Asanteni sana Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) kwa kuniteua kuwa Mjumbe wa Kamati ya Tuzo za Wanamichezo bora nchini nchi ya Mwenyekiti wetu Jemedari Said Kazumari @jemedarisaid nashukuru sana kwa nafasi hiii 🙏🙏🙏
Simba SC imemtambulisha Kiungo Mkabaji Allasane Maodo Kante Raia wa Senegal ambaye amesajiliwa kutokea CA Bizertin ya Tunisia kwa Mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
FT: Pyramids 2-1 Mamelod (agg 3-2)
⚽️Mayele 24’
⚽️Samy 56’
⚽️Rayners 75’ #CAFCLFinal
Pyramids Mabingwa wa CAF Champions League kwa mara ya kwanza katika historia, hawa Pyramids ni kama Azam FC kwa hapa kwetu Tanzania, tunawaombe uwekezaji wenu siku ulipe
FT: Simba SC 1-3 Singida BS
⚽️Ahoua 49’
⚽️Sowah 17’
⚽️Kayeke 35’ 48’ #crdbankfederationcup
Fainali sasa ni Singida vs Yanga SC, itakuwa bonge la fainali kama kusipokuwa na rotation
Klabu ya Chelsea imetwaa Ubingwa wa Conference League baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Real Betis ya Hispania, Chelsea inakuwa timu ya kwanza kushinda Makombe manne Ulaya.
1- Uefa Champions League 🏆🏆
2- Europa League 🏆🏆
3- UEFA Super Cup 🏆
4- Conference League 🏆
FT: Simba SC 1-0 Singida BS
⚽️Mukwala 43’ #NPL
Simba SC wamalima vipori vya Ligi Kuu leo dhidi ya Singida na kufikisha alama 72 huku Yanga akiongoza kwa alama 73.
Wydad Casablanca wamemtambulisha rasmi Stephano Aziz Ki (29) kama Mchezaji wao mpya kuelekea michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu, Aziz amejiunga na Wydad akitokea Yanga SC kwa Mkataba wa miaka mitatu.
FT: Mamelod 1-1 Pyramids
⚽️Ribeiro 54’
⚽️Karti 90+4’ #CAFCL
Pyramids wanaleta ugumu wa kazi kwa mwenyeji Mamelod Sundowns, sasa fainali ya marudiano inachezwa katika uwanja wa 30 June Cairo.
RS Berkane wamewasili Zanzibar saa 3:00 usiku hadi sasa hawajatoka ndani ya uwanja wa ndege wa Abeid Karume wanamalizia taratibu za uingiaji nchini
NB: Simba waliwasili Morocco saa 12:00 asubuhi kwa saa za Morocco na kuruhusiwa kutoka Airport saa 5:00
GG inatoa 😂 #UbayaUbwela
Shirikisho la soka Burkinafasso limetaja kikosi cha Timu ya Taifa kinachojiandaa na michezo ya kalenda ya FIFA, Aziz Ki amejumuishwa katika kikosi ila anatambulika kama mchezaji wa Wydad ya Morocco na sio Yanga
Yanga wanasubiria Wydad wamtambulishe ili watoe taarifa rasmi
Kikosi cha RS Berkane ya Morocco tayari kimenza safari ya kuelekea Zanzibar kikitokea Oujda Morocco kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) dhidi ya Simba SC unaochezwa Mei 25 2025 katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Klabu ya Zamalek ya Misri inaelezwa kuwa imetuma ofa ya USD milioni 1 kwa Yanga SC kama sehemu ya kuwashawishi wamnunue Clement Mzize (21) kuelekea kuboresha kikosi chao msimu ujao, Yanga SC inajifikiria.
Tottenham Hotspurs Mabingwa wapya wa Europa League 2024/25, wamemaliza ukame wa kukaa miaka 17 bila Kombe lolote kabati kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Man United goli likifungwa na Johnson dakika ya 42.