamshukuru Mungu leo 12/8 nikiwa na mgombea Urais mhe Salum Mwalimu Tumechukua fomu Tunakileta kwenu rasmi Chaumma mkiunge mkono tukafanye mabadiliko makubwa ya kupata Katiba mpya na sheria nzuri zitakazolinda Haki za watu .
Kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, Mgombea Makamu wa Rais Mheshimiwa Devota Minja ameendelea na shughuli za kampeni ambako leo hii Oktoba 24 amefanya mikutano mikubwa miwili kwenye majimbo ya Kinondoni na Mbagala.
Mheshimiwa Devota amenadi ilani ya CHAUMMA huku akiwaomba wananchi wakipe dhamana ya kuongoza nchi Chama cha Ukombozi wa Umma katika ngazi zote wakiwemo wagombea ubunge Moza Ally wa Kinondoni, Khadija Mwago wa Mbagala.
Mheshimiwa Devota pia amewaeleza wananchi kuwa na matarajio ya kesho mpya chini ya CHAUMMA na kuahidi kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakumba Watanzania.
#UwakilishiMakini
Uthubutu wetu leo ni msingi wa kesho bora ambayo tunaweza kujivunia.
Asanteni wananchi wa Ilemela na Nyamagana kwa imani yenu kwa @ChaummaT. Oktoba 29 kila mmoja wetu akapige kura ya ukombozi.
#UwakilishiMakini
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, mwanasiasa nguli Raila Odinga.
Pole nyingi kwa Wakenya na kila mmoja aliyeguswa na msiba huu mkubwa.
#RIPRailaOdinga
Mgombea Uraisi kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma CHAUMMA Mh.Salum Mwalim Leo October 7,2025 Ameendelea na Kampeni zake Feri,Jijini Dar es salaam kwenye Jimbo la Kigamboni.
Mwalim amesema endapo atapewa ridhaa atahakikisha kufutaa tozo Za kuvuka daraja la Kigamboni.
#UwakilishiMakini
#Chaumma2025