Leo nilipata fursa ya kutembelea Hospitali ya Queens iliyopo kusini mwa London kwa madhumuni ya kuonana na Timu ya Madaktari Bingwa na Wauguzi wanaotarajiwa kwenda Tanzania kwenye ziara ya kikazi. Hospitali hiyo ni sehemu ya Barking, Havering and Redbridge University Hospitals NHS Trust (BHRUT). Katika ziara hiyo wataalam hao wataendesha mafunzo katika Taasisi ya @TaasisiyaMifupa ya Muhimbili jijini Dar es salaam pamoja na Hospitali ya Mnazi Mmoja- Zanzibar.
Ziara hiyo ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na Mwanadiaspora Prof @GideonMlawa ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu katika Hospitali ya Queens ya London. Kwa muda mrefu Prof Mlawa kwa kushirikiana na wenzake katika Jumuiya ya TUHEDA wamekuwa wakiratibu ziara za aina hiyo pamoja na kupeleka misaada ya vitabu kwa vyuo vikuu vya tiba nchini Tanzania na vifaa tiba katika hospitali mbalimbali nchini.
Wanadiaspora wanafanya mambo mengi yenye manufaa kwa nchi yetu- wajibu wetu kama Ubalozi ni kuwatambua; kuwatia moyo na kuwaunga mkono katika shughuli wanazofanya zenye manufaa kwa nchi yetu.
Ninampongeza mwanadiaspora Hamida Mbaga kwa kutangaza bidhaa mbalimbali za utamaduni kutoka Tanzania katika soko la Uingereza. Kazi hii aliyoifanya kwa miaka mingi imemjengea sifa ya kuwa miongoni mwa waafrika wanaotumainiwa yanapofanyika maonesho ya bidhaa za Afrika nchini Uingereza. Ubalozi utashirikiana naye pamoja na wanadiaspora wengine kuonesha kazi za sanaa za Tanzania wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afrika yatakayofanyika Mwezi Mei mwaka huu https://t.co/8RSeQjvs1Q