Mpiga gitaa wa Bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Mabera aliyeitumikia bendi hiyo kwa miaka 47 mfululizo amefariki baada ya kuugua kwa muda. Mabera Said mtoto wa marehemu amesema mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri Goba, Dar es Salaam.
“Nawaomba tuendelee kujenga umoja tusibaguane kwasababu ya Vyama, Dini wala Ukabila, sisi ni Taifa moja, Mwl Nyerere katuacha tukiwa wamoja, naomba Uchaguzi usitugawe, nawaomba Wana- CCM, CHADEMA, ACT, CUF na Vyama vingine vyote tushikamane” -JPM akiwa Ifunda
#HABARI Rais @MagufuliJP amemteua Dkt Eblate Ernest Mjingo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Dkt Mjingo amechukua nafasi iliyoachwa na Dkt Simon Mduma ambaye amestaafu.
Unga unaotokana na kusagwa kwa pembe ya faru hausaidii chochote kwenye kuongeza nguvu za kiume hivyo Watu waache hiyo imani, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi Kamishna Msaidizi Emmanuel Moirano amesema hiyo imani imesababisha ujangili mkubwa dhidi ya faru.
#Arushaoneupdates
Timu ya Taifa ya Tanzania #TaifaStars itacheza mchezo wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi Oktoba 11, 2020 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Kikosi cha Stars kitawekwa wazi Oktoba 2, 2020 na kocha wake Etienne Ndayiragije.
Patrick Aussems ameteuliwa kuifundisha Black Leopards FC ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu. Aussems amewahi kuvifundisha vilabu vya AC Leopards ya Jamhuri ya Congo na Simba SC ya Tanzania.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtaka mgombea urais (CHADEMA), Tundu Lissu afike katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa Septemba 29. NEC imesema baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli.
#VPL Kikosi cha kwanza cha @mtibwaofficial dhidi ya @yangasc1935 , leo Saa 10:00 Jioni.
1. Mshery
2. H. Ramadhan
3. Issa Radhid
4. Geofrey Kigi
5. Dickson Job
6. Baraka Majogoro
7. Joseph Mkere
8. Boban Zirintusa
9. Ibrahim Ahmada
10. Salum Kihimbwa
11. Haruna Chanongo
#PICHA Wafanyakazi wa klabu ya @SimbaSCTanzania wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na menejimenti wakiwa katika semina ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu maisha ndani ya klabu hiyo.
Mwingereza Chris Grailey (29) ambaye alinukuliwa mara kibao akisema corona ni ugonjwa wa kipuuzi ambao huwapata wapuuzi tu huku akisema hayo ni mafua tu yaliyochangamka, kwa sasa yuko hoi akiwa anapumua kwa msaada wa mashine ya Oxygen baada ya kupata corona .
FT: Brighton 2-3 Man United (Maupay 40’P March 90+4’) (Dunk 43 O.G Rashford 55’ Fernandes 90+10’P)
Man United wamepewa penati nyingi (24) katika mashindano yote toka msimu uliopita, 20 kati ya penati 24 wamefunga magoli na nne ndio wamekosa #Arushaonesports
#HABARI Kamati ya amani nchini inayoongozwa na Mwenyekiti wake na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa, imepiga marufuku makanisa na misikiti, kutumika kumfanyia kampeni mgombea yoyote wa chama cha siasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki waumini wake.
“Samatta @Samgoal_77 hajashuka bali amepanda, Fenerbahce ni Taasisi sio ya Soka pekee ukitizama ina Basketball, kuogelea, volleyball n.k wanashikilia rekodi ya kushinda Ubingwa wa Uturuki karibu mara 28, naimani atacheza kama alivyokuwa anachezeshwa Genk”-@Salym
Mahakama ya Kisutu imemuhukumu Rutyfiya Abubakary (Amber Rutty) na Mpenzi wake Said Bakary pamoja na James Delicious kulipa faini ya Milioni 11 ama kwenda jela miaka 5, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa 3 ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
#Arushaonefmtz