Ukurasa namba 1 kwa afya yako! Chanzo aminika cha elimu, habari na kweli zote za afya; kila siku kwa lugha yetu pendwa ya kiswahili | Tufuatilie Sasa 👇
Kwa mujibu wa Tafiti Mbalimbali za Kimaabara, ulaji wa Stafeli unaweza kusaidia kupunguza hatari ya kupatwa na Saratani ya Matiti, Utumbo, Tumbo na Mapafu.
Hii inatokana na uwepo wa Kamikali za Acetogenins ambazo huharibu usafirishwaji wa Nishati inayotumiwa na Seli za Saratani katika kukua na kusambaa Mwilini.
Pia lina nyuzi lishe nyingi na maji vinavyosaidia mwili kuondoa Sumu na kuboresha Mmeng’enyo wa chakula, hivyo kuimarisha kinga ya Mwili.
Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, Prof. Mohamed Janabi alizungumza haya kama sehemu ya kuwakumbusha Watu umuhimu wa kutunza afya na kuishi Mtindo bora wa Maisha utakaosaidia kujilinda dhidi ya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza
Video: TBC
Mtama ni chakula chenye virutubisho muhimu kwa watoto. Una Nishati inayowasaidia kukua na kuwa na nguvu kwa shughuli za kila siku, na pia una Protini zinazochangia ukuaji wa mwili.
Una Madini chuma na Magnesiamu yanayosaidia kutengeneza damu na kuimarisha Mifupa. Hii husaidia mtoto kuepuka upungufu wa Damu na kuwa na afya bora.
Zaidi ya hayo, Mtama una nyuzi lishe zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula na kuzuia choo kigumu. Ni chakula rahisi, salama na chenye faida kwa watoto.
Unajua kuwa Mama kuwa Mkali sana ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuwa visababishi vya mtoto kupata 'Chango?'
Fuatana na Dkt. Jackline Urio, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto Kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili akifafanua baadhi ya visababishi vinavyoweza kupelekea Mtoto apatwe na hali hii.
Video: Muhimbili TV
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Momba, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Fidelia Kasongwa, amekamata gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 577 BNN, linalomilikiwa na Shule ya Msingi HQ iliyopo Tunduma, kwa kosa la kuwabeba wanafunzi 40 badala ya 15 kwa msongamano mkubwa, kinyume na Sheria na taratibu za Usalama barabarani.
Kujaza watoto wengi kwenye gari dogo si salama kwa afya zao kwani huwafanya wapumuliane, huwanyima Hewa ya kutosha, kusababisha wapate Joto kupita kiasi, Kizunguzungu, Kichefuchefu, Maumivu ya kichwa, Msongo wa mawazo na uchovu na wanaweza kusambaziana Magonjwa ya Kuambukiza kirahisi.
Kama ilivyo kwa watu wazima, Watoto hujitaji hewa Safi, Salama na ya Kutosha ili kukidhi mahitaji ya miili yao hivyo haki hii inapaswa kuheshimiwa na kila anayewahudumia, hata kama hawana uwezo wa Kujisemea wenyewe
Watoto wa kike wakijisaidia wanapaswa kusafishwa kutoka mbele kwenda nyuma ili kulinda afya ya sehemu za siri. Njia hii huzuia Bakteria kutoka sehemu ya haja kubwa kusogezwa kuelekea Uke au njia ya Mkojo, jambo linaloweza kusababisha maambukizi ya mara kwa mara hasa UTI
Aidha, inashauriwa kuwafundisha watoto usafi huu mapema ili wakue wakieleaa njia rahisi ya kuzuia maambukizi ya njia ya mkojo na Miwasho, na kujenga tabia sahihi ya usafi wanapokua.
Unajua njia unazoweza kutumia kutibu 'Chango' linalosumbua watoto?
Fuatana na Dkt. Jackline Urio, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto Kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili akifafanua baadhi ya njia unazoweza kutumia kuondoa hali hii
Video: Muhimbili TV
Watoto wachanga husumbuliwa na Chango (Colic) wanapokuwa na wastani wa umri wa wiki mbili au zaidi baada ya kuzaliwa. Chango ni maumivu makali ya tumbo anayopata mtoto na kulia mara kwa mara ikiwa Usiku, Mchana au Jioni.
Fuatana na Dkt. Jackline Urio, Bingwa wa Magonjwa ya Watoto Kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili akifafanua mambo unayopaswa kukagua kabla haujaamua kama Mtoto anasumbuliwa na Chango
Video: Muhimbili TV
Wanawake hasa wale wanaopata Allergy kirahisi wanashauriwa kutumia Pedi zisizo na rangi wala Manukato ili kulinda afya ya sehemu za siri.
Pedi zenye rangi au Manukato huwa na Kemikali zinazoweza kusababisha Muwasho, Vipele au Mzio (Allergy).
Pedi zisizo na rangi wala Manukato hupunguza pia hatari ya kupata maambukizi ya Fangasi na Bakteria, kwa sababu hazibadilishi mazingira ya Asili ya Uke.
P2 ni njia ya kuzuia Mimba inayopaswa kutumika kwenye mazingira ya Dharura pekee, na matumizi ya mara kwa mara yanaweza kumfanya Mwanamke adumaze afya yake ya Uzazi, kiasi cha kufanya apate Ugumu katika Kushika Ujauzito
Dkt. Living Colman
Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Hospitali ya Taifa Muhimbili
Video: Muhimbili TV
Wanawake waliojifungua wanashauriwa Kumyonyesha Mtoto ndani ya Masaa 24 ili kumuepusha asipate Umanjano, tatizo linalofanya Ngozi na Macho ya Mtoto yabadilike kuwa na rangi ya njano, hali inayohatarisha Maisha.
Ndealimbie Kileo, Muuguzi Mwandamizi Msaidizi, Hospitali ya Taifa Muhimbili
Video: Muhimbili TV
India imethibitisha visa viwili vya virusi vya Nipah katika Jimbo la West Bengal vikihusisha watumishi wa afya, na hatua za haraka zimechukuliwa kuwafuatilia watu wote waliokutana nao ili kudhibiti Maambukizi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa kwa sasa hatari ya virusi vya Nipah kusambaa kwa kiwango kikubwa ni ndogo, lakini limeitaka Jamii kuendelea kuwa makini kwani havina Chanjo wala Tiba Rasmi
Nipah ni Virusi hatari vinavyotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, hasa kupitia Popo. Dalili zake za awali ni Homa, Maumivu ya kichwa, Kutapika na Uchovu mkali, lakini zinaweza kuendelea hadi kusababisha maambukizi makali ya Ubongo, kupumua kwa shida, kupoteza fahamu na hata Kifo
Papai husaidia kuondoa changamoto ya Choo Kigumu kwa sababu lina Nyuzi lishe nyingi zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula kwa kuongeza ujazo wa Kinyesi na kukifanya kiwe laini, hivyo kurahisisha kutoka bila maumivu au kujikaza sana.
Pia papai lina kimeng’enya kinachoitwa Papain, ambacho husaidia kuvunja chakula tumboni na kufanya mmeng’enyo uwe rahisi zaidi. Hii hupunguza kukaa kwa chakula muda mrefu tumboni, hali inayochangia Choo kigumu.
Je, unajua matumizi makubwa ya Simu na Kompyuta yanaweza kukuleta madhara kwenye Afya ya Macho yako?
'Computer Vision Syndrome' ni matatizo ya Macho mtu anayoyapata akiwa anatumia vifaa vya elektroniki kama Simu na Kompyuta kwa muda wa masaa matatu na zaidi kwa umakini mkubwa. Msikilize Dkt. Jesca Lukinda, Daktari wa Macho Hospitali ya Taifa Muhimbili akifafanua jinsi ya kuepukana na Changamoto hii.
VIDEO: Muhimbili TV
Kufanya mazoezi kwa angalau dakika 150 kwa wiki ni muhimu sana kwa afya ya mwili. Kiasi hiki kinaweza kugawanywa, kwa mfano dakika 30 kwa siku kwa siku 5.
Mazoezi kama kutembea kwa kasi, Kuendesha Baiskeli, Kukimbia polepole, Kuruka Kamba au kucheza ngoma husaidia kuimarisha Mfumo wa Kinga, Moyo na Mapafu, na kupunguza hatari ya Magonjwa hasa yale yasiyo ya Kuambikiza kama Presha na Kisukari.
Mazoezi haya pia husaidia kudhibiti uzito wa mwili na kuboresha Mmeng’enyo wa chakula, Hupunguza Msongo wa mawazo pamoja na Kuboresha Usingizi
Watu wanaofanya 'Oral Sex' maarufu kama kuzama Chumvini wanaweza kupata maambukizi mbali mbali ya Magonjwa ya Zinaa Mdomoni na Kooni na kuwapelekea kupata Saratani ya Shingo ya Koo
Dkt. Baiya Kissiwa
Bingwa wa Magonjwa ya Uzazi na Kina Mama
VIDEO: Kalamu Media
Bamia huwa na Foliki Asidi inayosaidia ukuaji mzuri wa Ubongo na uti wa mgongo wa Mtoto tumboni, na hupunguza hatari ya Mtoto kuzaliwa na Matatizo ya mfumo wa fahamu, hasa katika miezi ya mwanzo ya Ujauzito.
Pia bamia huwa na Nyuzi lishe nyingi zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula na kuzuia Choo Kigumu, tatizo linalowasumbua Wajawazito wengi. Nyuzinyuzi hizi husaidia pia kudhibiti kiwango cha Sukari kwenye damu, jambo muhimu kwa afya ya mama.
Zaidi ya hayo, bamia imesheheni Vitamini na Madini kama vitamini C, vitamini A, Magnesiamu na Potasiamu, vinavyoimarisha kinga ya mwili na kusaidia afya ya Mama kwa ujumla.
Usitumie Mate kama kilainishi wakati wa Tendo la Ndoa kwasababu yana kauka haraka na huleta michubuko inayoongeza maumivu zaidi wakati wa tendo na hatari ya Magonjwa ya Zinaa
Hivyo mate hayana sifa za kilainishi sahihi, dawa ni kumundaa vyema mwenza wako ili apate mabadiliko yanayoweza kuzalisha ute ukeni mwake na sio kutumia njia za mkato.
Dkt. Baiya Kissiwa
Bingwa wa Magonjwa ya Uzazi na Kina Mama
VIDEO: Kalamu Media
Chupi za Pamba ni chaguo sahihi kwa wanawake kwa sababu zinasaidia kulinda afya ya sehemu za siri. Pamba ni kitambaa cha asili kinachopitisha hewa vizuri, hivyo hupunguza Joto na Unyevunyevu unaoweza kusababisha Maambukizi ya Fangasi na Bakteria, hali inayoweza kuleta Muwasho, harufu mbaya au Maambukizi ya mara kwa mara.
Chupi hizi hunyonya Jasho vizuri bila kuisumbua ngozi hivyo hupunguza hatari ya kupata Michubuko, Vipele au Muwasho.
Zinafaa kwa matumizi ya kila siku na kwa vipindi maalum kama Hedhi, Ujauzito au baada ya kujifungua. Zinasaidia kuweka usafi wa sehemu za siri kwa kuruhusu hewa kupita na kusaidia ngozi ibaki kavu.
Baadhi ya Mambo hatarishi yanayoongeza nafasi ya kuugua Ugonjwa wa Figo ni Uvutaji wa Sigara, Unywaji wa Pombe kupitiliza, Uzito Mkubwa, Matumizi Makubwa ya Chumvi na Sukari.
Ni muhimu kuepuka tabia hizi ili kulinda Figo zako.
Dkt.Garvin Kweka
Daktari Bingwa Bobezi wa Magonjwa ya Figo
Video: Muhimbili TV