The history of the Industrial Revolution shaped global progress. In Central Asia, it involved artistic innovation. Artifacts preserve its historical impact. This era’s legacy informs our modern world. 🧳 💐
Trying to eat healthier but the office snack table is constantly tempting me. Willpower is easier at home than in environments full of free treats. 👍 🍁 🍬
Organized my entire makeup collection today, and it feels like a weight off my shoulders! Found lipsticks I forgot I owned. Time to experiment with bold fall looks! BeautyRefresh 🎊
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema licha ya Serikali kutumia zaidi ya shilingi bilioni 54 kujenga Stendi ya Magufuli, baadhi ya maeneo ya Jiji yameendelea kugeuzwa kuwa stendi zisizo rasmi za mabasi, hali inayochangia ongezeko la foleni na kuvuruga utaratibu wa usafiri.
Akitoa mfano wa eneo la Shekilango, Chalamila amesema baadhi ya mabasi yamekuwa yakipaki kwenye hifadhi za barabara na kuyageuza maeneo hayo kuwa stendi, jambo linalosababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.
Chalamila ameyasema hayo leo, Juni 29, 2026, wakati wa kikao kilichowakutanisha wadau wa sekta ya usafirishaji, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Pwani, kilicholenga kujadili mikakati ya kudhibiti na kupunguza tatizo la foleni katika Dar es salaam.
“Ukienda Ubungo kuna Stendi ya Magufuli iliyojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 54, lakini leo tumeruhusu karibu kila eneo la mkoa kuwa stendi, Watu wa Uhamiaji hawawezi kufanya kazi yao kwa ufanisi, vyombo vya dola navyo haviwezi kutekeleza majukumu yao ipasavyo na katika miji mingi iliyoendelea duniani, unaweza kupandisha abiria na kuwapeleka hadi stendi kuu, lakini huwezi kupeleka basi hadi nyumbani kwa kila abiria,”amesema Chalamila.
#MillardAyoUPDATES