Wewe Msigwa unataka kucontrol CNN kama unavyocontrol leseni za online tv za Tanzania? Au unafikiri hilo ni gazeti unalotaka kufunga wakati wowote unaotaka?
Hao ulioenda kuhutubia hapo wamekuuliza mliua watu wangapi?
Je wamekuuliza kwanini hamjawapa Watanzania miili ya ndugu zao wakazike?
Wamekuuliza kwanini mlimpiga mama mia mzito risasi ya mgongoni?
Wamekuuliza kwanini majeruhi wamechukuliwa wakiwa wazima na kupelekwa Mortuary?
Unafikiri CNN, BBC, Al Jazeera wataachq kufanya kazi yao kwasababu wewe hupokei simu au haujibu msg?
Kwanini Leo haujawaalika CNN ili wapate nafasi ya kukuuliza maswali ujibu?
Wenye nia ovu ni nyie wauaji sio watu wanaoanika uovu wenu.
Ukatili wenu huu hamtaweza kufunika, kwa lolote.
Watanzania wa sasa sio wajinga.
MAANDAMANO DECEMBER 9!
MAANDAMANO DECEMBER 9!
MAANDAMANO DECEMBER 9!
MAANDAMANO DECEMBER 9!
MAANDAMANO DECEMBER 9!
MAANDAMANO DECEMBER 9!
MAANDAMANO DECEMBER 9!
Kabla ya kulala Retweet 🙏
Kama unasema kwamba vijana walilipwa kuandamana, unajua kwamba hao vijana walitoka Nchi jirani.
Unaunda hiyo inayoitwa tume ikafanye nini? Yaani unataka ikachunguze nini wakati wewe tayari unajua na unasema kwa uwazi?
Uelewa wa Watanzania wa sasa ni mkubwa sana.
Haya mambo hayahitaji propaganda na vitisho yanahitaji ukweli, ukweli huwa unajitetea wenyewe na hautaki kupuuzwa.
Ujumbe kutoka gerezani Ukonga wa Mh. Tundu Lissu
21/11/2025
Tume za Uchunguzi ni dekio la uchafu wa serikali na Jaji Mkuu Mohamed Chande ndiye msafishaji mkuu wa uchafu huo!!
Alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Mauaji Bonde la Ihefu mwaka 2006. Matokeo yake? Sifuri!!
Alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Vyombo vya Haki Jinai Mwaka 2023. Matokeo yake? Sifuri!!
Sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Mauaji Makubwa katika historia ya nchi yetu yote. Tutegemee matokeo gani? Sifuri!!
Hakuna Maridhiano bila Ukweli na Uwajibikaji!
Hakuna Amani bila Haki.
TAL, Ukonga Central Prison.
-Admin.
Anaitwa Larry madowo ni mzaliwa wa kijiji cha Mkadage wilayani Kilosa nchini Tanzania.
familia yake iliamia nchini kenya na kukana uraia wa Tanzania🇹🇿
itoshe kusema damu ni nzito kuliko maji
Tumpe Repost 300 kwa eshima 😊
Kwanini J.K Nyerere alibeba vita ya kupambania HAKI za majirani? Je, aliwapenda sana? Kwanini alikuwa tayari kuwapa majirani hadi msaada wa kivita kuhakikisha kimewaka? NITAKUTOA KAMASI KICHWANI.
Dar es Salaam ilikuwa ni sehemu ya HIJA kwa wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wanapigania uhuru kwao; South Africa, Mozambique, Angola, Zambia, Malawi na nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika.
Kutokana na msimamo wa serikali ya Tanganyika chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, nchi za Afrika ziliamua Tanganyika iwe Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika 1963.
Kamati ilikuwa ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU). 1963, Serikali ya Tanganyika chini ya Mwl, J.K. Nyerere ilitoa sehemu ambayo ilitumiwa na serikali ya kikoloni kama shamba; kuwa kambi ya wanajeshi.
Machi 30, 1959 ni siku hiyo, Serikali ya South Africa ilitangaza hali ya hatari na kuanza kuwaweka watu kizuizini, Sheria ya vyama visivyotambulika ilianzishwa na kupiga marufuku vyama vya PAC na ANC.
Mwl, Julius K Nyerere aliwapa hifadhi wapiganaji wa ANC kutoka South African na waliishi Mazimbu, Morogoro na Mbeya. Walifundishwa kupambana kijeshi dhidi ya mabeberu wakiwa katika ardhi ya Tanzania
Mwl, Julius Kambarage Nyerere, Machi 29, 1961 alimpokea, Phillip Kgosana ambaye aliwasili Dar-es-Salaam baada ya kutoroka kwa kukimbia South Africa kupitia Swaziland, Lesotho na Botswana.
Phillip Kgosana aliongoza wafuasi wa Pan Africanist Congress (PAC) kati ya waandamanaji 30,000 hadi 50,000 kutoka Langa na Nyanga hadi makao makuu ya polisi katika Caledon Square mjini Cape Town.
African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini kilipeleka baadhi ya watu wake wa kwanza waliojitolea kujifunza kupigana Kongwa. Waliita kundi lao la kijeshi Umkhonto we Sizwe (MK), yaani Mkuki wa Taifa.
Watu kutoka Afrika Kusini waliingia Tanzania kwa wingi kuanzia 1962. Walipitia Tanzania wakati wanaenda kupata mafunzo ya kivita. 1963 wengi wao walipita Tanzania na kwenda Russia kwa mafunzo.
Walianza kurudi Tanzania 1964 baada ya kufuzu. Muhimu kukumbusha kwamba hata hizo safari za kwenda nchi nyingine kupitia Tanzania, ziliwezeshwa kwa kupitia hati za kusafiria walizopewa na Serikali ya Tanzania.
1964 Pan Africanist Congress (PAC) ilihamisha makao yake makuu kutoka mjini Maseru, Lesotho walipokuwa wakifanya shughuli zao kisiasa zinazohusu siasa za South Africa hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania.
Baadhi ya wanajeshi wa Umkhonto we Sizwe (MK) wa Luthuli Detachment waliopigana Wankie Kampeni kule Zimbabwe pamoja na Zimbabwe African People’s Union (ZAPU) mwaka 1967, walikuwa Kongwa.
Uamuzi ulifanywa na serikali ya Tanganyika kufungua kambi ya wanajeshi Kongwa. Chama cha Namibia cha South West Africa People’s Organization (SWAPO), kilipeleka watu wake kwenye kambi ya Kongwa.
Kuanzia 1962, Sam Nujoma alifanya makubaliano na Serikali ya Tanganyika watu 200 kutoka Namibia waliojitolea waje Tanganyika, na kutoka hapo, waende nchi nyingine ili kupata mafunzo ya kijeshi.
Wengi walienda nchi za Egypt iliyokuwa chini ya Rais wake, Gamal Abdel Nasser kupata mafunzo ya kijeshi. Wengine walipelekwa Algeria mwaka 1963. Wengi wao walienda Kongwa walipomaliza mafunzo yao.
Wanajeshi wa kwanza kutoka Namibia kwenda Kongwa, walifika Aprili 1964. Waliendelea na mazoezi na mafunzo ya kivita. Waliohitimu walianza kufundisha wengine waliopelekwa moja kwa moja kutoka Namibia.
Mwaka 1965, vijana sita waliopata mafunzo ya kivita walirudi Namibia kwa siri na kuanza operesheni ya ukombozi. Miongoni mwao alikuwa Simeon Tshihungeleni na Johannes Otto Nankudhu.
Agosti 1966 kundi lingine lilipenya na kuingia Namibia. Lilikuwa kundi la kwanza kufyatua risasi ndani ya Namibia Agosti 1966; katika kundi hilo walikuwa Kongwa na silaha walizotumia walizipata Tanzania.
Mwl, Julius Kambarage Nyerere aliwapa hifadhi Samora Machel na Edward Mondlane. FRELIMO wameishi Musonya, Tunduru na Matchedje, Nyasa. Huko wameishi wakipewa mafunzo ya kijeshi kupambana msituni.
Wanajeshi kutoka Mozambique walianza kuingia Kongwa Aprili 1964. Katika kundi la kwanza alikuwamo Samora Machel. Alikuwa mmoja wa vijana waliopita Tanzania 1963 kwenda kupata mafunzo ya kijeshi Algeria.
Wanajeshi wa (Frente de Libertação de Moçambique - FRELIMO) na SWAPO waliungana na kukarabati jengo la shule na kulifanya jengo la kambi. Waliweka seng’enge kutenganisha kambi ya FRELIMO na SWAPO.
Chama cha FRELIMO kilianzishwa Dar es Salaam mwaka 1962 baada ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwaeleza viongozi wa vikundi mbalimbali lazima waungane kwa pamoja au waondoke Tanzania.
Ilipofika Mei 1964, wanajeshi wa SWAPO na FRELIMO wakatoka kwenye matenti na kuingia kwenye kambi waliyojenga- Kongwa. Wananchi wa maeneo ya Kongwa walijitolea kusaidia wanajeshi hao mwanzo.
FRELIMO, kulikuwa na wanajeshi zaidi ya 250 ilipofika Septemba 1964. Kundi la kwanza lilipenya kutoka Tanzania na kuingia Mozambique Septemba 1964. Risasi na bunduki walizotumia walivipata Tanzania.
Huu ndio ulikuwa mwanzo wa vita ya kuikomboa Mozambique. FRELIMO iliondoa wanajeshi wake Kongwa na kuwapeleka kambi nyingine ya Nachingwea 1966. Nachingwea ikawa kambi kubwa ya FRELIMO.
Vyama kutoka nchi ya Angola na Zimbabwe vilipeleka wapiganaji wake Kongwa. Chama cha Movimento Popular de Libertação de Angola (MPLA) cha Angola kilipeleka wanajeshi wake Kongwa mwaka 1965.
Baadhi ya wapiganaji wa kwanza wa MPLA waliofungua uwanja mpya wa mapambano mashariki ya Angola 1965 walikuwa Kongwa na baadaye Zambia. MPLA iliitumia Kongwa kama sehemu ya mafunzo ya kivita.
Hata wanajeshi wa National Union for the Total Independence of Angola (UNITA) walikuwa 11, walikaa Kongwa na wanajeshi wa SWAPO 1965 baada ya kufuzu mafunzo yao kutoka kwa Jamhuri ya China.
Wapiganaji wa Zimbabwe wa chama cha ZAPU ni miongoni wa wanajeshi waliofika Kongwa mwaka 1965. ZAPU haikuwa na wanajeshi wengi Kongwa; wanajeshi hao walihamishwa na kupelekwa Zambia.
Walipigana pamoja na MK kwenye Wankie Kampeni ya 1967. Wanajeshi wa Zimbabwe African National Union (ZANU) pia walikuwapo Kongwa, na baadaye walipelekwa kwenye kambi ya Itumbi iliyopo Chunya, Mbeya.
Na pia tukumbuke kuwa Kongwa haikuwa pekee yake katika kuhifadhi wapiganaji wa nchi za Aftika, kwani baadaye kambi nyingine zilifunguliwa Mgagao, SOMAFCO, Nachingwea, Bagamoyo na Itumbi.
Kwa hiyo, swali lako na hoja zako za KIPUMBAVU zinajibiwa na hizi shughuli za harakati ambazo Mwl, J.K Nyerere alizoendesha katika ardhi ya Tanzania ili kusaidia nchi za Affika kupata ukombozi wake.
Unashangaa nini kuwaona majirani katika JUMUIYA ya AFRIKA MASHARIKI wakiungana na Watanzania katika nyakati hizi ambazo waandamamaji wameuwawa kwa na hata idadi ya waliouwawa haitajwi na Serikali?
Vyombo vya habari vya ndani havielezi lolote kuhusu waliouwawa zaidi vinatumika kuonesha uharibifu wa mali. Msaada pekee wananchi wanapata ni kutoka kwa majieani, kwa haki zao kupaziwa sauti tu.
Jielimishe kidogo tu, ili uweze kupunguza kiasi cha kamasi katika ubongo. Haiwezekani ukawa mjinga na mpumbavu kwa wakati mmoja. Hakuna mashindano ya kuwa mjinga na mpumbavu. Karibu kama una swali.