#TajiriLaKihaya
Kwenye hii Issue ya Kariakoo mm na BlueTick yangu nitasema hivi;
Pale kariakoo asilimia kubwa ya wenye Ardhi hawakua na hela ya kujenga ghorofa…
Iliwabidi wawekezaji wachukue fursa, wanamfata mwenye Ardhi wanaingia mkataba..
Kwa mfano; Tajiri anajenga ghorofa alafu Atarudisha expense za ujenzi lets say for 10yrs bila kulipa rent- after 10yrs either atairudisha kwa mwenye ardhi au aanze kulipa kodi kwa walivyokubaliana…
Sasa huyu investor wakati wa ujenzi atafanya kila kitu kuhakikisha gharama za ujenzi zinakuwa ndogo- hata jenga nyumba imara saana akijua kwamba baada ya miaka 10 au miaka waliokubaliana haitakua ya kwake tena!
Matokeo yake Ratio ya cement inakua ndogo na hata cement inayotumika sio ile grade inayohitajika kwa ajili ya ghorofa, Nondo zinakua chini ya kiwango nk.
Au wengine wanauziana Floor… lets say mjengo ni ghorofa mbili mtu anauziwa ajenge Floor ya tatu!
Hii ndio mbaya zaidi, maana unapata mwanzo wakati ghorofa linajengwa BASEMENT iliwekwa ya uzito wa ghorofa mbili (materials nk) lakini kwa ajili ya tamaa - wanajenga ghorofa tatu hadi tano!
Mwisho wa siku inakua very weak💔
Sijui nataka kusemaje ila mwisho wa siku haya yote yanatokana na UFISADI NA UCHAWA uliopitiliza…
Ofisi zetu zilizopewa mamlaka ya kusimamia mambo kama haya hazifanyi kazi kwa UADILIFU!
Na matajiri wengi wanajificha kwenye chama tawala sio kwa sababu wanakipenda saana hapana… kwa minajili iwe rahisi kwao kupata shortcut na favor zisizo stahili!
Mtu akiwa mjumbe wa kamati kuu au hata mwanachama anaetambulika akienda ofisi ya umma amepiga kofia au shati la kijani jambo lake kupelekwa mbio mbio ni rahisi saana!
Au mtu akiwa na fedha- hebu fikiria mfano kupata passport tu inaweza chukua hadi miezi miwili kuipata- lakini kuna mtu passport anaweza kuipata ndani ya masaa 48.
Shortcut zinakuwa nyingi saaana💔 process hazifuatiliwi kabisaaa-