SOUTH AFRICA KILA MARA WATANZANIA WANAUWAWA.
Jana amefariki huyu Jamaa anaitwa JOE ZAMU ni mzaliwa wa Arusha.
Huyu jamaa amefariki kwa kuchomwa moto mjinj Cape Town akiwa ndani na mwanamke wake wa kiSouth Africa jamii ya Kaladi.
Kaladi ni wale machotara wa ki South Africa ambao wengi wao wamechanganya damu baina ya mtu mweusi na Mzungu, Muhindi au Mwarabu kisha akazaliwa mtoto.
Joe pamoja na mwanamke wake wamefariki hapo hapo kiasi cha kushindwa kutambulika yupi ni Yupi, na wamechomwa moto na raia wa South Africa 🇿🇦
Mpaka sasa Jamii ya Watanzania wanaoishi South Africa wanawatafuta ndugu zake na Joe ili wawape utaratibu juu ya ufanyaji DNA ili kuweza kutambua mwili wa Joe Zamu ni upi.
Hii si Mara ya Kwanza, Karibu kila Mwezi kuna Raia wa Tanzania anauawa South Africa, Na jamii ya Watanzania waishio South Africa hushirikiana Kwa Kila kitu.
Joe ana tambulika kuwa nyumbani kwao ni Arusha kwa maelezo ya marehemu kipindi cha uhai wake.
kwa yoyote yule mwenye details za Joe Zamu kuhusu familia yake anaombwa kuwasilisha taarifa kupitia namba hiyo chini.
+255763005575
Mohamed Taibalh Hamza Msangi