Taasisi ya @mamaalaskajamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tz (TWCC), Trade Mark East Africa na Ofisi ya Mbunge ya Karagwe, wamezindua semina ya kutoa elimu ya biashara, kutambua sheria na fursa kufanya biashara mipakani kwa wanawake wajasiriamali Karagwe
"Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau ya tasnia ya habari juu ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mwakabibi, kuweka chini ya ulinzi wanahabari. Tunaomba wanahabari wawe na subira wakati tunafanyia kazi suala hili" @innobash
Hongera Alexius Sylvester kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Karagwe.
Uchaguzi huo mdogo umefanyika Leo, Machi 13, 2021 katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Karagwe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akikabithiwa silaha za jadi na chief wa wangoni Emmanuel Matola Zulu baada ya Kilele cha Maadhimisho ya miaka 114 ya vita vya Maji Maji na Tamasha la Utalii na Utamaduni lililofanyika Songea - Ruvuma, 27.2.2021
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, @innobash (kushoto) akifurahia jambo na Askofu Almachius Rweyongeza wa jimbo Katoliki la Kayangabaada ya kupata Baraka na chai ya pamoja katika makazi ya maaskofu yaliyopo Kasharara – Kayanga – Karagwe. Leo Februari 16, 2021.
"Vijana wetu @TaifaStars_ wametulia na kucheza mpira kwa kujiamini na kila mechi wamezidi kuonesha kwamba Tz tunaweza. WaTz tuendelee kuzipa moyo timu zetu za taifa. Tumejipanga kuzijengea uwezo na tutafika malengo ya kuiweka nchi yetu kwenye raman ya michezo kimataifa"@innobash
Mapendekezo ya kukomesha ajali za moto Karagwe.
“Wafanyabiashara waweke walinzi wenye uhakika maana walinzi wengi ni wazee sana na walevi, kila duka liwe na kifaa cha zima moto ili kusaidia kuzima milipuko kabla haijasambaa Zaidi”
amesema Godfrey Mheruka mkuu wa Wilaya Karagwe
‘‘Mkuu wa Wilaya ninakuamini katika uchapa kazi lakini tunapozungumzia kukomesha ajari za moto tukumbuke na kukomesha ubovu wa gari letu la zimamoto, hatuwezi kujenga fire brigade kama ya ulaya lakini tukawa na gari bovu bovu” amesema Waziri Bashungwa
"Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF lazima liweke kipaumbele kwenye michezo ya watoto wa shule za msingi na sekondari ili kupata wachezaji wazuri wa timu za Taifa.
Serikali imetenga shule 56 kwa ajili ya kufundisha michezo ili kuzalisha wanamichezo wengi nchini"alisema Bashungwa
Bashungwa ameiagiza Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kuongeza kasi katika kutekeleza usimamizi wa kazi za Sanaa.
"Nawaagiza COSOTA kujitangaza kutumia vyombo vya habari na njia nyingine ikiwemo Mitandao ya kijamii ili mnayotekeleza wadau wenu wayajue" alisema Bashungwa.
Serikali itashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF katika kuendeleza mchezo wa Mpira wa Miguu.
"Serikali tuko tayari kushirikiana na TFF, Hivyo lazima shughuli zote za michezo za timu za taifa za ndani na nje ya nchi Serikali iwe na taarifa" Mhe. Bashungwa @innobash
"Naendelea kusisitiza suala la Utawala Bora kwa Vyama na Mashirikisho yote ya Michezo, pia hakikisheni mnasaidia ustawi wa timu zetu za Taifa,"
alisema Waziri Mhe.Bashungwa
wakati wa Kikao cha Maandalizi ya Kushiriki Michezo ya Olimpiki mwaka 2021
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Innocent Bashungwa akiongea wakati wa Kikao cha Maandalizi ya Kushiriki Michezo ya Olimpiki mwaka 2021.
Kikao ambacho kimefanyika Desemba 22, 2020, Jijini Dar es Salaam.