Important to Note in the Marketing
1. Know who is your customer
2. Know what they really want.. and why
3. Know where to find them
4. Know how to get and keep their attention
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameungana na waumini mbalimbali kushiriki Ibada ya Jumatano ya Majivu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu, Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma leo tarehe 18 Februari 2026.
Ibada hiyo, imeongozwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dodoma, Wilbroad Kibozi.
Akitoa mahubiri katika Ibada hiyo, Askofu Kibozi, amewasihi waamini kutumia kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma, kujitoa kwaajili ya wahitaji pamoja na kuombea familia, vijana, watoto na Taifa kwa ujumla.
Pia amesema katika kipindi hiki ambacho waumini wa Dini ya Kikristo na Kiislamu wanakutana pamoja katika mfungo, ni vema kupendana, kuheshimiana na kujaliana.
Askofu Kibozi amesema wafanyabiashara wanapaswa kuwa wema na wakarimu katika kipindi hiki na kutambua kipindi hiki sio cha upandishaji bei ya bidhaa za vyakula bali inapaswa bei za bidhaa kupunguzwa.
Ibada ya Jumatano ya Majivu ni mwanzo wa kipindi cha Kwaresma ambacho hutumika na waumini wa Dini ya Kikristo kwaajili ya mfungo.
Unatafuta nguo za Kiume, Casual zimetulia, hazina rangi za kupitiliza, na hazibanduki zikiguswa na pasi?
Chimbo lipo Kkoo!
Code kali, ubora wa kuaminika, bei za Kizalendo.
Piga +255755328132 sasa. Boresha muonekano wako, tufiche shida kidogo 🤛🏼
📍 Dodoma
▪️SERIKALI YATOA MWONGOZO WA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026.
Serikali imetoa mwongozo rasmi wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa mwaka 2026, yatakayofanyika kuanzia Machi 1 hadi 8 kote nchini.
Hayo yamebainishwa Februari 17, 2026 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, ambapo amesema maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa yakiongozwa na mwongozo maalum uliotolewa na Wizara.
Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2026 ni “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”, ikilenga kujenga uelewa wa kuwekeza katika maendeleo jumuishi kwa kutambua na kutekeleza haki za wanawake na wasichana kwa vitendo.
Amesisitiza kuwa kaulimbiu hiyo imejikita katika nguzo za Dira ya Taifa ya 2050 na inahusisha makundi yote ya kijamii.
Katika mwongozo huo, Waziri Dkt. Gwajima ameeleza kuwa kila mkoa utawajibika kuratibu maadhimisho na kutoa taarifa kwa umma kuhusu ratiba na maudhui ya shughuli zitakazofanyika. Aidha, sare rasmi ya maadhimisho itakuwa vazi la batiki, ambapo kila mkoa utahamasishwa kutumia wazalishaji wa ndani ili kuinua uchumi wa wajasiriamali wa ndani, hususan wanawake.
Amefafanua kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanajengwa juu ya misingi ya Ulingo wa Beijing wa mwaka 1995 unaolenga kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kupitia ajenda 12 muhimu, ikiwemo kupinga umaskini, ukatili wa kijinsia, kuboresha afya na elimu, pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na uchumi.
Aidha, amesema maadhimisho hayo yatahusisha midahalo, makongamano, maonesho ya wajasiriamali, uzinduzi wa miradi ya kijamii, mashindano ya kielimu na michezo ya kuelimisha, utoaji wa tuzo kwa wanawake vinara pamoja na matembezi ya hiari siku ya kilele. Pia, wananchi wataelimishwa kuhusu huduma za msaada wa kisheria, uwezeshaji wa kiuchumi na maadili ya jamii.
Waziri Dkt. Gwajima amesisitiza kuwa maadhimisho hayo hayahusiani na itikadi yoyote bali ni ya wanawake wote kwa kushirikiana na wanaume kama wadau wakuu wa maendeleo. Amevitaka vyombo vya habari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha taarifa za maadhimisho zinawafikia wananchi wote, huku akibainisha kuwa Wizara itaungana na Mkoa wa Geita katika maadhimisho hayo na tathmini ya ushiriki wa mikoa itatolewa Machi 30, 2026.
MWISHO
Nawatakia Waislamu wote kheri na mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tusujudu kwa shukrani mbele za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujalia neema adhimu ya kuufikia tena mwezi huu katika imani. Tunapotekeleza nguzo hii muhimu, tumwombe atujalie kudumu katika ibada na upendo kwake na jamii na akaipokee funga yetu. Katika kufunga na kusujudu mbele zake sote tuendelee kuiombea nchi yetu amani, umoja, mshikamano na ustawi kwa wote.
Ramadan Mubarak!
Tafakari
Qur'ani Tukufu Sura Al-Baqara 183
“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.”
RAIS SAMIA ATEULIWA KUWA KINARA WA UMOJA WA AFRIKA KATIKA AFYA YA UZAZI, MAMA NA MTOTO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, @SuluhuSamia ameteuliwa kuwa Kinara wa Umoja wa Afrika katika masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahmoud Thabit Kombo, tarehe Februari 16, 2026, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Waziri Kombo amesema uteuzi huo umefanywa na Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika, ukitambua juhudi na uongozi wa Rais Samia katika kupambana na kupunguza vifo vya mama na mtoto nchini Tanzania. Kupitia nafasi hiyo, Rais Samia atakuwa na jukumu la kuhamasisha nchi wanachama kushirikiana, kubadilishana uzoefu, pamoja na kufanya tathmini za mara kwa mara kuhusu maendeleo ya sekta ya afya ya uzazi, mama na mtoto barani Afrika.
Ameeleza kuwa uteuzi huo unaendelea kuifanya Tanzania kuonesha dhamira ya dhati ya kuchangia uongozi wa Bara la Afrika katika kujenga mifumo imara ya afya inayolinda haki ya kila mwanamke na mtoto kupata huduma bora na salama.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Seif Shekalaghe, amesema Rais Samia alianza kuonesha dhamira thabiti ya kupunguza vifo vya mama na mtoto tangu mwaka 2016 alipokuwa Makamu wa Rais. Amefafanua kuwa kupitia kampeni ya kuzuia vifo vya mama na mtoto iliyoanzishwa chini ya uongozi wake, Tanzania imepiga hatua kubwa ambapo kiwango cha vifo vya uzazi kimepungua kutoka takribani vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2022.
Dkt. Shekalaghe amesema mafanikio hayo yametokana na msisitizo, ufuatiliaji wa karibu na uwajibikaji katika utekelezaji wa ajenda ya afya ya uzazi, akisisitiza kuwa uteuzi wa Rais Samia ni heshima kubwa kwa Taifa na chachu ya kuimarisha zaidi huduma za afya ya uzazi nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
#TanzaniaYetuSote #NchiYetuKwanza #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
🌙Ramadhani Mubarak! Ubalozi wa Marekani unawatakia heri wale wote wanaoadhimisha mwezi huu mtukufu. Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uwe ni wakati wa amani, tafakari na toba, ukileta na kuongeza umoja, huruma na ustawi kwenu na kwa wapendwa wenu. Ramadhani Kareem!
Fanya biashara bila makato.
Tumia huduma zote za CRDB ukiwa na uhakika hela yako haipungui.
Utapata pia na
✅ Mkopo wa 50M
✅ Lipa Hapa
✅ TemboCard
#BenkiKimpangoWako
#TaifaKwanza#KataaVurugu
Kuchaguliwa kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) ni kielelezo tosha na majibu dhidi ya propaganda chafu dhidi ya Taifa letu zinazofanywa na Wanaharakati Uchwara wanaoishi nje ya nchi kwa kushirikiana na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki futari na makundi mbalimbali ya wananchi katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Ikulu ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 19 Februari, 2026.
___
#KaziNaUtuTunasongaMbele#TabasamuLaUtu#MaendeleoEndelevu
Mazoea Hayaa.
Nimefika Makumbusho Nimeingia Hotelini Nimeagiza Supu na Vitafunwa na Juice.
Vitu Vishaaletwa Naenda Kunawa Mikono nakumbuka Nimefunga.
Wakuu Hii Kwenye Dini Tunafanyaje Niwaombe Warudishe, Au Nilipie ti Niwape Vitu Vyaoo au Nile tu..?
Share your Comments.
📍 Dar es Salaam
▪️USHIRIKIANO WA TANZANIA NA QATAR WAIMARIKA KATIKA MICHEZO NA UWEKEZAJI
Mkutano muhimu ulifanyika tarehe 16 Februari 2026 katika Ubalozi wa Taifa la Qatar, Dar es Salaam, ukimkutanisha Balozi wa Qatar Bw. Ahmed Abdulla Al-Dossari na Mheshimiwa Paul Christian Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania. Mheshimiwa Waziri alieleza shukrani za Serikali kwa uhusiano imara uliopo kati ya mataifa hayo mawili, akisisitiza kuwa ushirikiano huo umeendelea kuzaa matokeo chanya katika sekta za maendeleo, uwekezaji na diplomasia ya kimkakati.
Katika mazungumzo hayo, Waziri aliwasilisha rasmi maandalizi ya Tanzania kuelekea kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika 2027, akibainisha fursa za uwekezaji katika miundombinu ya hoteli jijini Arusha, uboreshaji wa viwanja vya mpira wa miguu, pamoja na kukuza sekta ya utalii. Alisisitiza umuhimu wa kunufaika na uzoefu wa Qatar uliopatikana wakati wa kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2022, tukio lililotambulika kimataifa kwa ubora wa miundombinu, usimamizi na mchango wake mkubwa katika uchumi na maendeleo ya sekta ya michezo.
Kwa upande wake, Balozi wa Qatar Bw. Ahmed Abdulla Al-Dossari alithibitisha dhamira ya kuendeleza ushirikiano huo kupitia kubadilishana uzoefu, kuimarisha ziara za kikazi, na kufuatilia mapendekezo yaliyowasilishwa kwa hatua za utekelezaji. Pande zote mbili zilikubaliana kuharakisha mchakato wa makubaliano rasmi na kuendeleza miradi ya pamoja itakayochochea maendeleo ya michezo, utamaduni, utalii na uwekezaji, hatua inayotarajiwa kuongeza thamani ya kimkakati na kiuchumi kwa mataifa yote mawili.
Ninawatakia Wakristo wote Kwaresma njema na yenye baraka. Safari hii muhimu kiimani kwenu mnayoianza leo kwa ibada ya Jumatano ya Majivu iwe fursa ya kutafakari, kuendelea kuimarisha uhusiano na Mwenyezi Mungu; na kudumu katika ibada, kuiombea nchi yetu amani, umoja, mshikamano na ustawi kwa wote. Mwenyezi Mungu azipokee funga, sala na sadaka zenu na awakirimie mema yote mnayomuomba kwa mtu mmoja mmoja, familia, ndugu, jamaa, marafiki na Taifa kwa ujumla.
Tafakari
Biblia Takatifu Yoeli 2:12-13
“Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.”
📍Free Online Webinar
Join us on 19–20 February 2026 for a powerful online kickoff under the theme: “Conducting AI Literacy for Technical and Non-Technical Audiences.”
🕒 1500–1700 HRS (EAT)
💻 Zoom Meeting
🎟 Free Entrance (Certificate: 20,000 TZS / $20)
Let’s build AI knowledge for everyone. Register here: https://t.co/1YYF5Idetc
USHIRIKIANO WA TANZANIA NA MAREKANI WAZIDI KUIMARIKA, MIRADI MIKUBWA YA KIMKAKATI KUJA HIVI KARIBUNI.
Katika mkutano baina ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia na Kaimu Balozi wa Marekani, Andrew Lentz, uliofanyika Desemba 08, 2025 uliangazia kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kimkakati kati ya mataifa mawili.
Mazungumzo hayo yameibua upya dhamira ya kujenga ushirikiano wa kisasa unaoweka mbele manufaa ya pamoja, ustawi pamoja na kuimarisha biashara, uwekezaji na usalama wa muda mrefu.
Katika mkutano huo, Marekani imesisitiza utayari wa kushirikiana na Tanzania kwenye utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo (1) Mradi wa LNG wenye thamani ya USD Bilioni 42 utakaoiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kama msambazaji mkubwa wa gesi asilia, Mradi wa Tembo Nickel – Ngara (USD Milioni 942) unaolenga kuzalisha Nickel kwa betri za magari ya umeme na kuimarisha mnyororo wa nishati safi; pamoja na (3) Mradi wa Mahenge Graphite (USD Milioni 300) utakaoifanya Tanzania kuwa mtoa huduma muhimu wa malighafi za betri na nishati mbadala duniani.
Ushirikiano huu unaendelea kuijenga Tanzania kama kitovu cha uchumi wa kisasa na nishati safi barani Afrika. #DiraYaSamia @ikulumawasliano
Msimu wa kufurahia na familia umefika!
Mwajiri, lipa wafanyakazi wako mapema na kwa urahisi kupitia CRDB Internet Banking
Huu ndio ule mshahara unaopaswa kutunzwa hadi February… lakini unajua utakavyopotea 😂
#TushavukaHuko
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Ivan Lancaric, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 11 Desemba 2025.