Ee Bwana tunakuomba utuopoe katika maovu yote, utujalie kwa wema amani maishani mwetu, kusudi kwa msaada wa huruma yako, tuopolewe daima na dhambi, wala tusifadhaishwe na jambo lolote, tunapongojea kwa matumaini kurudi kwake Mkombozi wetu Yesu Kristo!🙏
Wazee wastaafu tuna haki kutoa mawazo yetu tuwe ndani au nje ya CCM. Umri tumepewa na Mungu asiyetenda kosa. Ni mamlaka kutafakari ushauri wetu na kuupokea au kuupuza au kuuboresha KIDEMOKRASIA. Badala ya kujibu hoja wanakuja machawa kutushambulia kwa propaganda za kashfa za uongo. Kwa nini hamupeleki tuhuma hizo nzito mahakamani? Miaka nenda, miaka rudi? Hamuwezi kutunyamazisha tunapotetea haki, ukweli misingi ya amani na maslahi mapana ya taifa na mustakabari wa vizazi vijavyo. Jamii inayojielewa inatambua hamjui mtendalo. KAJISAHIHISHE