Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizungumza na baadhi ya wananchi aliowakuta ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Meru wakati wa ziara ya kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero za ardhi katika mkoa wa Arusha.
#kaziiendelee
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza zoezi la kutambua vipande 17,000 vya ardhi katika kata sita zenye mitaa 32 katika halmashauri ya jiji la Mbeya na kuwapatia wamiliki wake Leseni za Makazi.
Usikose kutazama Makala Maalum ya Urasimishaji Makazi Holela mkoa wa Dar es Salaam kupitia Runinga ya TBC1 siku ya jumamosi tarehe 29 Mei 2021 kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano usiku hadi saa nne.
#kaziiendelee.