Dabi ya Kariakoo imetamatika katika dimba la Uhuru, Jijini Dar es salaam, huku Mnyama, Simba SC, akiibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC.
Mabao ya Simba yamefungwa na Neo Maema pamoja na Elie Mpanzu katika kipindi cha pili, huku bao pekee la Yanga likifungwa na Peter Shalulile katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2026/2027.
#MillardAyoUPDATES
VIDEO:
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Manyema na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa BAKWATA Taifa, Sheikh Hamid Masoud Jongo, ametoa onyo kali kwa Waislamu nchini dhidi ya kushiriki au kushawishiwa kushiriki maandamano na ghasia, akisema kuna njama mpya ya kuingiza vijana Waislamu ili wapoteze maisha kama sehemu ya mpango wa kuvuruga amani ya nchi.
Akizungumza katika Hotuba ya Ijumaa, Sheikh Jongo amesema kuna watu ambao hawataki nchi iwe tulivu, na bado wanafanya mipango ya kuvuruga utulivu na sasa wanatafuta visingizio vya kuibua maafa mapya.
Adai kuwa kuwa ghasia zilizotokea siku ya uchaguzi zilifanywa na vijana walioshawishiwa, na tayari zimeleta hasara kubwa kwa taifa, ikiwemo watu kupoteza maisha, wengine kuumia na mali nyingi kuharibiwa hususan vituo vya mafuta na miundombinu ya mabasi ya mwendokasi.
Sheikh Jongo amesema kutii mamlaka ni wajibu wa Kiislamu, hata pale panapowaletea maumivu akisisitiza pia wajibu wa kufuata maagizo ya vyombo vya usalama, akitolea mfano agizo la kutotembea usiku.