Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), magonjwa yasioambukizwa ikiwemo Shinikizo la juu la Damu, Kisukari, Magonjwa ya Moyo, Kiharusi, Magonjwa ya Akili, Magonjwa ya mfumo wa Hewa, Saratani nk yanaua takribani watu milioni 41 kila mwaka.
Je, wajua?
Kila siku watu takribani 1000 wanapoteza maisha yao kutokana na ugonjwa wa Pumu (Asthma). Chukua tahadhari zaidi kwa ugonjwa kwa kuepuka vichochezi ikiwemo moshi na vumbi
Chanzo:Shirika la Afya Duniani (WHO).
Leo ni siku ya kimataifa ya kusafisha mikono, tunakumbushana kuwa kuvaa glavu haiondoi kutosafisha mikono. Safisha mikono kwa maji ya kutiririkana sabuni kabla ya kufanya kitendo kinachohitaji kuvaa glavu na baada ya kuvua.
#WorldHandHygienceDay
Kwa mujibu wa utafiti wa Wizara ya afya Zanzibar na WHO, asilimia 20 ya watu wanatumia chumvi kwa wingi na asilimia 10.9 wanatumia vyakula vilivyosindikwa viwandani. Hali hii inapelekea kuongezeka kwa unene na hatari ya magonjwa yasiyoambukizwa.
Kwa mujibu wa utafiti wa Wizara ya afya Zanzibar na WHO, bado kuna changamoto ya watu kutozingatia dawa ambapo takwimu zinaonesha kuwa mtu mmoja kati ya watu watano wenye shinikizo la juu la damu ambae anatumia dawa na kati ya hao asilimia 3.2 tu ndio wameweza kuthibiti ugonjwa.