@EduTalkTz Tafuteni namna nyingine ya kuhamasisha matumizi ya kiswahili kwenye maisha ya kawaida kwanza, badala ya kukitumia kama chaka la kufichia madhaifu ya mfumo wa elimu ya Tanzania.
@EduTalkTz Kwa taarifa yako kiswahili hakipendwi hata kwenye biashara. Hebu tembea kutoka ikulu magogoni hadi Pugu usome mabango yote barabarani, ukokotoe ni % ngapi yako kwa kiswahili. Sikiliza muziki wa Bongo fleva usikie wanavyojaziajazia kiingereza. Tafuta namna nyingine ya kuhamasisha
@EduTalkTz Kwahiyo wakisomeshwa kwa kiswahili ndio watafaulu hiyo kiingerrza? Wewe ulisomeshwa kwa kiswahili?
Unakwepa tatizo halisi kwa makusudi unang'ang'ania kiswahili. Nina uhakika unafahamu kuwa tatizo siyo lugha lakini una maslahi yako binafsi unayotetea.
@HKigwangalla@tanpol Mama Samia ametumia hekima sana kufungulia maji yapite kuliko kuyazuia ambayo ingeleta mafuriko na hasara. Na maji haya yatapita kwenye njia yake bila madhara yoyote.
@HKigwangalla Maoni ya Dr Kigwangalla yako kwenye kitabu chake ambako ameyafafanua vizuri sana kuhusu systems strengthening. Yeyote mwenye nia nzuri ya kuyaelewa kama scholar akakisome kile kitabu, kinapatikana kwenye bookshops.
@eli_njex@ayubu_madenge Jimbo la Sumbawanga sasa linaendelezwa na Askofu Beatus Urassa, ambaye si ajabu kule Mashati Rombo alikozaliwa pengine nao wanasema hajawafanyia kitu. Wote hao ni watumishi katika shamba la Bwana hivyo popote walipo ni kwao, sio lazima iwe pale walipozaliwa.
@Jambotv_ Pendekezo la kuongeza idadi ya wabunge ni la hovyo kuliko yote ambayo nimepata kuyasikia katika haya maboresho ya sheria yanayojadiliwa.
Kama kila kata ina diwani mmoja na anatosha, basi kila wilaya inaweza kuwa na mbunge mmoja na akatosha.
@EduTalkTz@ummymwalimu Weka pia matokeo ya zile shule zilizofanya vizuri ili iwe balanced. Au unamaanisha Tanga nzima kote wamefeli?
Mbona hata katika familia moja wapo wanaofeli na wanaofaulu? Au mwenzetu huko kwenu utokako wote wilaya nzima ni division one tupu? Hizi hoja chokonozi hazina nia nzuri
@EduTalkTz@SuluhuSamia Kwahiyo unaamini wakisoma kwa kiswahili katika mazingira hayohayo bila kuboresha miundombinu na rasilimali watafaulu?
Wacha kuleta majibu mepesi yanayokwepa tatizo halisi.
Mbona huleti mifano ya shule za serikali zilizofanya vizuri kwa kutumia lugha hiyohiyo ya kiingereza?