Bei ya soda ya coca-cola dukani ni Sh 700, Katika restaurant Sh 2000, airport Sh 5,000 ndani ya ndege Sh 7,000. Soda ileile, ujazo ule ule, utamu ule ule thamani tofauti. Nini nakimaanisha ? Iko hivi Kuna mtu ana digrii moja ya kozi ile, chuo kile kile lakini mmoja anapata mshara laki 3, mwingine laki 7, mwingine milioni 2 mwingine milioni 20.
Thamani ya mtu inatokana na mahali alipo, ukiona unakanyagwa pandisha thamani yako kwa kubadilisha location.Mshumaa hauna thamani mchana kweupe, lakini ni mfalme giza linapoingia. Jua "timing" yako na mahali ambapo "mwanga" wako unahitajika zaidi.
My friend Ukiona sehemu huthaminiwi, usikasirike. Hiyo ni ishara kwamba muda wako wa kuhama umefika. Nenda pale ambapo watu watasema tulichelewa kukujua.Wakati mwingine "location" mpya inahitaji uende peke yako. "Tai haruki na njiwa. Ili upae juu, lazima uachane na kundi linalopenda kubaki chini"
Pambana✍️
🏆👏🏼 Pep Guardiola: “Congratulations Arsenal, Mikel Arteta, his staff, backroom staff, all the players, fans for this Premier League…
…they deserve it!”. ✨
Kuna kazi mtu unafanya.
Zinakupa pesa.
Ila,
Sio kazi ambazo ni guarantee ya maisha ya leo, kesho na vizazi vyako.
Ni PATH ya kukutoa sehemu moja kwenda nyingine.
Mfano.
Udereva wa magari yote.
Ujenzi
Boda
Agent
Dalali
Fundi wa furniture
Fundi wa AC
Uchomeleaji
Freelancing
Mawawinga
Na kazi nyingi au zote zinazokupa pesa ndogo ndogo ya kila siku.
Fikiria madereva ambao hawakujiandaa kupokea uzee wana hali gani.
Fikiria na hao wote katika uzee watakuwa na hali gani wanapo relax.
Boda mzee?
Agent wa magari mzee?
Badala yake.
Ile ni fursa ya kuandaa maisha bora ya baadae nje ya hiyo kazi.
Kwake na vizazi vyake.
Changamoto ni kwamba.
Katika umri wa ujana ambapo hizo fursa zinawapa pesa.
Watu tuna relax na kutumia pesa katika mambo ya ajabu kama.
Pombe.
Kubadili wanawake.
Kusomesha na
Kuzaa zaa among others.
Ndiomana baadae tunapata hawa wazee bodaboda.
Wazee content creator.
Wazee wa vijiweni wanaosumbua watoto wao wanaopambania familia zao.
Baadae inakuwa lawama kwa ndugu wenye kipato mpaka kugombania mirathi na mambo kama hayo.
Lengo la hii tweet ni.
Ijue kazi yako na uifikirie in 30 years to come itaendelea kukupa pesa? Kama hamna basi usi relax bro.
Normalize kutolidhika hatakama sisi wote tutakufa. Angalia watoto wako wataishije baada ya wewe kutokuwepo.
Angalia katika miaka yako 50 utakuwa umeshika nini cha kukupa pesa bila wewe kushughulika kwa nguvu.
Fanya kazi yako kama path ya kukupa kikubwa zaidi.
Save pesa kwa malengo ya kufanya kitu kikubwa zaidi.
Duka la simu linaweza kufa.
U winga unaisha.
Udalali unaisha.
U content creator unaisha
Kuwa boda au bajaji kuna mwisho.
Kuwa dereva kuna mwisho.
Sasa baada ya hapo utakuwaje? Hizo kazi zitaisha ukiwa umejenga mazingira salama bila wewe kushugulika?
Utakuwa na hardware kubwa watoto wako waendeleze?
Utakuwa na nyumba nyingi?
Utaendelea kuwa content creator?
Utakuwa na lodge nyingi?
Utakuwa ume diversify assets zako?
Pambana sasa bila kuchoka huku ukijiweka bora kwaajili ya kesho.
KULA UJANA VIBAYA UPATE TABU KUMEZA UZEE.