Hakuna wa kuja kutuokoa! Tujiandae kabisa kisaikolojia! Lissu hatupambanii bali anatuonyesha njia
Sisi ndo tunatakiwa kumpambania na kujipambania
Waovu hawaendi kumwachia labda akubali masharti yao
Tundu Lissu is human - he needs our support! Nobody is coming to save us!
#FreeTunduLissu
Wauaji walimualika Benny Hinn aje Tanzania kwa mwaliko wao, Lengo kuhadaa Wakristo na watu wa kanisa
Kabla hajaja akampigia simu Apostle Mwingira maana ni marafiki, Aakasema mimi siwezi kutumika kusafisha damu za watu.
Kama unakuja uje kivyako, ila mimi siwezi kuja kukupokea!
See the focus?
Hakuna kitu kinaweza kumtoa kwenye focus Tundu Lissu! Na sisi tuwe na hii laser sharp focus tuache kuwa emotional kila wakati!
Msianze kuniambia eti moyo sijui roho imeniuma! Tumeumizwa mara ngapi? Hakuna shortcut! LAZIMA kupambana bila kuchoka na hawana busara wala utu! Wako tayari kutuua na kututeka wote!
Machawa wa Abdul na wa Mwamba wamefurahi jana kuwa Lissu aliambiwa ana kesi ya kujibu ila hawajui kuwa hapo kulikuwa na dirisha ndogo iliyobaki ya kimama kuchomoka - sasa amefungua kila avenue!
Mengine siweki wazi maana mi naona hii chess game na Lissu anachofanya ila wapumbavu wanachekelea tu maana ni mazuzu 🙄 complete idiots!
Sisi tuendelee kujipanga kuweka shinikizo muda umekaribia 🔥💪🏽
Tuanze mazoezi mapema tukomboe nchi
#TutaelewanaTu
#FreeTunduLissuNow
#SamiaMustGo
Haya tunaambiwa na mdau kuna simu inasubiriwa saa 7 usiku wa manane tujue maamuzi!
Ila hawa ma fomfoo feliaz wanachosha! Nchi inaendeshwa kiwaki ila sisi tunasema #FreeTunduLissu
Hatupoi!
SC Tundu AM Lissu (Since 1968)
Mahambe Primary School.
Ilboru Secondary School.
Galanos High School.
University of Dar Es Salaam (LLB).
University of Warwick (LLM).
Formerly: MP, TSL President.
Currently: CHADEMA party Leader & TZ President in waiting!
Afisa Mahusiano ya Umma, Propaganda na Upotoshaji katika Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali akitoa ufafanuzi wa tuhuma zinazoikabili Serikali yake tukufu kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye yupo ‘bizee’ katika mambo ya festivo.
DAVID DJUMBE- 'NILIBAKI NA MAUMIVU YA PINGU MPAKA ASUBUHI, MAANAKE HAZIKUWA PINGU ZA POLISI WA KAWAIDA, BALI NI ZA WALINDA USALAMA'
Tazama LIVE: https://t.co/3PzpYGRApi
Bunge lenye vyama vingi vilivyo huru huongeza ufanisi katika kuisimamia Serikali Kuu, kutathmini bajeti, na kuhakikisha kodi za wananchi zinasimamiwa kwa uwazi. #KatibaMpya
VIDEO:
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, leo Jumapili Agosti 09, 2026, amepinga kauli ya serikali kuwa imeshafikia makubaliano na vyama vyote vya siasa isipokuwa kimoja.
Mpina amerejea kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa tarehe 30 Julai 2026, alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu, ambapo alidai kuwa vyama vyote viko vizuri isipokuwa chama kimoja ambacho kimeelezwa na wadau siasa kuwa CHADEMA.
Mpina amebainisha kuwa msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu maridhiano bado upo vile vile kama ulivyotangazwa kwenye matamko ya kamati kuu ya chama hicho. Mpina amesema kuwa hakuna maridhiano yoyote yanayoweza kufanyika bila kuzingatia misingi mitatu mikuu: Ukweli, Haki, na Uwajibikaji kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Amesema kuwa CHADEMA pia ilishatoa taarifa tarehe 3 Agosti 2026 kuwa haijawahi kukutana kwa siri na CCM au serikali kwa mazungumzo yoyote.
“Sasa haya maneno ambayo anayazungumza mtawala kwamba ameshaelewana na vyama vya siasa isipokuwa chama kimoja ina maana gani? Ina maana gani?” amehoji Mpina.
Katibu wa Idara ya Fedha na Uchumi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Jamal K. Ali, amemuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa masuala ya fedha ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo kisheria, na kutoa taarifa kwa Watanzania kuhusu matokeo ya ukaguzi huo Kwani Chadema inakusanya Fedha Kwa Watanzania na Kisha Viongozi kutumia Kwa maslahi Binafsi.
"Kwa Sasa wanachadema Pamoja na Viongozi wenzake HECHE Hawana Imani naye tena Kutokana na ubadhulifu Anaendelea kuufanya ndani ya CHADEMA" Amesema Jamal.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma, Ndugu Jamal ametoa madai kuhusu usimamizi wa fedha ndani ya CHADEMA, akieleza kuwa kuna maswali yanayohitaji ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha za chama hicho.
Aidha, amezungumzia umuhimu wa vyama vya siasa kuwa na mikakati ya kuongeza mapato na kusimamia rasilimali zao kwa ufanisi.