Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu Prof. John Ruhangisa amesema hayo wakati akifanya mahojiano maalum ya kipindi cha Katiba Kitaa jijini Arusha.
#KatibaKitaa
Mahakama haziwi huru kwa kusahihisha madhara yaliyokwisha kutokea, uhuru wa kweli wa mahakama hupimwa kwa uwezo wake wa kuzuia dhulma kabla haijavaa sura ya sheria. Haki inayochelewa baada ya uharibifu kutokea si ushindi wa sheria, bali ni ukumbusho wa udhaifu wa taasisi zilizopaswa kulinda haki tangu mwanzo.
Kuna watu wana kipaji cha hali ya juu kabisa cha kujitoa ufahamu, kuongea upupu mchana kweupe kwa kujiamini asilimia mia moja, wakidhani Watanzania wote ni mbumbumbu wa kuamini kila wanachosema. Ni mchanganyiko wa ubinafsi, majivuno na ego uliopitiliza unaowasukuma kupuuza ukweli, kujiona wao pekee ndio wenye akili na maarifa, na kudharau uwezo wa Watanzania wa kuchambua na kutambua ukweli. Bahati mbaya kwao, kujiamini kupita kiasi hakubadilishi uongo kuwa ukweli, wala hakuwafanyi wengine kuwa wajinga.