Sehemu ya hotuba yangu mapema leo Ikulu jijini Dar es Salaam nilipozindua Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika Nusu Fainali.
📍Mbinga
25.09.2024
Mapema leo wakati wa Ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. @SuluhuSamia Wilaya ya Mbinga.
Tumetoa ONYO kwa wafanyabiashara wanaoenda kununua mahindi vijijini kwa wakulima kutokiuka bei elekezi ya kununua vijiji ambayo inatakiwa isiwe chini ya 500 hadi 600 kwa kilo.
Kama Serikali tumeahidi Kuanzia mwaka kesho 2025 maeneo yote yenye vituo vya kununua mahindi yatakua na mashine za kisasa za kusafishia mahindi.
Aidha nimeweza pia kuongelea Kahawa inayozalishwa Mbinga na kumfahamisha Mheshimiwa Rais pamoja na wananchi kuhusu mfumo mpya wa mnada wa TMX utakaowafaidisha wakulima na kuwaokoa na mfumo kandamizi wa makangomba. Tumepiga pia marufuku vyama vya msingi kushikilia fedha za wakulima, na vyama vya ushirika kwenda kukopa kwa jina la wakulima ili hali hizi fedha hazifiki kwa wakulima.
#Agenda1030
Tanzania wholeheartedly endorses Dr. Faustine Ndugulile
Vote for Dr. Faustine Ndugulile
@DocFaustine
for WHO AFRO Director!
His experience and commitment to health matters make him the right choice for Africa’s Future.
#Ndugulile4WHOAFRO
Ujenzi wa Kampasi ya Babati ya Chuo cha Uhasibu Arusha, naupongeza Uongozi wa Chuo kwa ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa mradi huu kwa utaratibu wa force account.
Nimeweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Tawi la Babati mkoani Manyara. Naupongeza sana uongozi wa Chuo kwa kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma ya elimu karibu na Jamii.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), ameungana na abiria wengine kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kuonja ladha ya usafiri huo ambao Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa mradi huo wa kimkakati unakamilika na kuchangia kuchochea biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu. Aliyekaa karibu naye ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Mhandisi Ismail Hassan Rumatila,
📍 Mtanana, Dodoma.
Mapema jana 20.08.2024 kwenye Kituo cha Umahiri cha Uhifadhi wa Nafaka wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo hicho, ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isidory Mpango.
Tarehe 19.08.2024 nilipata nafasi ya kumpokea Makamu wa Rais Dr. @dr_mpango ambaye aliweka jiwe la msingi la Kiwanda cha Kusindika Zabibu katika Wilaya ya Chamwino. Kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika tani 7-8 za zabibu kwa siku.
Kiwanda hiki ni matokeo ya juhudi zetu za pamoja na kinatarajia kupunguza utegemezi wetu wa mchuzi wa zabibu kutoka nje, ambao unagharimu takriban Shilingi Bilioni 19.5 kila mwaka.
Nawahimiza wakulima wa Dodoma na Chamwino kuongeza uzalishaji wao ili kunufaika kikamilifu na kiwanda hiki.
Kama Waziri wa Kilimo, ninawahamasisha wananchi kuongeza uzalishaji wa zabibu na mazao mengine ya kimkakati, hasa kwa kuzingatia hali nzuri ya kilimo ya Dodoma. Serikali imejipanga kuhakikisha masoko ya uhakika kwa zao la zabibu, ikichochewa na ongezeko la mahitaji ya mvinyo.
Yesterday I had the honor of welcoming and hosting the Vice President of Tanzania, Hon. Dr. @dr_mpango who laid the foundation stone for a new Grape Processing Factory in Chamwino District, with a capacity to process 7-8 tons of grapes daily. This factory is a testament to our collective efforts and aims to reduce our reliance on imported grape juice, which costs us approximately TZS 19.5 billion annually.
As the Minister of Agriculture, I encourage our citizens to increase grape production and other strategic crops, especially given Dodoma’s favorable agricultural conditions. The government is committed to ensuring stable markets for grapes, driven by the rising demand for wine.
I urge farmers in Dodoma and Chamwino to increase their production to fully benefit from this facility.
#Agenda1030
Machache yaliyojiri kwenye Ziara za Mheshimiwa Rais Dkt @SuluhuSamia mikoa ya Rukwa, Katavi, Songwe, Kigoma, Morogoro.
Tunatambua kazi ni kubwa kuleta mapinduzi na maendeleo tunayo yahitaji kubadilisha sekta ya Kilimo Tanzania na kama anavyosema Mhe. Rais Dkt.@SuluhuSamia Kazi ndio kwanza imeanza.
Tumedhamiria na tutatekeleza kufikia #Agenda1030
Yesterday 16.08.2024, I had the pleasure to meet and hold discussions with the Minister of Agriculture from Malawi, Hon. Sam Dalitso Kawale.
Our discussions focused on various aspects of adding value to agricultural production, particularly in crops such as maize, tobacco, and tea. Hon. Kawale is in the country on a visit to the ITRACOM factory, which produces FOMI fertilizer, to explore how it can help improve productivity for farmers in Malawi.
During our discussions, I mentioned that the Ministry will send a team of experts to Malawi to learn about tobacco and peanut production, where in Malawi, peanuts are grown as a second crop in the same season after the tobacco harvest. This technique will help increase productivity for our farmers so that they do not rely on a single crop throughout the entire farming season.
We also discussed how to enhance research and development in both countries, particularly in maize, tobacco, and tea crops, to advance the agricultural sector and produce better seeds.
Siku ya Jana 16.08.2024 nimekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo kutoka Malawi, Mhe. Sam Dalitso Kawale jijini Dodoma.
Mazungumzo yetu yalijikita katika nyanja mbalimbali za kuongeza thamani ya uzalishaji kwenye Sekta ya Kilimo, hususan katika mazao ya mahindi, tumbaku, pamoja na chai. Mhe. Kawale yupo nchini kwa ziara ya kutembelea kiwanda cha ITRACOM ambacho kinazalisha mbolea aina ya FOMI, ili iweze kusaidia kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima nchini Malawi.
Majadiliano pia yalitizama namna wanaweza kununua mbolea ndani ya Tanzania inayozalishwa na kiwanda chetu cha Intracom.
Katika mazungumzo yetu, nilgusa namna Wizara imejipanga kutuma timu ya wataalamu nchini Malawi ili kujifunza namna ya kuzalisha tumbaku na zao la karanga, ambapo kule Malawi, karanga hupandwa kama zao la pili baada ya uvunaji wa tumbaku katika msimu mmoja. Mbinu hii itaongeza tija kwa wakulima wetu ili wasitegemee zao moja katika msimu mzima wa kilimo.
Pia, tumedhamiria kujifunza na kuendeleza masuala ya utafiti katika nchi zote mbili, hususan katika mazao ya mahindi, tumbaku, pamoja na chai ili kuendeleza sekta ya kilimo na kuzalisha mbegu bora.
#Agenda1030
Salaam Ndugu Zangu
Namshukuru Mungu kwa baraka za afya na nguvu ya kuendelea kulitumikia Taifa.
Jana tarehe 10.08.2024 tulipata nafasi na heshima ya Mheshimiwa Rais Dkt. @SuluhuSamia kushiriki kikao na Maafisa Kilimo 850 Ikulu Chamwino, Dodoma.
Maafisa Kilimo hao ni pamoja na Maafisa Ugani ambao ni kundi maalum lililopewa kipaumbele ili tuweze kufikia #Agenda1030 ya kuongeza uzalishaji na kilimo chenye tija ifikapo mwaka 2030
Tumeendelea kuimarisha huduma za ugani kwa kuwekeza kwenye
-ununuzi wa pikipiki 6,439 za maafisa ugani sawa na asilimia 95.76
-Sare 6,456 za maafisa ugani sawa na asilimia 96
-Vishkwambi 4,446 sawa na asilimia 66
-Magari 25 kwa ajili ya maafisa Ugani
-Ujenzi nyumba 50 za maafisa ugani umeanza
-Vipima udongo 143
Niwashukuru Maafisi Kilimo na Wadau wote walioweza kujumuika na sisi, na kama Mhe Rais @SuluhuSamia alivyotuelekeza Kazi ndio IMEANZA.
Tusimuangushe, mmewezeshwa sasa nendeni mkatekeleze.
Kwa pamoja tunaweza.
#KilimoNiBiashara
Katika Kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya Nane Nane ambapo pamoja na mambo mengine nimeweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Maabara Kuu ya Kilimo Dodoma, ya kisasa na ya mfano kwa Bara la Afrika.
Kilimo, mifugo na uvuvi ni sekta ambazo zimeajiri asilimia kubwa ya wananchi wetu, na ustawi wa nchi yetu unazitegemea kwa kiasi kikubwa. Umuhimu wa sekta hizi ndio msingi wa uamuzi wa kuziongezea ukubwa wa bajeti kwa zaidi ya mara 4 katika kipindi cha miaka mitatu.
Hatua hizi zimeanza kuleta matokeo makubwa ambayo sote tunayashuhudia ikiwemo kuongezeka kwa uzalishaji, huduma za maafisa ugani, idadi ya wananchi wanaojiajiri kupitia sekta hizi hasa vijana na wanawake, kuongezeka kwa usindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kuongezeka kwa mitaji, masoko, pamoja na ujenzi wa bandari za uvuvi.
Nimeendelea pia kusisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi bora wanaopenda maendeleo ya wananchi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa badala ya viongozi wanaojali maslahi yao binafsi. Utekelezaji wa mipango yote tunayojiwekea unategemea umadhubuti wa viongozi tunaowachagua kuanzia ngazi ya Serikali ya Mtaa.
Tuendelee Kuchapa Kazi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Yusuf Mwenda, Katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es salaam, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi hiyo muhimu huku jambo kubwa likiwa ni kuweka mikakati ya kutekeleza maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuboresha ukusanyaji kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Salaam Ndugu Zangu,
Kwanza nitangulize shukran kwa Mwenyezi Mungu wa Rehema kwa kutuwezesha na kutufanikishia shughuli yetu ya Kilele cha Maonesho ya Nane Nane jana 08.08.2024 Nzuguni, Dodoma.
Shukrani zangu za dhati pia zinaenda kwa mgeni wetu rasmi, Mhe. Rais Dkt. @SuluhuSamia kwa kuwa nasi kwenye maadhimisho haya, lakini pia kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa ushirikiano tunaouhitaji kuleta maendeleo na mapinduzi kwenye setka ya Kilimo na Mifugo na Uvuvi nchini.
Shukrani zangu zingine ziwaendee Wizara za Kilimo NA Mifugo na Uvuvi, pamoja na Taasisi zake na wabia wake. Hakika maonesho ya mwaka huu yamekua ya kipekee, na nafarijika kuona ijayo itakua BORA zaidi na Nane Nane Dodoma patakua pamebadilika sana.
Shukrani zangu zingine ziwaendee wadau wa sekta binafsi na wadau wa maendeleo. Tunashukuru sana kwa ushirikiano katika kufanikisha shughuli hii.
Yote pia yasingewezekana bila wadhamini wetu wakuu GSM na Azania Bank. Shukrani za dhati ziwafikie.
Mwisho ni Viongozi na Wakurugenzi, Wafanyakazi na Watumishi wa Taasisi mbali mbali za Serikali walioweza kuungana na sisi.
Kwa pamoja tuendelee kutekeleza #Agenda1030