Ahsanteni sana wanaharakati mlioko instagram, tiktok na Facebook. Kwa sasa mnalibeba jahazi sababu mimi na @MariaSTsehai tumenyimwa access na wananchi walio wengi….
Mnafanya kazi iliyotukuka…
Uanaharakati ni title ya kujivunia. Nyerere, Nelson Mandela wote walikuwa wanaharakati na harakati zao zikoleta uhuru kwenye nchi zao… LETS KEEP PUSHING
Nuruvazi, Tanzanite, Marcus,Vinepa, Uhuru na wengineo…..
🔥🔥💯
Ujumbe muhimu SANA SANA. kutoka Dada wa Taifa
Gen Z 🇹🇿 this is your moment to take back your country! Tunawasapoti all the way - nyie ni Taifa letu
Thank you so much sister @mangekimambi for this inspiring message - and you hit the nail on the head!
JUMUIYA YA MADOLA YATOA MSIMAMO KUHUSU TANZANIA.
Katika taarifa ya tarehe 20 Septemba CMAG imesisitiza yafuatayo:
1. Kuendeleza mchakato unaojumuisha pande zote, unaoaminika na unaowezeshwa kupitia ushirikiano kati ya vyama vya siasa.
2. Kulinda uhuru wa kiraia, uhuru wa kisiasa na uhuru wa vyombo vya habari.
3. Kuhakikisha taratibu za kisheria katika kesi ambazo bado hazijamalizika zinafanyika kwa haki, kwa wakati na kwa uwazi.
4. Kuweka mifumo inayoaminika ya kuhakikisha uwajibikaji, kutoa haki kwa walioathirika na kulipa fidia stahiki.
Tanzania itaendelea kubaki kwenye ajenda rasmi ya CMAG, huku Jumuiya hiyo ikiitaka Serikali kuweka tarehe ya mapema ya ziara ya Katibu Mkuu kwa ajili ya mazungumzo na Dikteta JIKE (Samia) na wadau wengine.
REPOST 200.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 433
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema tumesikia hoja za mshtakiwa na Mahakama inatamka kwamba shauri kwa upande wa utetezi limefikia mwisho.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kwa vile sasa kesi ya pande zote mbili imefungwa tunaomba Mahakama itupangie siku ya kuja kuwasilisha hoja za mwisho.
Sijawasiliana na upande wa mashtaka naomba nipendekeze tarehe yangu ya kuwasilisha hoja za mwisho.
Waheshimiwa Majaji natambua kwamba shauri limepangwa kuisha tarehe 25 September 2026 na mwenendo wa kesi una kurasa zaidi ya 1000, itakuwa kazi kubwa sana lakini naomba mimi kuanzia Jumatano ya tarehe 23 Septemba 2026 nitakuwa tayari kwa ajili ya kufanya final submission.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka mnasemaje?
Katuga: Tunaungana na mshtakiwa ila hajasema tufanye kwa maandishi au kwa mdomo.
Kwa tarehe aliyoipendekeza sisi tutajitoa Jumatano hiyo hiyo na sisi tutakuwa tayari kufanya final submission. Waheshimiwa majaji ingawa upande wa utetezi umefunga kesi ila tulikuwa na hamu sana ya kufanya cross kwa mashahidi wa Lissu waliokuwa wamebakia
Watu wanacheka sana, wanamuona Katuga kama kituko😂😂😂😂
Jaji Ndunguru: Hiyo amri mbona mahakama bado haijaitoa?
Tunakubaliana kuwa siku ya Jumatano shauri litakuja kwa ajili ya mawasilisho ya mwisho saa tatu kamili asbuhi
Imepigwa High Coooouuuuurrrrtttttt
Majaji wanatoka,
Mhe. Lissu anaangana na Mawakili wake pamoja na Viongozi wa Chama pamoja na watu mbalimbali waliojitokeza Mahakamani.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 18, 2026
Last time tuliishia part 431 so leo tunaendelea na -;
Part 432.
Mhe. Tundu Lissu ameingia Mahakamani watu wana vibe sana wanaimba Mwamba Mwamba huku wakipiga makofi mengi sana.
Majaji wote watatu wameingia na kuketi kwenye viti vyao.
Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama na kutambulisha jopo lake na kuwa wako tayari kuendelea.
Mhe. Lissu na yeye anasema niko tayari kuendelea.
Mhe. Lissu amesimama na kusema kwamba nimekutana na Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ambaye nilikuwa nimependekeza awe shahidi wangu wa leo, nimekutana nae Mahakamani kwenye chumba hiki hiki waheshimiwa majaji, naweza kuthibitisha kwamba ameheshimu wito wa Mahakama amekuja na nimezungumza nae kuhusu yeye kuwa shahidi wa upande wa utetezi na nimezungumza nae kiasi cha kutosha, baada ya kumueleza maeneo ambayo ningependa ayatolee ushahidi ameniambia kwamba yeye hawezi na hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wangu kwa maneno yake mwenyewe amesema
“Yeye yuko upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia”
Kwahiyo amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.
Nimemuelewa Waheshimiwa Majaji kama hayuko tayari siwezi kumlazimisha kutoa ushahidi ambao hataki kuutoa.
Waheshimiwa Majaji Kingai ameniambia kitu kingine kuhusiana na mashahidi wengine wawili IGP Camillius Wambura na CDF Jacob Mkunda, amesema vilevile hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama msimamo wao utakuwa ni huo huo kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kwasababu ile ile kuwa wako upande wa wale wanaoombea na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.
Katika Mazingira haya waheshimiwa majaji maana yake ni kwamba sina mashahidi zaidi kwahiyo naomba kufunga ushahidi kwa upande wa utetezi.
Ni hayo tu waheshimiwa majaji.
Naomba Repost yako.
Tundu Lissu; Waheshimiwa Majaji baada ya maelekezo ya Mahakama. Nimeonana na Msajili wa Mahakama hii. Amekuja kuniona kuniletea taarifa za summons za kuwaita mashahidi wa Mahakama
Tundu Lissu; Mheshimiwa Msajili amenitaarifu mashahidi wote watu walipelekewa summons Dodoma. Hata hivyo haikuwezekana kuwapa nakala za summons baada ya kusemekana wapo nje ya nchi
Tundu Lissu; Mheshimiwa Msajili anasema kati ya hao watatu mmoja ambaye ni Kamishina wa Polisi Afande DCI, Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi anatizamiwa kurudi nchini leo
Tundu Lissu; Msajili amenipa ahadi kuwa siku ya Ijumaa Kamishina wa Polisi atakuwepo Mahakamani kuja kutekeleza wito wa Mahakama. Wale wengine wawili ambao ni Jenerali Jacob Nkunda ambaye ni Mkuu wa Majeshi na IGP Camillius Wambura haijulikani watakuja nchini lini
Tundu Lissu; Katika hali ya namna hiyo napendekeza tuhairishe kesi hadi siku ya Ijumaa saa 8 na nusu mchana ili session ya asubuhi nitumie kushauriana na shahidi ikiwa ni pamoja na kuchukua maelezo yake.
Tundu Lissu; by saa 8 na nusu nitakuwa tayari kuendelea naye. Kuhusu waliobaki tusubiri tumalizane na aliyepo. Then tutafanya maamuzi
Tundu Lissu; Mwisho, nafahamu jinsi ambavyo ratiba ya shauri hili ilivyo, vilevile na mimi nataka sana twende kwenye final submission, ili tupate muda wa kusubiri uamuzi wenu. Kama watatii wito wa Mahakama na kuja imani yangu ni kwamba hatutochukua muda mrefu.
Tundu Lissu; Kama mpaka tunamaliza na huyu aliyepo tukimaliza na hawajaja nafikiri naweza kuwa na uamuzi kama bado nawahitaji au lah. Wasipokuja kabisa Waheshimiwa Majaji hilo litakuwa mikononi mwenu. Kwa sababu nyie ndiyo mlio toa summons, mimi ya kwangu ni hayo Mheshimiwa.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashtaka
Nassoro Katuga; Waheshimiwa Majaji kwa masikitiko sina pingamizi la kuhairisha kesi. Waheshimiwa nakumbuka Mahakama ilisema mwisho tarehe 18
Jaji: Hapana. Tarehe 26. Siku 14 za kazi.
Nassoro Katuga; Kwa maana hiyo hatupingi kuhairisha kesi. Tunaomba Mahakama hii imsisitize mshtakiwa mashahidi wake wafike kwa wakati.
MAHAKAMA; 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Jaji; si mashahidi wake jamani, yeye ndiyo anatakiwa kuwaleta Mahakamani. Wewe wanakuhusu nini?
Nassoro Katuga; Kwa hiyo Waheshimiwa tunaomba tusisitize mshtakiwa aweze kuwaleta. Tutakuwa tumepoteza siku ya leo nusu na kesho tungeweza kumaliza shauri
Nassoro Katuga; Suala la kama wasipofika anaiachia mahakama, Mahakama ifanye nini. Yeye ndiyo anatakiwa kuiomba Mahakama iwafanye nini
Jaji; Unaposema anaiachia Mahakama, Mahakama ifanye nini. Nimekumbuka ule msemo wako Mahakama siyo mama yako.
MAHAKAMA; 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Nassoro Katuga; Ni hayo tu Waheshimiwa Majaji.
Jaji; kwa hiyo shauri kwa leo linahairishwa hadi Ijumaa tarehe 18. Saa 8 kamili badala ya saa 8 na nusu.
Hii taarifa ni kubwa and beyond politics - this is a global human rights award
Tundu Lissu is more than deserving 🙏🏽
Tundu Lissu anastahili hii tuzo muhimu ya Sakharov ambayo ni ya kimataifa na si ya kisiasa bali ni ya kutambua harakati zake za haki za binadamu!
Tuzo ya Sakharov ni tuzo ya heshima kwa watu binafsi au makundi yaliyojitolea maisha yao kulinda haki za binadamu na uhuru wa mawazo. Tuzo hiyo, iliyopewa jina la mwanasayansi na mpingaji wa sera za serikali wa Urusi, Andrei Sakharov, ilianzishwa mnamo Desemba 1988 na Bunge la Ulaya. Orodha fupi ya wagombea huandaliwa kila mwaka na Kamati ya Mambo ya Nje pamoja na Kamati ya Maendeleo ya Bunge la Ulaya.
Tundu Lissu ni icon wa Taifa na anaelewa nafasi yake katika historia
Mungu aendelee kumwongoza ✊🏽
#FreeTunduLissu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 431
Tumerejea Mahakamani.
Imepigwa high court
Majaji wanaingia muda huu ili tupate mrejesho wa nini kinaendelea kuhusu wale mashahidi wengine.
Anasimama Katuga anasema Corum yao ni ile ile na mshitakiwa yupo na shauri linaendelea kwa utetezi na sisi tuko tayari.
Anasimama Mhe. Lissu anasema baada ya maelekezo ya Mahakama nimewasiliana na Mhe. Msajili wa Mahakama hii amekuja kuniona na kuniambia kuhusu utekelezaji wa amri ya Mahakama kuhusu kuwaita hao Mashahidi watatu.
Mhe. Msajili amenitaarifu kuwa Mashahidi wote watatu walipelekewa wito Dodoma, hata hivyo haikuwezekana kuwaserve nakala za summons kwasababu wote watatu wapo nje ya nchi.
Mhe. Msajili amesema kati ya hao watatu mmoja ambae ni Kamishna Wa Polisi Ramadhani Kingai, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai anatazamiwa kurudi nchini leo.
Na Msajili ameniahidi kwamba siku ya Ijumaa kamishna wa Polisi Kingai atakuwepo Mahakamani ili kutekeleza huo wito wa Mahakama.
Wale wengine wawili Jenerali Jacob Mkunda na Wambura IGP hawajulikani watarudi lini?
Katika Mazingira haya napendekeza Mahakama iahirishe shauri leo hadi ijumaa saa nane na nusu Mchana ili ile session ya asubuhi niweze kuitumia kushauriana na huyo shahidi ambae atakuja, ikiwa ni pamoja na kuchukua maelezo yake.
Na natumaini Waheshimiwa Majaji by saa nane na nusu tutakuwa tayari kuendelea nae na kuhusiana na waliobaki itabidi tusubiri tumalizane na huyu tuliyenae ili tufanye maamuzi baadae na hao wengine.
La mwisho ninafahamu jinsi ambavyo ratiba ya shauri hili iko tight na naomba niwafahamishe kuwa na sisi twende kwenye final submission ili muweze kukaa baadae kutafakari na kuamua kesi hii.
Vyovyote itakavyokuwa kama watatii wito wa Mahakama ni imani yangu kwamba hatutachukua muda mrefu.
Na wasipokuja kabisa hilo litakuwa mikononi mwenu maana nyie ndio mmetoa wito wa wao kuja kutoa ushahidi, Mimi ya kwangu ni hayo Waheshimiwa Majaji.
Katuga kwa masikitiko hatuna pingamizi la kupinga ahirisho na Mahakama ilipoongeza session hii hadi Tar. 18/09
Jaji Nduguru anasema sisi tuliongeza 14 working days.
Katuga: Basi tunaomba Mahakama imsisitize Mshitakiwa Mashahidi wake waweze kufika.
Watu wanasonya 😂😂 😂
Jaji Ndunguru: Sasa jamani hao si mashahidi wa Mshitakiwa mnaguna nini? Mshitakiwa anajua namna ya kufuatilia. Hebu uwe unawaelekeza.
Katuga: Pia kuhusu ombi lake la kwamba wasipokuja hao mashahidi anaiachia Mahakama hilo hawezi kuiachia kwasababu yeye ndio mashahidi wake na Mahakama imeshatoa summons kwahiyo atasema anaiomba nini Mahakama?
Jaji Ndunguru: Anacheka kwamba the court is not your nini ile huwa mnarushiana humu.😂
Majaji wanateta hapo kidogo.
Jaji Ndunguru: Tukutane Ijumaa saa nane kamili mchana.
Naomba Repost yako.
Kundi kubwa na lenye nguvu zaidi ya kisiasa ndani ya Bunge la Umoja wa Ulaya (The EPP Group) limependekeza jina la Tundu Lissu, kuwania Tuzo ya Sakharov 2026.
Tuzo hiyo ya Uhuru wa Kujieleza (kwa Kiingereza: Sakharov Prize for Freedom of Thought) ni heshima ya juu zaidi inayotolewa na Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kutambua watu binafsi, vikundi, au mashirika ambayo yamejitolea maisha yao kutetea haki za binadamu, uhuru wa kujieleza, demokrasia na kuhimiza utawala wa sheria.
EPP imeeleza kuwa Tundu Lissu ni kielelezo halisi cha utetezi wa demokrasia, siasa za vyama vingi, utawala wa sheria na uhuru wa kimsingi, kwa gharama kubwa sana za maisha yake binafsi, huku wakiongeza kuwa anawakilisha muunganiko thabiti wa ujasiri, msimamo na umuhimu wa kijiopolitiki.
Mshindi wa tuzo hii ukabidhiwa cheti cha heshima (diploma) pamoja na zawadi ya fedha taslimu kiasi cha Euro 50,000 (sawa na takriban shilingi milioni 150+ za Kitanzania), na hafla ya kukabidhi tuzo hii hufanyika mwezi Desemba kila mwaka, katika ofisi za Bunge la Ulaya mjini Strasbourg, Ufaransa.
Watu wengi ambao wameshinda tuzo hii ni wale waliopitia mateso, vifungo, au hatari kubwa kwa ajili ya misimamo yao. Baadhi ya waliowahi kushinda tuzo hii ni pamoja na:
Nelson Mandela na mwanaharakati wa Urusi Anatoly Marchenko (Hawa ndiyo walikuwa washindi wa kwanza kabisa mwaka 1988).
Malala Yousafzai (Mwanaharakati wa elimu kwa watoto wa kike kutoka Pakistan - 2013).
Kofi Annan na wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa (2003).
Kuteuliwa kwa Tundu Lissu kuwania tuzo hii kunamuweka kwenye orodha ya watu wanaotambuliwa kimataifa kwa kupigania demokrasia licha ya changamoto kubwa wanazopitia.
REPOST 200
Video ya kwanza ikionesha Mangi aliyepigwa mkwara na kumuacha Mwenyekiti BAVICHA akidharirishwa.
Video ya pili ni mama mmoja aliyejitosa kwenda kumtoa kijana aliyeluwa akipigwa na polisi.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 430
Mhe. Lissu anasema amemaliza maswali ya Re Examination.
Job Mrema amesimama na kusema tunaleta chini ya kifungu cha 156(4) cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6.
Mahakama itumie mamlaka yake ili tuweze kumrecall na kufanya further cross examination na kwa mujibu wa kumbukumbu siku ya jana alitoa ushahidi wake hapa Mahakamani kuhusiana na shauri hili na akiwa chini ya kiapo alitoka Mahakamani na kwenda kuzungumza na kuzalisha ushahidi mwingine.
Tunaona ushahidi huo utaisaidia Mahakama kutenda haki na alikwenda kusema akiwa chini ya kiapo. Tupewe nafasi tumuulize maswali kuhusu ushahidi huo aliousema na Naomba kuwasilisha.
Anasimama Mh. Lissu amekunja sana uso.
Majaji wanasema kaa kwanza mshitakiwa. tunataka kujua mambo kadhaa.
Jaji Ndunguru anauliza sasa mtu akiapa Mahakamani kwahiyo akienda hata nyumbani anakuwa chini ya kiapo? Hebu tusaidie kuelewa.
Watu wanacheka sana 😂😂😂
Job Mrema: Waheshimiwa Majaji kiapo amelala nacho kwasababu alipoapa alikuwa nacho, akifika hapa anaambiwa kiapo chapo kinaendelea.
Kwahiyo shahidi huyu afanyiwe further cross examination, sisi tumeangalia ni kwamba moja ya sababu yuko kwenye kiapo na kiapo chake hakijasitishwa, shahidi huyu akiwa bado kwenye kiapo. Amezalisha ushahidi.
Jaji Ndunguru anateta na wenzake hapo.
NB. Katuga mjinga ila kwenye hili naona ujinga wake umemtuma asiliseme hili yeye amuache kilaza Job Mrema. Huyu Mrema kwa kumbukumbu zenu ni miongoni mwa Mawakili waliokwenda kutetea ndege za Tanzania zilizokuwa zimezuiwa Afrika ya Kusini halafu Serikali ikaangukia pua na Kingereza chake kilikuwa ni ZE ZE ZE ZE ZE Mwanzo mwisho. Nitawatafutia ile video niwatumie hapa muone kiwango cha ukilaza.
Jaji Ndunguru: Tulikuwa tunaangalia off record.
Cross Examination inatokana na examination in chief sasa kama kitu kimeongelewa huko kwani kipo hapa Mahakamani??? Hilo pia la kwamba kiapo ameenda nacho hadi nyumbani hiyo tafsiri yako haiko sahihi, Ushahidi uko Mahakamani na mnamuuliza mambo yaliyosemwa Mahakamani.
Hayo mengine hayapo Mahakamani. Kwahiyo ombi hilo halina mashiko.
Mhe. Lissu anasimama anasema Waheshimiwa Majaji niliomba summons kwa ajili ya mashahidi kwahiyo nataka kujua majibu kuwa mashahidi hao wako wapi na tunakwendaje mbele.
Pia siwezi kumuweka shahidi kizimbani kabla sijamuanda kwahiyo lazima nikutane nao na niwaelekeze cha kufanya ili wakija kugeuka hapo kizimbani basi niwashughulikie sawasawa.
Eneo la kuwaandalia Mashahidi na kukutana nao ni hapa hapa Mahakamani kwasababu sina eneo lingine ambalo naweza kukutana na mashahidi wangu.
Siwezi kwenda ofisini kwao wala gerezani so nilazima tuonane na kupanga hapa hapa Mahakamani.
Jaji Ndunguru anasema tulitegemea utuambie kuwa una shahidi au hauna maana ni mashahidi wako na Mahakama ilishatoa summons kwahiyo tutabreak ili msajili atupatie feedback.
Tukutane saa tano na dakika aroboini.
Naomba Repost yako.
Kwa kuwa umeshika msimamo sahihi utatetewa na wapenda haki wote na Mungu atakupigania!
Hata asiyejua siasa ameona nguvu kubwa inayotumika kutaka kukuchafua na kukutoa kwenye reli - kosa lako ni kuweka msimamo mliokubalina na mwenyekiti wako Tundu Lissu kukataa kuridhiana kwenye giza au kumwangukia kimama mwuaji!
Many people do not appreciate what you do lakini usikate tamaa! Tunaelekea ukingoni na ukweli utasimama!
Hii vita tumeshashinda - mwambie Lissu - simameni hivihivi pamoja na imara - sisi tunawaamini! Hizi kelele zingine just Ignore! Just focus!
Nani alileta Uvumi kwamba Heche anaongea na mkuu wa Usalama mpaka kupewa Passport ?
1. Issue ilianza na wewe kutoa salamu za Lissu vijana wakakupiga Spana, kuhusu kujikomba sana kwa Samia
2. Ukajibu hiyo tweet ya @Sativa255 kuonyesha mtu mwenye mahusiano na mfumo ni @HecheJohn anaongea na mkuu wa usalama wa Taifa
3. Ukapigwa sana kama mpira wa kona,
4. Ukarudi na kutukana watu kuhusu Keyboard na Mic
4 . Ukachapika tena sana tu kuliko mwanzo , ulipigika vibaya sana na tuhuma nyingi unaishi Sea Cliff ambapo unasema unafanya biashara na ujakana kuwa hapo Sea Cliff ambapo umeonana sana Vicent mdogo wake Lissu kumshawishi namna ambavyo uongozi wa Sasa wa CHADEMA una fail kumsaidia Lissu, na kwamba wewe una access na mfumo kumtoa
5 . ukaitisha Press Fake baada ya watu kukulima sana hapa ndani ,
6.Sasa umeligeuza Suala la CHAMA ukaomba Mnyika akutupie Taulo na hii kazi ameifanya mara nyingi wakati suala ni lako sio la CHAMA
7. Asubuhi umekuja na huu ujumbe kwamba uma cancel umepata pa kutokea sasa
Ila ukiongea na Watu unasema Heche ameogopa sana amekuomba uache
Lema wewe siasa zako za janja janja acha utoboi uwezi wamudu wananchi , hakuna mwana siasa anayemudu wananchi especially wewe
Ulipewa Lift tu kama kigogo ukajipa utukufu, huna huo utukufu
Ujajibu tuhuma za sea cliff zote wala kufafanua chochote
Shukuru mnyika amekurushia taulo kwa kupotosha Video ya @mangekimambi
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 16, 2026
Last time tuliishia part 428 so leo tunaendelea na -;
Part 429
Mahakama imeanza.
Imepigwa high coooooourt
Majaji wameingia.
Mhe. Lissu nae ameingia kama kawaida makofi mengi yanapigwa mengi kwa ajili ya kumkaribisha Mwenyekiti Tundu Lissu.
Katuga anawatambulisha wenzake.
Jaji Ndunguru anasema tuendeleee.
Anasimama Mhe. Tundu Lissu anasema naomba kuzungumza kidogo na shahidi wangu naona amenitumia ujumbe hapa kabla hatujaendelea na nitamfuata.
Wanaenda kuzungumza Mhe. Lissu na Mhe. Heche pale kwa dakika kama tatu.
Wanaongea na kutikisa vichwa wamekubaliana wamemaliza na Mhe. Lissu anarejea kwenye kizimba chake.
Majaji wanazungumza kama dakika tano sijui wanajadili nini?
Mhe. Lissu: Shahidi kuhusu suala la Utekaji na ripoti ya SADC.
Heche: Hilo suala la Utekaji ukurasa wa 6 wa ripoti hiyo unazungumzia masuala ya Utekaji.
Katuga: Ukurasa wa 6 hakuutaja wakati wa kutoa ushahidi huo.
Mhe. Lissu: Tusipotezeane muda toa neno ukurasa wa 6.
Heche: Suala la Utekaji lipo kwenye ripoti ya SADC ukisoma utaona.
Mhe. Lissu: Ulisema maneno ya utekaji, kukinukisha kwamba sio kila mahali nilitumia hayo fafanua?
Heche: Nilimaanisha maudhui ni yaleyale kuzungumzia mfumo wa Uchaguzi. Choice of words tu ndio lilikuwa ni suala linalotofautiana.
Mhe. Lissu: Kuhusu Uchaguzi wa Tarime ukasema haukuwa huru na haki na hivyo hupaswi kuwa Mbunge na haukuwa na mamlaka hayo ya kukataa kuwa mbunge au hukuwa na huo uwezo?
Katuga: Hatukuuliza hivyo.
Mhe. Lissu: Rekodi zituongoze.
Jaji: Sikuwa na uwezo wa kukataa kuwa Mbunge
Heche: Ufafanuzi wangu ni kwamba returning officer ndio anatangaza Mbunge.
Mhe. Lissu: Mkurugenzi wa Uchaguzi akawa mgombea na sasa ni Mbunge wa Butiama na ukasema haikuwa sahihi. Fafanua?
Heche: Nilisema kwamba kanuni za CCM zinataka mwanachama wake ili agombee anapaswa kuwa na uanachama wa miaka mitano.
Kwahiyo naamini alijiunga na CCM akiwa bado ni Mkurugenzi wa Tume maana asingeweza kuruhusiwa kugombea ikiwa takwa la miaka mitano bado hajakidhi.
Mhe. Lissu: Tume ya Chande uliulizwa kuhusu wewe au Chama kuitwa. Na ukaoneshwa na mabarua mengi lakini ukasema hukuitwa. Fafanua. Usiingize mambo mapya Wakili wa Serikali atanuna.
Heche: Mimi sikupokea barua yoyote ya Mwaliko kutoka tume ya Chande na kuhusu Chama hakikupokea maana kilikuwa kimefungiwa.
Katuga: Kuhusu chama isiingie maana hakusema hivyo.
Mhe. Lissu: Tusomewe record inasemaje?
Jaji Ndunguru: Alipoitwa na tume ya Jaji Chande. Barua ilikuwa ameandikiwa Katibu Mkuu na haikuandikwa kwa Chama.
Heche: Haikuwa addressed kwa Chama.
Mhe. Lissu: Uliulizwa na maswali kuhusu Chama kwenda Bungeni na kutoa maoni kuhusu muswada wa Sheria. Kuhusu kuwaondoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi.???
Heche: Bado watumishi wa umma ndio wanasimamia Uchaguzi na mapendekezo yetu yalikuwa ni Tume kuwa na Wafanyakazi wake kuanzia ngazi ya kitaifa hadi chini na sio watumishi wa umma.
Mhe. Lissu: Kuhusu Thabo Mbeki Foundation na Mwalimu Nyerere Foundation tofauti yake. Fafanua
Heche: Thabo Mbeki Foundation inafanya kazi nchi zaidi ya moja tofauti na Mwalimu Nyerere Foundation ambayo inafanyakazi Tanzania tu ndo maana nilisema yenyewe ni International.
Part 430 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 425
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche
Katuga: Waambie Majaji kuhusu kama Chadema mlikuwa tayari kutoa ushirikiano kwenye Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29..?
Heche: Hatukuwa tayari kwasababu hatukualikwa
Katuga: Ni ushahidi wako kuwa hamkuikubali Tume ya Jaji Chande?
Heche: Ndio
Katuga: Kwa jibu lako kuwa hamkuwa mmeikubali Tume ya Chande nitakuwa sahihi nikisema hamkuwa tayari kuipa ushirikiano?
Heche: Sijui.
Katuga: Kwa jibu lako, ni kweli ulikuwa hujui kama Chadema mlikuwa tayari au hamkuwa tayari kutoa ushirikiano?
Heche: Ni kweli
Katuga: Ulipata wapi mamlaka ya kumjibu mshtakiwa kuwa Tume ya Chande haikuwaita?
Heche: Ni kweli haikutuita.
Katuga: Mihimili ya dola ni ipi?
Heche: Bunge, Serikali na Mahakama
Katuga: Unajua ni jukumu la serikali kusimamia sheria..?
Heche: Najua
Katuga: Unajua ni Serikali ndio ina jukumu la kumshtaki mtu yeyote aliyevunja sheria?
Heche: Ni sahihi
Katuga: Unajua Jukumu la kulinda amani limekuwa vested kwa Serikali…?
Heche: Najua
Katuga: Waambie Majaji kama unajua ama hujui kuchoma kitu cha mpira unakifanya kitoe harufu???
Heche: Inategemea kitu chenye harufu kitatoa harufu kama hakina harufu hakitoi harufu
Katuga: Waambie Majaji kuchoma matairi yanafanya yatoe harufu?
Heche: Sijawahi kuchoma matairi kwahiyo sijui.
Katuga: Unajua au hujui kuna njia nyingi za kukifanya kitu kinuke au kukinukisha?
Heche: Sijui
Katuga: Unajua moja ya njia ya kukifanya kitu kinuke ni kukichoma???
Heche: Sijui
Katuga: Nilikusikia ukisema kuwa ulimsikia P17 yeye ndio alichapisha hotuba ya 3/4/2025.??
Heche: Niliskia
Katuga: Ulimsikia akisema kupitia wewe sisi tumechapisha?
Heche: Sikumsikia
Katuga: Unakumbuka au Hukumbuki kuwa P3 (PW13) alisema yeye alipanga kuzuia uchaguzi kwa kurusha mawe.
Heche: Sikumbuki
Katuga: Unapotisha kuvunja amani unakuwa unamtisha nani?
Heche: Sijui.
Katuga: Ulieleza kuwa kwenye hotuba ya Jaji Chande hakuna majina ya watu waliouwawa au waliokufa
Heche: Ndio
Katuga: Uliisoma hotuba ya jaji Chande?
Heche: Ndio niliisoma.
Katuga: Unajua au hujui taarifa rasmi ya jaji Chande ilikabidhiwa kwa Rais.
Heche: Najua alisema anamkabidhi na alisema ni ya kwake.
Katuga: Ushahidi wako ni kwa mujibu wa hotuba au taarifa rasmi?
Heche: Unatokana na hotuba na taarifa ile aliyoisoma.
Katuga: Unajua au hujui Chadema kupitia kwa Katibu Mkuu John Mnyika kilialikwa na kilishiriki kutoa maoni kuhusiana na mabadiliko ya sheria za uchaguzi
Heche: Najua.
Katuga: Unajua au hujui kuwa Kati ya mapendekezo ya Chadema ya kutowashirikisha watumishi wa umma kwenye uchaguzi kulipelekea Mabadiliko ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Uchaguzi
Heche: Hayo sio mapendekezo yetu, mapendekezo yetu yalikuwa juu ya mfumo mzima.
Katuga: Unajua au hujui kwamba mwaka 2024 kifungu cha 6 cha Sheria kilibadilishwa na kuondoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi?
Heche: Najua kilibadilishwa na kusema watumishi waandamizi ndio watasimamia uchaguzi.
Katuga: Waambie Majaji kama uliiambia Mahakama hii kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 ulikuwa mahabusu Mtumba.
Heche: Ndio nilikuwa mahabusu.
Katuga: Ulisema ulipotoka mahabusu uliambiwa na watu kuhusu vurugu zilizotokea na hotuba ya Chande?
Heche: Sahihi
Katuga: Huu ni ushahidi wako au kwa mujibu wa hotuba ya Chande?
Heche: Hotuba ya chande
Katuga: Ni sahihi ulisema kuwa kipindi hicho ndio watu wengi waliuwawa?
Heche: Ni kweli
Katuga: Ni sahihi kuwa mali zenye thamani nyingi zilichomwa?
Heche: Sikumbuki ila alisema zina thamani fulani.
Katuga: Ni sahihi kuwa mali nyingi sana ziliharibiwa?
Heche: Sina ufahamu
Katuga: Unajua kuwa 70% ya waliokamatwa baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025 alisema kuwa walichocheka na hotuba zenu?
Heche: Sijui wewe ndio unaniambia
Katuga: Unamjua Katibu wa Chadema kata ya Mikocheni?
Heche: Simjui
Part 426 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako