Ewe Mola, hakika Wewe ni mwingi wa kusamehe, unapenda kusamehe, basi nisamehe.
Ewe Mola, uturehemu juu ya ardhi, chini ya ardhi, na siku ya kusimamishwa mbele yako.
Ni dua yenye maana nzito sana, inatufundisha kumuomba Mwenyezi Mungu rehema.
Hii aya inazungumzia hali ya mtu anapokaribia kufa, wakati roho yake inakaribia kutoka, lakini bado hakuna wa kuizuia, na hakuna atakayemsaidia ila Mwenyezi Mungu tu.
Yaani watu waliomzunguka mgonjwa wanatafuta mganga au mponyaji, lakini hakuna wa kuizuia roho isichukuliwe.
Kioo kinachomsaidia dereva kutazama mbele ni kikubwa kuliko vioo viwili vya pembeni vinavyomsaidia kuangalia nyuma..
Tutumie nguvu nyingi kuangalia tunakokwenda kuliko tulikotoka
Nyuma pangekuwa muhimu Mungu angetuwekea macho kisogoni..📌📌