Watanzania tupende kuheshimu Mawazo ya Mtu. Mwalimu Nyerere alisema Ccm sio Mama yangu au Baba yangu. Watu usio weza kuwaacha ni wazazi hawa wawili tu.tusipige rungu mtakwa ya Mtu. Mimi Lazima niwe Mkweli Nashindwa kumwelewa Mtu anae sema hakuna Mungu huyu ndio shida kwangu.
Watanzania kila Mtu kwa Dini yake anatakiwa kuliombea Taifa Letu Mema, Neno La Mungu linasema Heri wapatanishi wataitwa wana wa Mungu, tukae tuondoe Tofauti zetu kama Taifa na Watoto wa Baba Moja,Neno La Mungu linasema hajishushae atakwezwa. Kujishusha sio Ujinga Ni Hekima .
Sijawai kuwa mwana chama wa chama Siasa ni mchambuzi Na Mshauri wa Siasa Miaka 30 ,Amani ni Tunda La Haki na Haki uinua Taifa na Mungu ni Mungu wenye Haki. Watanzania wenzangu Shetani Yuko kazini Tusimpe Nafasi kuliharibu Taifa Letu, Tusipo ziba hufa tutajenga ukuta.
Niombi Langu kwa Mungu Taifa Langu Tanzania liwe Salama salimini, Upepo Huu Wa kisiasa huweze kupita Salama , tukae kama watu wa Taifa Moja kuondoa tofauti zetu,tusitumie Nguvu, Tutumie Akili na Maarifa. Tunao Nchi zilizo fanya Makosa leo zinajuta, Mungu tusaidie.
Wanasiasa wote Wa pande zote mbili , Tanzania , Sipo angali dhambi hii ya kuharibu Tanzania mtaibeba Nyie Nchi mmeikuta toka Mikono Salama ya waasi wa Taifa Letu , tunu hii ya Amani ,Haki , upendo na umoja wa Taifa letu inazidi kuwepo, Bila kujali tofauti zetu kivyama vya Siasa.
Nitakuwa Wa Mwisho kukubali kwamba kama Watanzania Tumeshindwa kumaliza tofauti zetu za kisiasa Mezani. Tukaanza kutumia Nguvu kutatua Matatizo yetu ndani ya Nchi yetu, wakati Mungu ametupa Hekima na Busara, tumetatua Matatizo ya majirani zetu, harafu ya kwetu ya tushinde.
Hatuna Tanzania ingine ya kukimbilia Hii Nchi tulipewa na Mungu , unaweza kubadili Dini yako lakini huwezi badili utaifa wako wa asili. Naomba tukae kama Taifa tuondoe tofauti zetu asiye taka kushindwa sio Mshindani, tusimpe faida shetani na Maadui wetu. Mungu ibariki Tanzania.
Rais Samia Suluhu , Nina kuomba sana , Mheshimiwa Rais , kaa na Usalama wa Taifa na vyombo vingine vya usalama, tuondoe tofauti zetu ndani ya Nchi yetu nzuri, Naona tunako Elekea tuwe wa kweli si kuzuri sana , hata Mungu anapenda Madhiano. Sina chama ni Mzalendo wa kweli.
Mungu ya saidie Mataifa yetu na viongozi wake watatue Matatizo ya Nchi zao kwa kukaa Mezani na wapinzani wao. Mungu ana penda sana upatanishi kuliko kutumia nguvu za vyombo vya Usalama . Haki uinua Taifa. Hata Mungu aliye umba Dunia ana mpinzani Shetani.
Rais Samia suluhu, Mimi ni mpenda haki na Amani, pia Ni mchambuzi wa Siasa Muda Mrefu, Naomba kaa na vyombo vya usalama wa Taifa , waliopo na wastaafu watoe Ushauri wao, pia kama hautajali waite , Mawaziri kuu wastaafu na Rais Mstaafu, kurudisha Amani na umoja wetu. 🙏🏽🙏🏽
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu . Sina chama chochote cha Siasa, Ni Mshauri na Mchambuzi wa Siasa zaidi ya Miaka 30 Sasa ni mzee miaka 70 Sasa, Nakuomba Rais wangu Mwachie Tundu Lisu, tusiwape Maadui Wa Taifa Letu Wa ndani na nje. Kufurahi mzozo huu. Mungu akupe Hekima na Busara.
Rais wangu Samia Suluhu , Nakuomba Sana Kwa Mamlaka Uliyo Nayo. Mwachie Mh. Lisu awe Huru. Tunaharibu Nchi yetu kwa Mikono yetu wenyewe. Tunawapa maadui wetu na maadui wako kupata nafasi ya kuliumiza Taifa Letu , Tusikubali ilo litoke.
Mimi ni mpenzi wa Yanga Lakini nimeumia kushindwa kwa Simba ni kushindwa kwa Taifa nzima la Tanzania, Ni sawa kuiombea Nchi yako ikiwa vitani na Nchi nyingine Kupigwa na kushindwa vita.
Kama mchambuzi wa siasa na Mshauri za Siasa za Tanzania muda mrefu sasa, Nadhani G55 kujitoa Chadema Mapema walikosa kusoma Alama za Nyakati, kwanza kukosa sababu za Msingi , pili wengi wanao ondoka ni watu wa mbowe. Nadhani aileti picha nzuri kwa watanzania.
Ningepata Nafasi ya kukutana na Mheshimiwa Rais Samia Suhusu Ningeshukuru Sana Kama mzee wa Miaka 70 nimekuwepo toka utawala wa Mwalimu Nyerere, Kuna jambo la kusaidia Rais Samia Suluhu ni kiongozi Mzuri, Mwalimu Nyerere aliwatumia wazee kumshauri nje ya vyombo vyake.
Naiombe Tanzania iwe Nchi ya Amani , Haki na Utuivu. Tukae Kama Taifa bila kujali tofauti zetu. Tutatue tofauti zetu kwa Haki na Amani. Ndugu wakae Pamoja kwa Umoja. Tujenge Taifa Lenye Maridhiano. Haki na Amani na umoja.
Rais samia suluhu , lazima tuwe wa kweli kama Rais Mwanamke Umefanya kazi kubwa sana kukamilisha Miradi aliyoiacha Mtangulizi wako , Watu wengi hawa kukutegemea kabisa nakupa hongera ingawa mimi sipendi uchawa. Upande wa Upinzani Nakuomba wachie Lisu ana kuharibia mema yako .