KINDA WA TANZANIA ALIYETWAA TUZO YA MFUNGAJI BORA WA AFCON U17
Dismas Shida Athanasi mwenye umri wa miaka 14 alitwaa tuzo ya Mfungaji Bora (Golden Boot) ya AFCON U17 licha ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika mashindano hayo.
Kijana huyo aliisaidia Tanzania kufika fainali ya AFCON U17 na kufuzu kwa Kombe la Dunia la U17. Tayari ameanza kuvutia klabu mbalimbali kutoka Ulaya zinazotaka huduma yake.
Shida amekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika mashindano yote (alizaliwa tarehe 26 Desemba 2011). Alikuwa akicheza dhidi ya wachezaji wenye umri wa miaka 16 hadi 17 huku yeye akiwa na miaka 14 pekee. Kipaji halisi kwa umri sahihi.
NINI MAONI YAKO?
Huyu Aje CHADEMA kwa lipi wakuu,
Huyu kama anakuja aje kama mwanachama wa kawaida, Kitendo cha kumkaribisha anaonekana kama ana uspecial fulani, Hapana
Nani ajuaye? Labda Yuda hakuwa na nia mbaya sana dhidi ya Yesu. Huenda alifikiri anawapiga changa la macho Wayahudi. Alijua Yesu ni mtu wa miujiza, mwenye uwezo wa kujinasua katika hali yoyote. Pengine aliamini atachukua vipande vyake 30 vya fedha, huku Yesu akiwashangaza tena waliokuja kumkamata.
Anyway , CCM haipo tena. TUBU na karibu CHADEMA. Umetukanwa sana. Dhihaka hiyo hapaswi kufanyiwa hata Mwenyekiti wa TAWI.
@princebetrody Hizo ni Grift roller, kuna nyingine unatumia kama msasa, nyingine kama steel wire, matumizi yake ni kitoa kutu au kitoa rangi kwenye kuta au bati unapotaka kufanya marekebisho.
Zina machine yake hii ndio unazifunga.
Kleruu alizikwa kwa heshima zote mkoani Kilimanjaro. Ili kuuenzi mchango wake, serikali ilijenga mnara wa kumbukumbu Isimani na kukipa jina lake Chuo cha Ualimu cha Kleruu kilichopo Iringa. Aidha, mwanamuziki nguli Mbaraka Mwinshehe alitunga wimbo maalumu wa kumuenzi na kumlilia.
Hata hivyo, muda huponya majeraha ambayo awali huonekana kutoweza kupona. Miaka mingi baadaye, tukio hilo la kusikitisha liligeuka kuwa somo la upatanisho na msamaha wa kitaifa. Baada ya miongo kadhaa ya uhasama wa kimya kimya, familia za Mwamwindi na Dkt. Kleruu zilikutana, zikapeana mikono ya heri na kusameheana yaliyopita.
Kama ishara kubwa ya upatanisho huo na namna jamii ilivyoweza kusonga mbele, mtoto wa Said Mwamwindi, Ndugu Amani Saidi Mwamwindi, alikuja kuwa Meya wa Manispaa ya Iringa kwa kipindi kirefu, akiongoza mji ule ule ambao baba yake alihusishwa na tukio lililotikisa taifa miaka ya sabini.
Dkt. Wilbert Kleruu: Kisa cha Mkuu wa Mkoa Msomi na Mkulima wa Iringa
Imeandikwa na @Chakushangaza
Ilikuwa siku ya Sikukuu ya Krismasi, tarehe 25 Desemba 1971, mkoani Iringa. Tofauti na viongozi wengi wa ngazi yake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Katibu wa Chama cha TANU, Dkt. Wilbert Kleruu, hakuwa mtu wa kupumzika. Akiwa amezaliwa mwaka 1929 huko Mwika, Kilimanjaro, Kleruu alikuwa lulu ya kipekee katika serikali changa ya Rais Julius Kambarage Nyerere. Alikuwa msomi wa kiwango cha juu aliyekuwa ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sayansi ya Siasa na Uchumi wa Kilimo nchini Marekani mwaka 1962.
Mapenzi yake makubwa kwa falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea yalimfanya aaminiwe kwa dhati na Mwalimu Nyerere, hasa baada ya kuonyesha mafanikio makubwa mkoani Mtwara kwa kuanzisha takribani vijiji 750 vya Ujamaa ndani ya muda mfupi. Mafanikio hayo ndiyo yaliyomfanya Nyerere kumhamishia Iringa mwaka 1971 ili akabiliane na kile kilichoitwa βukabailaβ mfumo wa wakulima matajiri waliomiliki maelfu ya ekari za mashamba na matrekta katika eneo la Isimani, ambao hawakuwa tayari kuhamia katika mfumo wa vijiji vya ushirika.
Siku hiyo ya Krismasi, Dkt. Kleruu aliwaruhusu dereva na wasaidizi wake kwenda kusherehekea sikukuu pamoja na familia zao. Yeye mwenyewe, akiwa na njaa na uchovu, alishika usukani wa gari lake la kazi aina ya Peugeot 404 na kuelekea katika Kijiji cha Ujamaa cha Ndolela, ambako alishinda siku nzima akilima na kupanda mahindi bega kwa bega na wanakijiji.
Wakati akirejea Iringa mjini jioni hiyo, alipita katika Kijiji cha Mkungugu na kumkuta Said Abdullah Mwamwindi, mkulima tajiri mwenye umri wa miaka 28, akilima shamba lake kubwa kwa kutumia trekta. Dkt. Kleruu, ambaye alijulikana kwa msimamo mkali, kauli za kunyoosha mambo na wakati mwingine matumizi ya lugha kali dhidi ya wale aliowaona kama wazembe, alisimamisha gari na kwenda kumhoji Mwamwindi kuhusu sababu za kuendelea na kilimo cha kibinafsi na kile alichokiona kuwa ni kukaidi sera za kijamaa.
Hapo ndipo dhoruba ilipoanza. Majibizano makali yalizuka na baadaye kuvuka mipaka. Masimulizi ya tukio hilo yameendelea kutofautiana kwa miaka mingi. Wapo wanaosema kuwa Kleruu alimchapa Mwamwindi kwa fimbo mbele ya wake zake, huku wengine wakidai kuwa alipiga teke makaburi ya wazazi wa Mwamwindi yaliyokuwa katika eneo hilo la shamba, jambo ambalo lilihesabika kuwa mwiko mkubwa katika mila za Wahehe.
Hasira zilipopanda na kufikia kilele chake, Mwamwindi alikimbilia ndani ya nyumba yake huku Kleruu akimfuata akidhani kuwa alikuwa akikwepa mahojiano. Ghafla, Mwamwindi alitoka akiwa na bunduki ya kuwindia (shotgun) na kumfyatulia risasi ya tumboni Mkuu huyo wa Mkoa. Dkt. Kleruu alianguka chini na kufariki dunia papo hapo.
Baada ya tukio hilo, Mwamwindi alionyesha utulivu uliowashangaza wengi. Aliubeba mwili wa Dkt. Kleruu na kuuweka katika siti ya mbele ya gari lile lile la serikali. Kisha akaliendesha gari hilo hadi Kituo Kikuu cha Polisi cha Iringa mjini, akipita mbele ya askari wa usalama barabarani waliokuwa wakilisalimia gari la Mkuu wa Mkoa bila kufahamu kilichokuwa kimetokea. Alipofika kituoni, alikabidhi bunduki hiyo na kusema maneno yaliyobaki katika kumbukumbu za historia:
"Kachukueni mbwa wenu kwenye gari, nimeshammaliza."
Habari hizo zilileta simanzi nzito nchini na kumliza Rais Nyerere kwa kumpoteza mmoja wa wasomi na viongozi aliowategemea sana. Msako mkubwa ulifanyika na kupelekea kukamatwa kwa watu wapatao 23, wakiwemo baadhi ya wakulima matajiri pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC).
Licha ya wakulima wenzake kuchanga maelfu ya dola kwa ajili ya kumtafutia Mwamwindi mawakili wabobezi kutoka nje ya nchi, jitihada hizo hazikuweza kubadilisha mwelekeo wa kesi. Hatimaye, Mwamwindi alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa. Inasemekana kuwa Mwalimu Nyerere aliisaini hukumu hiyo mara moja, ikiwa ni miongoni mwa hukumu chache sana za kifo alizowahi kuzisaini katika kipindi chake cha urais.Dkt.
πππ