Ninawapongeza na kuwatakia kheri wanawake wote katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Siku hii inatupa fursa ya kipekee ya kutambua, kujivunia na kusherehekea mafanikio tuliyopata, hasa katika elimu, afya, uchumi na uongozi.
Siku hii inatukumbusha pia wajibu wetu wa msingi kwa waasisi wetu na kwa vizazi vya sasa na vijavyo; wa kuendelea kupanga na kutekeleza mipango ya kumwezesha mwanamke, ikiwa ni sehemu muhimu ya kazi ya kukomboa familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
Nawatakia Waislamu wote kheri na mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tusujudu kwa shukrani mbele za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutujalia neema adhimu ya kuufikia tena mwezi huu katika imani. Tunapotekeleza nguzo hii muhimu, tumwombe atujalie kudumu katika ibada na upendo kwake na jamii na akaipokee funga yetu. Katika kufunga na kusujudu mbele zake sote tuendelee kuiombea nchi yetu amani, umoja, mshikamano na ustawi kwa wote.
Ramadan Mubarak!
Tafakari
Qur'ani Tukufu Sura Al-Baqara 183
“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.”
"Tuko katika hatua za mwisho za kukamilisha Reli ya Kisasa (SGR) na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ambalo linatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2026. Kukamilika kwa Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere na kuanza kufanya kazi kwa FGL si mafanikio ya kihandisi pekee, bali ni injini za uchumi wetu" Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Leo Rais Samia Suluhu Hassan katoa moja ya hotuba bora kabisa kuwahi kutolea na Mkuu wa Nchi kwenda kwa jumuiya ya wanadiplomasia.
1. Kaanza kwa kukiri yaliyotokea Oktoba 29 na umuhimu wa Serikali kuchukua hatua ilizochukua baada ya vurugu hizo kutokea.
2. Amekua muungwana kwa kuwashukuru kwa waliompongeza kwa ushindi na kupokea ushauri wa wale ambao hawakumpongeza.
3. Ameonyesha nia ya dhati ya Tanzania kuendelea kukua na kukomaa kidemokrasia.
4. Amezungumzia hatua zinazoendelea kuhakikisha Taifa linaponywa na vidonda vya kisiasa.
5. Ameelezea dira yake ya uchumi ambayo imewaweka vijana mstari wa mbele na kuwaomba mabalozi na nchi na taasisi zao zishirikiane na Tanzania ili kufanikisha dira yake ya maendeleo.
Leo Rais ameongea kama Rais, kama Mkuu wa Nchi, na kama Amiri Jeshi Mkuu. Hotuba ilikua na kila kitu na ilijitosheleza. Ndio maana tunaendelea kusema Mama Did It 🇹🇿🙌🏾.
Jumuiya ya Ulaya (EU) imeiondoa Tanzania kwenye orodha ya nchi zilizoainishwa kuwa katika hatari kubwa ya utakatishaji wa fedha na ufadhili wa ugaidi (AML/CFT).
Kuondolewa kwa Tanzania katika List hiyo kuna manufaa yafuatayo;
✅itapunguza vikwazo vya kikanuni katika miamala ya kifedha.
✅ Itaimarisha imani ya wawekezaji wa kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ili kuhakikisha taifa linakuwa na maendeleo endelevu, Serikali itaendea kuuheshimu na kuulinda uhuru wa Mahakama ili iweze kuwa chombo kitakacho hakikisha kunakuwepo kwa upatikanaji wa haki.
Akizungumza katika Januari 13, 2025 wakati wa akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania (TMJA) Amesema “Mahakimu mtakubalina nami kuwa hakuna taifa litakaloweza kuwa na maendeleo endelevu na ustawi wa watu wake bila usimamizi mzuri wa haki, uwepo wa Mahakama Huru yenye uwezo na uadilifu ni nguzo muhimu ya Utawala bora na ni msingi wa upatikanaji wa haki.”
Serikali itaendelea kuulinda na kuuheshimu uhuru huu wa Mahakama ila nitoe rai kwenu, Mheshimiwa Jaji Mkuu na waheshimiwa Majaji na Waheshimiwa Mahakimu kuwa uhuru huu hauna budi kwenda sambamba na uwajibikaji, uadilifu, Nidhamu, utii wa Sheria na uzalendo kwa taifa lenu lazima hayo yaendane na Uhuru wa Mahakama.”
#MillardAyoUPDATES
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, ameahidi kwenda kumlilia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili atoe Tsh. bilioni 1 au bilioni 2 ambazo zitatumika kuwakopesha Vijana waliojiajiri kwenye Online TV ili waweze kuboresha kazi zao ikiwemo kuwa na vifaa vya kisasa.
Makonda amesema hayo leo January 13,2026 Jijini Dodoma wakati akiongea na Watumishi wa Wizara ya Habari kwenye halfa fupi ya kukabidhiwa ofisi na Waziri Palamagamba Kabudi iliyofanyika muda mfupi baada ya Viongozi hao kuapishwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makonda amesema “Vijana wengi wa Taifa hili wamejiajiri kwenye habari hasa Online TV, nitaenda kumlilia Dkt. Samia atupatie fedha bilioni 1 hadi bilioni 2 tuwakopeshe Vijana wawe na vifaa vyao wenyewe ili usirekodi kwa kisimu, urekodi kwa camera ya maana una kompyuta yako ili utengeneze content ambayo Dunia itaona na kuiona Tanzania katika uzuri wake”
#MillardAyoUPDATES
Hotuba yangu kwa Taifa tunapomaliza mwaka 2025 na kukaribisha mwaka 2026.
Ninawatakia nyote kheri ya Mwaka Mpya 2026. Mwenyezi Mungu atujalie ukawe mwaka wa baraka na mafanikio zaidi kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mungu ibariki Tanzania.
#HABARI Jeshi la Polisi Tanzania limetoa shukrani kwa wananchi wote nchini kwa ushirikiano waliouonyesha katika kulinda na kudumisha amani kipindi chote cha Sikukuu ya Krismasi, iliyoadhimishwa 25 Desemba 2025.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Dodoma DCP David Misime, amesema hatua hiyo imewezesha sherehe za mwaka huu kufanyika kwa utulivu na bila changamoto za kiusalama.
Amesema hali ya usalama imeendelea kuwa shwari katika maeneo yote ya nchi, huku wananchi wakiendelea kusherehekea sikukuu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi bila wasiwasi wala hofu.
" Jeshi la Polisi limeeleza kuwa ushirikiano baina ya wananchi na vyombo vya ulinzi umekuwa nguzo muhimu katika kufanikisha dhamira ya kulinda amani na kutengeneza mazingira mazuri ya kusherehekea, "amesema
Akitoa wito kwa umma, Msemaji wa Jeshi hilo amewataka Watanzania kuendelea kuilinda amani kama msingi wa maendeleo ya taifa.
“Tunaendelea kuwasihi wananchi kudumisha amani kwani ndiyo inatupa fursa ya kusherehekea bila hofu tukiwa na marafiki na jamaa,” amesema.
Ameongeza kuwa bila amani hakuna shughuli za kijamii na kiuchumi zinazoendelea kwa ufanisi.
Kupitia taarifa hiyo amebainisha kuwa shughuli za kiuchumi, ikiwemo biashara, usafirishaji, huduma za kijamii na kazi za utumishi wa umma zinaendelea kama kawaida bila wasiwasi wowote.
Aidha Jeshi hilo linasisitiza wananchi kuendelea ushirikiano na utulivu huku likiahidi kuendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yo te na , kuhakikisha kila raia anabaki salama wakati wote.
Pia limewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa mapema pale wanapotilia shaka viashiria vya uvunjifu wa amani, ili kuchukua hatua za haraka na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza. #EastAfricaTV
Dkt. Samia Suluhu Hassan , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anawatakia Watanzania wote Heri ya Sikukuu ya Krismasi.
Tusherehekee sikukuu hii kwa amani, upendo na utulivu, tukidumisha mshikamano wa kitaifa.
Tumejifunza
Tunajenga Mustakabali Mpya Wa Matumaini
Tunaendelea Mbele Kwa Umoja
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Gutteres amesema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa kwa Afrika na duniani kama nchi yenye amani na mshikamano wa kijamii.
Amesema hayo leo baada ya kupokea ujumbe maalum kutoka Tanzania, ambapo ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa (UN) ungependa kuona Tanzania ikiendelea kuwa na mfano kwa nyingine.
🚨 Ibrahima Konaté: “Personally I do not think Mo Salah played his last game for Liverpool. You saw how much he loves this club”.
“He is a player that everyone loves, the coach loves, he loves the coach, everyone loves each other at this club”.
TANZANIA NI MFANO WA AMANI NA MSHIKAMANO DUNIANI- GUTERRES
Ujumbe wa Mheshimiwa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 14 Desemba 2025, wakati akipokea Ujumbe Maalum kutoka Tanzania.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mheshimiwa Antonio Guterres, amesema kuwa “Tanzania imekuwa ni rejea muhimu ya amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote,” wakati akipokea Ujumbe Maalum kutoka Tanzania.
Ameeleza kuwa taswira ya Tanzania kama kielelezo cha amani ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, lakini taifa liliweza kuvuka mtihani huo kwa mafanikio, ikiwa ni mara ya kwanza kukabiliwa na changamoto hiyo.
“Umoja wa Mataifa ungependa kuona Tanzania inaendelea kubaki katika umoja wake na kuwa mfano bora kwa mataifa mengine,” alisema Katibu Mkuu Guterres alipokuwa akipokea Ujumbe Maalum uliobeba salamu na ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Kombo, pamoja na ujumbe wake.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa yenye maana, jumuishi na shirikishi ili kushughulikia chanzo cha matukio ya vurugu yaliyotokea tarehe 29 Oktoba, pamoja na kutafuta njia za kudumu za kuyazuia yasijirudie tena.
Aidha, aliahidi msaada kamili wa Umoja wa Mataifa wakati wote na hata baada ya Tume ya Uchunguzi iliyoanzishwa nchini Tanzania kukamilisha majukumu yake.
Amani ni tunu tuilinde. Machafuko hayajawai kuwa na jawabu za changamoto za Taifa lolote ulimwenguni. Na mataifa yalioingia kwenye machafuko kwanjia ya kudai haki swali la kujiuliza izo haki wamezipata?
Je maisha yao kabla na baada ya vurugu yapoje? Na nini wanakitamani kwa sasa?
Alikiba anasema kila Mtanzania ana Haki ya Kuchagua Chama Chochote na yeye kama Mtanzania Chama chake ni CCM. Kama ambavyo pia mashabiki wana vyama vyao vya siasa hata yeye Msanii ana Chama chake!!
DODOMA; RAIS Samia Suluhu Hassan, amemteua Plasdus Mbossa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, imesema: “Plasdus Mkeli Mbossa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)”.