Nyama ya sungura ni chakula bora kwa afya kwani ina protini nyingi, mafuta kidogo na kalori chache. Hii husaidia kupunguza uzito, kujenga misuli na kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa haina cholesterol nyingi na ni rahisi kumengโenywa. #StaySafe
Kiafya unatakiwa kubadilisha filter ya kuchuja maji kwenye friji kila baada ya miezi sita ili kupata maji salama, vipi wewe unabadilisha kila baada ya muda gani?. #StaySafe
Unajiuliza typhoid umeitoa wapi wakati matango na baadhi ya matunda yanayo liwa na maganda unayaosha kwa maji ya bomba. Mianya ya magonjwa ni mingi sana kikubwa ni kuangalia namna ya kuepuka tu ๐ .#StaySafe
Unapiga mswaki kwa maji ya bomba lakini unakunywa maji ya kuchemshwa๐โโ๏ธ . Unataka kuniambia hayo maji ya bomba unayopigia mswaki huwa huyamezi?๐๐. Usishangae ukipata typhoid mianya ni mingi.
Tafiti mbalimbali za kiafya zinaonyesha kufanya massage mara kwa mara huondoa huzuni,stress na msongo wa mawazo. Pia hufanya mtu kuwa na furaha kwa kuchochea uzalishwaji wa hormone aina ya Endorphins ndani ya mwili. โ๏ธ #StaySafe
Huwezi kutaja asali bila kuwasifia nyuki kwa kazi nzuri wanazofanya. Je, wajua asali hutumika kutibu vidonda? Tena vidonda vilivyo chimbika? Asali ina vitu vingi sana ambavyo vina faida kwenye kada ya Afya . Heri ya siku ya Nyuki Duniani. #StaySafe
Dada unampango wa kubeba UJAUZITO? Epuka msongo wa mawazo (stress), Afya ya akili ina mchango mkubwa sana katika uwezo wa kushika mimba. Pumzika, fanya mazoezi mepesi, na pata usingizi wa kutosha.โ๏ธ #StaySafe
Kama unajiandaa kubeba ujauzito; Epuka matumizi ya pombe, sigara, na madawa ya kulevya, hii husaidia huongeza nafasi ya kupata ujauzito salama na kuzuia madhara kwa mtoto anayetarajiwa. #StaySafe