Watu ndani ya CCM wamevurugwa. Sasa ndo naamini upinzani halisi utatoka ndani ya CCM yenyewe. Nadhani kuna jambo lina fichwa fichwa hivi kwa sababu ukimsikiliza Polepole na Gwajiboy wote wanasema nitakapo amua kusema mazito nchi chama na Nchi vitalipukaaaaa
VIDEO:
"Injinia Hersi Said ametuthibitishia kwamba ni mfanyakazi wa GSM na wakati huohuo ni Rais wa klabu ya Yanga... a conflict of interest (Mgongano wa kimaslahi). Inapotokea kwamba wewe ni kiongozi wa klabu, halafu wewe pia ni sehemu ya watumishi wa kampuni inayodhamini hiyo klabu . Inapotokea conflict of interest anasimama upande gani? Hili ni tatizo la kwanza ambalo Yanga wenyewe wanatakiwa walione", - Golugwa.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara Amani Golugwa akizungumza na Jambo TV siku ya Ijumaa juu ya mchango unaodaiwa kutolewa na klabu ya soka ya Yanga kwenda kwa CCM.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina, amesema moja ya mambo yaliyomshangaza ni pale aliposemwa mbele ya wananchi kisa kusimama na kutetea kero zao ikiwemo Bei ya zao la pamba na miundombinu ya Barabara.
Ameyasema hayo leo wakati akiongea na wananchi wa Mwandoya, Jimbo la Kisesa Mkoani Simiyu baada ya kupokelewa na kuomba udhamini.
"Kiongozi badala ya kutusikiliza wawakilishi wa wananchi unaanza kutudhihaki, halafu unataka tuseme hatukudai, tumeondolewa bungeni kwa sababu ya kusimamia maslahi yenu na wameona wachague watu wao wa Ndiyo mzee, atakachoambiwa yeye sawa tu" amesema Mpina
Kaimu Katibu Mkuu, Mh. John Mnyika. Akitoa salamu za rambi rambi, alipoungana na ndugu, jamaa na wanachadema wengine katila msiba wa Marehemu MC Mwingira leo Songea.
Apumzike kwa Amani Kamanda Mwingira.🙏🏽🙏🏽
TANZIA
Kwa huzuni na masikitiko makubwa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatangaza kifo cha George Mwingira, maarufu kama MC Mwingira, msanii mkubwa na shupavu wa chama, aliyefariki dunia katika ajali ya basi la SAMA Luxury lililokuwa likisafiri kutoka Songea kuelekea Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Jumanne, Agosti 12, 2025.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Iyovi, mkoani Morogoro.
MC Mwingira alitumia kipaji chake cha muziki na uandishi wa nyimbo kuhamasisha mapambano ya kudai haki na demokrasia. Alijulikana sana kwa wimbo maarufu “Tundu Lissu Wakimbize Mchaka Mchaka”, uliotumika kama wimbo rasmi wa CHADEMA katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Wimbo wake wa mwisho kuutunga na kusambaza ndani ya chama ulikuwa “No Reforms, No Election”, uliobeba ujumbe wa kudai mabadiliko ya kidemokrasia.
Kwa sasa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Misheni Mikumi, mkoani Morogoro.
Ratiba kamili ya mazishi itatangazwa mara baada ya mashauriano na familia.
Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wasanii wenzake, pamoja na wanachama wote wa CHADEMA kwa msiba huu mzito.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.
Mhe @AdvMahinyila , Mwenyekiti Baraza la Vijana Chadema(Bavicha) Taifa akizungumza na vijana nchi nzima jama siku ya vijana dunia kupitia zoom meeting(mtandao) ya kuzuiliwa kwa Bavicha kukusanyika kwa pamoja.