Kuna siku hutajisikia kuomba.
Kuna siku hutakuwa na nguvu ya kufanya kazi.
Kuna siku utataka kurudi kwenye tabia zako za zamani.
Ndipo unapohitaji nidhamu kuliko hisia.
Usisubiri motivation kila siku.
Jenga utaratibu ambao utaendelea hata siku ambazo hujisikii.
GIRISHONI amefanya niipakue hii makala, tusikilize wote.
Wote sasa tukatazame makala ya BBC AFRICA EYE ya mwaka 2026 inaangazia mapambano ya kisiasa ya Tundu Lissu na jaribio la mauaji dhidi yake la mwaka 2017, ikionyesha juhudi zake zinazoendelea za kudai mageuzi ya mfumo wa uchaguzi nchini Tanzania licha ya kukabiliwa na mashtaka ya uhaini aliyopewa mwaka 2025.
Halafu baadae tutapata muda wa kujadili kipeperushi cha Serikali katili ya CCM kilichotolewa na GIRISHONI.
Big failure, ni aibu hata kutangaza. Yaani , mauzo yote ya SABASABA sawa na zawadi ya sendoff KATORO. Uchumi hauko sawa hata kidogo. Rekebisheni siasa za Nchi zinavyoendelea kabla majuto hayajawa makubwa zaidi. Mitaani kuko vibaya sana.
Jude anaweza asiwe a very talented player ila jamaa ana kitu kinaitwa "Work ethic"
Hata siku hayupo vizuri he still shows up.
Hii ndio mentality ya mtoto wa kiume.
Leo IMF na Benki ya Dunia wametoa ripoti mbili muhimu sana. Nilichokiona ni kwamba, taasisi hizi mbili zimefika kwenye hitimisho moja. Dunia imebadilika, lakini Afrika bado haijabadilika kwa kasi inayotakiwa.
IMF inasema:
- Afrika sasa haishindani na Ulaya. Inashindana na Asia.
- Mapinduzi ya AI, semiconductors na data centres yanafanyika nje ya Afrika.
- Bara linakosa productivity revolution. Uchumi unakua, lakini uzalishaji wa kila mfanyakazi bado ni mdogo.
- Bei za chakula na mafuta zinaendelea kuliumiza bara kuliko maeneo mengi duniani.
- Misaada inapungua wakati mahitaji yanaongezeka.
Benki ya Dunia inasema:
- Hakuna nchi ya Afrika iliyopanda daraja la kipato mwaka huu.
- Afrika inazalisha utajiri, lakini Waafrika wengi hawaongezi kipato kwa kasi hiyo.
- Maliasili peke yake hazitoshi. Manufacturing, exports na taasisi imara ndizo zinazopandisha uchumi.
- Nchi nyingi zimekwama kwenye Lower Middle Income Trap.
- Changamoto kubwa ya Afrika siyo umasikini. Ni uzalishaji mdogo.
Kwa kifupi, taasisi hizi mbili zinasema jambo lilelile kwa lugha tofauti.
Karne iliyopita waliokuwa na maliasili walipata tija. Karne hii inawalipa wanaozalisha zaidi kwa kila mfanyakazi, wanaongeza thamani ya bidhaa zao, na wanaojenga taasisi imara.
Hapo ndipo mjadala wa kweli wa maendeleo ya Afrika unapaswa kuanzia.
Mambo yamesimama kisa kesho, msipotafuta majibu ya tar 29/10 mtaendelea kuviziana na watu kila siku, malizeni mambo mapema watu wafanye kazi hadi 2030.