Katika kuendeleza ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia kati ya Tanzania na Uturuki, nimefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoğan jijini Antalya. Mazungumzo yetu yamegusia kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Uturuki.
Tumekubaliana kuweka mazingira wezeshi ya biashara, kuondoa vikwazo vya kibiashara vilivyosalia na kupanua masoko ya bidhaa za kilimo na madini. Pia, nimewahimiza wawekezaji wa Uturuki kuwekeza nchini katika viwanda vya nguo, usindikaji wa chakula na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi, sambamba na kuhamisha teknolojia ili kuongeza uzalishaji, thamani ya bidhaa na fursa za ajira.
Aidha, tumejadili kupanua fursa za masomo na mafunzo ya amali kwa wanafunzi wa Tanzania, pamoja na kuendeleza utekelezaji wa mikataba ya ushirikiano katika uwekezaji na kodi, ikiwemo Mkataba wa Ushirikiano kati ya TIC na Ofisi ya Rais ya Uwekezaji ya Uturuki, na Mkataba wa Kuepusha Utozaji wa Kodi Mara Mbili.
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) ambapo amesema Tanzania inaelekeza nguvu katika hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinazozalisha fursa kwa vizazi vijavyo.