*RAIS SAMIA AMUASILI MTOTO MCHANGA ALIYETELEKEZWA NZEGA*
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto mchanga wa kike leo tarehe 11 Machi, 2026, katika makazi yake, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.
WANANCHI WAPONGEZA UONGOZI WA RAIS SAMIA KUPITIA PROGRAMU YA JENGA KESHO ILIYO BORA (BBT)
Wananchi wamepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia kwa kuanzisha na kuendelea kutekeleza Programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (Building a Better Tomorrow – BBT) kupitia Wizara ya Kilimo, inayolenga kuwahamasisha vijana na wanawake kujikita katika sekta ya kilimo.
Programu hiyo inalenga kuongeza uzalishaji wa mazao na kuboresha maisha ya vijana na wanawake kwa kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara. Kupitia mpango huo, vijana na wanawake wanapatiwa fursa ya kupata ujuzi wa kisasa wa kilimo pamoja na matumizi ya teknolojia ili kuongeza tija katika uzalishaji.
Aidha, programu ya BBT inalenga kuongeza ajira zenye staha nchini kwa kuwahamasisha vijana na wanawake kutumia kilimo kama chanzo kikuu cha kipato na maendeleo ya kiuchumi.
Wananchi wameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira yanayowawezesha vijana na wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo biashara, kwa kuwapatia utaalamu wa kilimo na kuwasaidia kuongeza mavuno pamoja na kipato chao.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
VITUO 36 KUTEKELEZA KITITA JUMUISHI CHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO DAR ES SALAAM
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia kupitia Wizara ya Afya imeanza utekelezaji wa Kitita Jumuishi cha Huduma za Afya ya Mama na Mtoto chenye lengo la kuimarisha ubora wa huduma za afya na kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga nchini.
Mpango huo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga kwa kuboresha huduma zinazotolewa katika vituo vya afya.
Katika utekelezaji wa mpango huo, jumla ya vituo vya afya 36 katika Mkoa wa Dar es Salaam vimechaguliwa kuwa vituo vya mfano vitakavyoonyesha utekelezaji bora wa huduma za afya ya mama na mtoto.
Aidha, mpango huo unahusisha usambazaji wa vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na utoaji wa mafunzo na mafunzo elekezi kazini kwa watoa huduma za afya ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinaendana na viwango vya kitaifa na kimataifa.
Kitita hicho kinazingatia huduma muhimu zinazohusu afya ya mama na mtoto kuanzia huduma za wajawazito kabla ya kujifungua, huduma wakati wa kujifungua, huduma za watoto wachanga pamoja na huduma za mama baada ya kujifungua, hatua inayolenga kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma salama na bora kuanzia kipindi cha ujauzito hadi baada ya kujifungua.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA YA UMEME LINDI NA MTWARA
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia imewekeza Shilingi milioni 704 kwa ajili ya kufunga transfoma ya ziada katika Kituo cha Kupooza Umeme cha Mahumbika mkoani Lindi, hatua inayolenga kupunguza changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Kupitia uwekezaji huo, uwezo wa kituo hicho umeongezeka na kufikia takribani MVA 35, jambo litakalosaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme na kuboresha huduma kwa wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi katika ukanda huo.
Ufungaji wa transfoma hiyo ni sehemu ya jitihada za muda mfupi za Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Sambamba na hatua hizo, Serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya muda mrefu ya kuimarisha miundombinu ya umeme katika ukanda huo. Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa kusafirisha umeme kutoka Songea kupitia Tunduru hadi Masasi na hatimaye kufika Mahumbika, ambao unatarajiwa kuongeza upatikanaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Aidha, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kusafirisha umeme kutoka Mkuranga kupitia Somanga na Kilwa hadi Lindi, ambao utaunganishwa na miundombinu ya usambazaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara, hatua itakayosaidia kuongeza uthabiti wa huduma ya umeme katika maeneo hayo.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
SHILINGI BILIONI 3.065 KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA YA TENGERU – NAMBARA (ARUSHA)
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia imejipanga kukamilisha ujenzi wa barabara ya Tengeru – Nambara mkoani Arusha katika mwaka wa fedha 2026/2027.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 3.81 inajengwa kwa kiwango cha lami, na Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ikiwa imetenga jumla ya Shilingi bilioni 3.065 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wake.
Serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo katika kuboresha miundombinu ya usafiri na kurahisisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo. Hadi sasa, ujenzi wa mita 500 tayari umeanza kutekelezwa.
Aidha, mapema mwezi Machi mwaka huu ujenzi wa mita 700 utaanza baada ya usanifu wake kukamilika. Tayari mkandarasi yupo katika eneo la mradi na anaendelea na utekelezaji wa kazi katika kipande chenye urefu wa kilometa 1.2.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia inaendelea na mradi wa ukarabati na uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga uliopo Mkoani Rukwa.
Mradi huo ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 60.1. Hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 96, hatua inayoonesha mafanikio makubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya usafiri wa anga katika eneo hilo.
Uboreshaji wa uwanja huo unatarajiwa kuimarisha huduma za usafiri wa anga, kuongeza fursa za biashara na uwekezaji, pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Rukwa na maeneo ya jirani.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Rais wa Kenya, Mhe. William Samoei Ruto, amepongeza mafanikio ya huduma za Treni ya Kisasa ya Mwendo Kasi (SGR) ya Tanzania, zilizoanza rasmi tarehe 14 Juni 2024. Ameeleza kuwa huduma hizo kwa sasa husafirisha wastani wa abiria 10,000 kwa siku kati ya Dar es Salaam na Dodoma.
Aidha, amebainisha kuwa huduma za usafirishaji wa mizigo kwa njia ya SGR, kutoka Kituo cha Pugu hadi Kituo cha Ihumwa (ICF), zilizoanza tarehe 27 Juni 2024, ni hatua ambazo zimeimarisha zaidi ufanisi wa usafiri na uchukuzi nchini.
Rais Ruto amesisitiza kuwa maendeleo haya ni hatua kubwa ya maendeleo kwa ukanda wa Afrika Mashariki, yakichochea biashara, usafirishaji na ushirikiano wa kiuchumi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Ninawapongeza na kuwatakia kheri wanawake wote katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Siku hii inatupa fursa ya kipekee ya kutambua, kujivunia na kusherehekea mafanikio tuliyopata, hasa katika elimu, afya, uchumi na uongozi.
Siku hii inatukumbusha pia wajibu wetu wa msingi kwa waasisi wetu na kwa vizazi vya sasa na vijavyo; wa kuendelea kupanga na kutekeleza mipango ya kumwezesha mwanamke, ikiwa ni sehemu muhimu ya kazi ya kukomboa familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutekeleza ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea michuano ya AFCON 2027 inayotarajiwa kufanyika nchini.
Ujenzi wa Uwanja wa Arusha unaendelea vizuri, vilevile ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na Uwanja wa Uhuru ukiendelea sambamba na maboresho ya viwanja vingine vya mazoezi.
Hatua hizi zinalenga kuimarisha miundombinu ya michezo na kuhakikisha maandalizi yote yanakuwa imara ili kuiwezesha Tanzania kuwa mwenyeji bora wa michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika. ⚽️🏟️
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Karibuni Tanzania.
Karibuni Nyumbani.
Leo nimejumuika na Marais wa nchi na Wawakilishi wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha.
Miaka 26 tangu kurejeshwa kwa umoja huu, umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuunganisha nguvu za nchi zetu kama ndugu, kuongeza sauti ya pamoja katika masuala mbalimbali, na kujenga mustakabali wenye mafanikio kwa wananchi wa Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt @SuluhuSamia akishiriki kikao cha ndani pamoja na baadhi ya Wakuu wa Nchi wanachama wa East African Community (EAC), kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa @jumuiya
Kikao hicho kimefanyika katika Arusha International Conference Centre (AICC) tarehe 07 Machi 2026, kikilenga kujadili masuala muhimu ya ushirikiano, maendeleo ya kikanda na mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #MaendeleoEndelevu #DiraYaSamia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia akiwasili katika Mkutano wa Ndani wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), tarehe 07 Machi 2026.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#TabasamuLaUtu #maendeleoendelevu
#diplomasiayakiuchumi #DiraYaSamia
SERIKALI YAIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME USHETU KUPITIA MRADI WA UMEME WA JUA KAYENZE
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. @SuluhuSamia inaendelea kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kupitia utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Jua wa Kayenze wenye uwezo wa kuzalisha megawati 5 (MW), uliopo katika Jimbo la Ushetu, mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri wa Nishati na Mbunge wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Salome Makamba, amesema mradi huo unazalisha megawati 5 za umeme zinazounganishwa katika Gridi ya Taifa kupitia njia ya msongo wa kilovolti 33 (33kV), hatua inayosaidia kuongeza upatikanaji wa umeme katika eneo la Ushetu na maeneo ya jirani.
Amesema mradi huo ulikamilika mwezi Mei mwaka 2025 na kuanza kutoa huduma mara moja, na hivyo kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme kwa wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi.
Mbali na uzalishaji wa umeme, Mhe. Salome Makamba amesema mradi huo pia umechangia maendeleo ya jamii kwa kujenga jengo la zahanati katika Kijiji cha Kayenze kwa gharama ya shilingi milioni 130.
Aidha, akizungumzia hali ya usambazaji wa umeme katika Jimbo la Ushetu, Mhe. Makamba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongoji 136 vya jimbo hilo.
Ameongeza kuwa vitongoji takribani 100 vilivyosalia vinatarajiwa kufikiwa na huduma ya umeme ifikapo mwaka 2030, jambo litakalosaidia kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Ushetu.
#KaziNaUtuTunasongaMbele #TabasamuLaUtu #maendeleoendelevu #DiraYaSamia
Leo tuponaungana na dunia kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani tunatambua mchango mkubwa wa wanawake katika kujenga familia, kuimarisha jamii na kuendeleza Taifa.
Kaulimbiu ya mwaka huu inatukumbusha kuwa maendeleo ya kweli yanajengwa juu ya haki, usawa na ushirikishwaji, pamoja na moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine.
Mwanamke ni mama, mlezi, kiongozi na nguzo muhimu ya familia na jamii. Hata katika changamoto, wanawake huonyesha ujasiri na hekima, wakigeuza changamoto kuwa nguvu ya kuijenga jamii na Taifa.
Heri ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa wanawake wote. 🌍✨
@ikulumawasliano@SuluhuSamia
#womensdays #DiraYaSamia #kazinaututunasongambele
Serikali inalenga kukamilisha korido nzima ya SGR ya Dar es Salaam–Mwanza na kuanza uendeshaji kamili wa huduma za reli hiyo ifikapo mwaka 2028, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Mradi wa Reli ya Kisasa ya Mwendo Kasi (SGR) unaounganisha Dar es Salaam na Mwanza una urefu wa takribani zaidi ya kilomita 1,300, Hadi kufikia Machi 2026, utekelezaji wa mradi huu umeendelea kwa kasi, ambapo vipande vingi tayari vimekamilika.
Kwa upande wa kipande cha mwisho (Lot 5: Isaka–Mwanza) chenye urefu wa kilomita 341, maendeleo ya ujenzi yamefikia asilimia 68.
Katika kipande hicho:
Ujenzi wa madaraja umefikia asilimia 90
Uwekaji wa reli (track laying) umefikia asilimia 53
Mafanikio haya yanamaanisha kuwa sasa zaidi ya asilimia 78 ya maeneo ya vijijini yameunganishwa na gridi ya taifa ya umeme. Hatua hii imeongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nishati kwa wananchi wa vijijini na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini
Serikali ya Tanzania, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme katika asilimia 100 ya vijiji vyote 12,318 vya Tanzania Bara kufikia mwaka 2020.