Mbwa akikaribia kufa hupoteza uwezo wa kunusa. Inawezekanaje taasisi yenye miaka zaidi ya 30 inaendeshwa na wanaharakati waliolowea ughaibuni ambao hawana weledi, maono, ujuzi wala uhalali?!!!
Nilisema na leo narudia tena. Ikiwa CHADEMA haitatoka hadharani na kukataa kuendeshwa kwa rimoti na wanaharakati uchwara, utakuwa ndio mwisho wake. Kansa iliyoanza itawamaliza. Lazima wakate kidole. Chama ni taasisi, Chama ni vikao, Chama ni utaratibu.
Kwa maoni yangu, CHADEMA iko katika hali ya “Chama kuwekwa mateka” yaani “party capture”. Watu ambao sio vikao, si viongozi, hawatajwi popote na Katiba yao, wameteka, wanaendesha, kutoa maamuzi & muelekeo wa Chama wakijiita wanaharakati. ANOMIE! Timed bomb!
Kufanya ukatili kwa binadamu kwasababu ya mali au mapenzi ni woga wa maisha. Nyumba zinajengwa, pesa zinatafutwa na wachumba wamejaa tele. Kuanza upya si udhaifu. Wazee wetu hawakuogopa kujipanga upya. Jamii lazima tutafakari kuhusu malezi & afya ya akili.
Nimemtembelea na kutoa pole kwa Rais mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dr. Aman Abeid Karume pamoja na Balozi Ali akarume kufuatia msiba wa Mama yao mpendwa, hayati Bibi Fatma Karume. Mwenyeezi Mungu awajaalie subira na uvumilivu.
Nimeshiriki maziko ya marhum Mama Fatma Karume Mazizini Unguja. Mwenyeezi Mungu amjaalie maghfira na rehma. Poleni sana familia. Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raajiuun.
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama yetu, Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kilichotokeo leo tarehe 21 Septemba, 2026.
Kifo chake ni pengo kwa familia na Taifa kwa ujumla, kwani alikuwa sehemu muhimu ya historia adhimu ya Zanzibar kuanzia wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mapinduzi Matufuku ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daima tutaendelea kukumbuka, kuenzi na kuheshimu mchango wake katika kuhifadhi kumbukumbu na urithi wetu, pamoja na kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Taifa letu.
Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, familia ya Hayati Sheikh Karume, ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote. Ninawaombea Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
Huyu katumwa apeleke rambirambi Kizimkazi kwa Mhe. Rais yeye kakaidi ameenda kulima parachichi. Huku ni kumkosea heshima Mwenyekiti wake TL. Wanaharakati uchwara walio nje ndio wanampa kiburi. Wanamtafutia ya mboga…
Mwanzo Lissu alimuagiza Heche, “endeleeni nisiwakute nilipowaacha, tutagombana…” (waende ktk maridhiano).
Juzi ameagiza rambirambi zifikishwe kwa Mhe. Rais Kizimkazi. Ni kipi hamuelewi?!! Picha iko wazi, lakini inahitaji upeo mkubwa kuiona. Siasa ni mbinu…!
CHADEMA imekwama kwenye tope na hawana tena UWEZO na MAARIFA ya SIASA ya kujinasua. Viongozi wake wana MSONGO mkubwa. Wenye nafasi hawana PLAN na wenye IDEA wanahofu kuonekana wasaliti. Wanaharakati FEKI wameshika RIMOTI lakini hawajui kusoma wala kuandika…!
Kwa maoni yangu, CHADEMA iko katika hali ya “Chama kuwekwa mateka” yaani “party capture”. Watu ambao sio vikao, si viongozi, hawatajwi popote na Katiba yao, wameteka, wanaendesha, kutoa maamuzi & muelekeo wa Chama wakijiita wanaharakati. ANOMIE! Timed bomb!
Nimemsikia mara mbili, Tundu Lissu akimtaka Makamu wake Heche kupeleka salamu za pole kwa Mhe. Rais kufuatia msiba wa mwenza wake. Lakini ajabu, hadi sasa sijamuona Heche kufika Kizimkazi ili kupeleka ujumbe huo wa Mwenyekiti wake TL. Liko tatizo kubwa CDM!!
Ninawatakia Waislamu na Watanzania wote kheri na baraka za Sikukuu ya Maulid. Kumbukizi ya siku hii njema ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) itukumbushe kuendelea kuishi kwa upendo, huruma, uvumilivu na kuwajali wengine.
Tusherehekee kwa amani na furaha, huku tukidumisha umoja na mshikamano wetu. Mwenyezi Mungu Mtukufu aendelee kuibariki nchi yetu, kuitunza katika amani na utulivu, na kutuwezesha kuijenga kwa maendeleo na ustawi wa wote.
Mawlid Al Nabi Mubarak.
Met with HE Daniel Francisco Chapo, President of FRELIMO and President of the Republic of Mozambique. I conveyed a message of cooperation and solidarity from HE. Samia Suluhu Hassan, the Chairperson of CCM and President of the United Republic of Tanzania.