Mkasambaza Picha kwamba huyu ni Ndugu yangu wa Damu. Jamaa anaitwa Hamza na ni Dereva Malori. Tusitumie Kipindi hiki kigumu na kizito cha Majonzi kusambaza Chuki dhidi ya watu wengine. Tunaumiza watu wasio na hatia kwa maandiko yetu tunakuwa hatuna tofauti na wauwaji.
IF you allow anyone to decide what's good for you on your behalf; be sure they will one day decide what's bad for you, if it's good for them.
Ukiruhusu mtu yeyote akuchagulie analodhani ni jema kwako; kaa ukijua kwamba kuna siku atakuchagulia lililo baya, kama kwake ni zuri.
Facts checking
CCM walihubiri kwamba reforms zimefanyika na 4Rs zinafanya kazi vizuri
CHADEMA wakasema ni ulaghai mtupu ( No reforms, No Election)
ACT Wazalendo tukasema wacha tuingie kupambana na tuta Linda kura
Yaliyojili
CCM amethibitisha no reforms zilizofanyika 👇
Nimeona picha—nimesikitishwa sana na matukio ya kumwagika kwa damu, vifo, majeraha na madhara mengine yanayotokana na Uchaguzi
Ni jambo la kusikitisha kuona wananchi wakipoteza maisha kwa sababu ya kutumia haki yao ya kikatiba ya kushiriki maandamano ya amani. hili halikubaliki na hatua zichukuliwe. Tanzania ni yetu sote.
May the heavens be with us through this mission of a free Uganda!
Thank you Butambala, thank you Uganda!
Ssembabule see you soon!
#MissionToFreedom#protestvote2026🇺🇬
Master Tindwa Ngamba Mtopa.
Master Tindwa Ngamba Mtopa hakuwa tu mtangazaji wa Clouds Media Group (CMG) katika kipindi cha michezo cha Sports Xtra. Hapana. Master Tindwa kwetu wengine ni kaka. Master Tindwa ni ndugu na jamaa yetu.
Wadogo zake Master T, kuanzia kwa Mwl, Faraji Ngamba Mtopa hadi kwa Gift Ngamba Mtopa mama yake na mjomba wake Master Tindwa, anaitwa Malcom. Hakika, kifo chake kimetusikitisha na kutuumiza.
Master Tindwa Mtopa Ngamba, mwanachama na mfuasi kindakindaki kabisa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hakuwahi kujihusisha na ukosoaji wa Serikali ya CCM au kuwa mpinzani. Aliamua kupenda na kujadili soka.
Bahati mbaya hata waajiri wake, Clouds Media Group (CMG) hawaelezi ukweli wa kifo chake. Wafanyakazi wenzake wa Clouds Media Group (CMG), hawaelezi ukweli na sababu ya kifo chake. Wamekuwa wanafiki.
Ipo hivi. Siku ya kupiga kura uchaguzi mkuu 29.10.2025 Master Tindwa alikuwa nyumbani kwao, Buza, Temeke. Alikuwa ndani anatazama runinga tu. Huko nje akasikia sauti na kelele nyingi na watu wakipiga mayowe..
Master Tindwa akatoka sebuleni na kwenda barazani kwao hapo, kuchungulia nje kuna jambo gani. Ghafla akasikia risasi ya tumbo, anageuka kurufi ndani risasi nyingine ikarushwa na kumpata kwenye makalio.
Ndugu zake wakajitokeza kumvuta hadi ndani baada ya hiyo gari kupita. Wakati huo risasi zinarindima na kurushwa kama mvua. Hiyo ilikuwa saa 10 alasiri. Wakambeba kujaribu kumkimbiza hospitali…
Barabarani wakazuiwa hairuhusiwi mtu kutembea barabarani isipokuwa vyombo na vikosi vya ulinzi usalama pekee yake. Wakaamua kurudi ndani, damu zikendelea kuvuja kwa wingi sana katika majeraha..
Ndugu zake waliokuwepo wakaamua kumtafuta kwa kumpigia simu kaka yao mkubwa ambaye ni askari wa JWTZ (nitahifadhi kikosi chake) kutoka huko hadi nyumbani Buza, Temeke amefika saa 12:45 jioni.
Kaka yao (jina lake nalihifadhi) mkubwa amefika nyumbani na kumchukua Master T, akampakata kwenye mapaja na kupanda pikipiki. Kwa kuwa amevaa sare za JWTZ, wakafungua vizuizi vyote akawa anapita.
Akiwa njiani wakimpeleka hospitali, alikuwa anasema anasikia pumzi inamuishia. Wakafika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke. Madaktari wakafanikiwa kumtoa risasi kadhaa. Master T akafariki saa 1:30 usiku.
Hivyo, watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV na wana tasnia wenzake na Master T, kama mnataka kumtakia heri huko alipo, ni vizuri kueleza sababu za kifo chake na kukemea kwa sauti kali sana. Hivyo, mtamtendea haki.
Master T, umefanya kazi katika chombo cha habari ambacho hakina habari za kifo chako. Hii ni huzuni sana. Pumzika kwa amani Master Tindwa Ngamba Mtopa. Rest Well Master T. Fare Thee Well Mdengereko. 🕊️
What we have witnessed across our nation is not just tragedy, it is a wound to the soul of Tanzania. Every loss, no matter whose side it was on, is a loss to us all.
In times like this, words carry weight. May ours be the kind that heal, not harm. I mourn with every family that will never be the same again. We must remember that power, politics, and opinions come and go, but lives, once lost, never return.
May we find the wisdom to heal, the courage to listen, and the strength to rebuild what this pain has broken.
#Tanzania #Healing
___________________________________________
Kile tulichoshuhudia kote nchini siyo tu janga, bali ni jeraha katika roho ya Tanzania. Kila maisha yaliyopotea, bila kujali yalikuwa upande gani, ni hasara kwetu sote.
Wakati kama huu, maneno yana uzito. Tuchague kusema yale yanayoponya. Ninaomboleza pamoja na familia zote ambazo hazitakuwa kama zamani tena. Tukumbuke kwamba mamlaka, siasa, na maoni hubadilika, lakini maisha yakipotea, hayarudi tena.
Tupate hekima ya kuponya, ujasiri wa kusikiliza, na nguvu za kujenga upya kile kilichovunjwa na maumivu haya.