Zingatia haya Juu ya Mafuta Ya Mbegu za Mimea
1. Ni chanzo cha Omega 6.
Watu wanaodhaniwa wamezidiwa Omega 6 wanatakiwa kupunguza Matumizi.
2. Ni Dhaifu kwenye Moto. Sio Salama Kuyakaangia na ukarudia Kuyapikia. Unalisha mwili Free Radicals ambazo HUUMIZA na Kuchakaza mwili.
Kitambi hakiwezi kuonekana ni Ugonjwa mpaka pale Daktari atakapo kuambia ni Chanzo cha Maumivu yote unayo Pitia. Na suluhisho ni “Kupunguza uzito”.
Kukificha na Mkoba, Nguo pana, na Mkanda Hakuwezi kusaidia hapo baadaye Kuondoa maumivu ya mwili.
Daaa! Hakuna Unene wa Asili bali ni wakutengenezwa.
Jamaa ana kilo kama 130 hivi. Kaagiza Mtoli wa ndizi Bakuli kubwa, Chapati 4 na Soda 1.
.
Huyu anakosa Elimu ya;
-Sayansi ya Makundi ya Vyakula
-Sayansi ya Kitambi
-Sayansi ya Mwili wake Unavyo dhurika na vyakula.
TUTAVUKA TU
Adui Mkubwa wa Miili yetu ambaye tunatakiwa Kushughulika naye ni Sukari.
-Watu wengi wanaugua Magonjwa kwa matumizi mabaya ya Sukari na sio Chumvi.
-Sukari alikua adui kabla ya mwongozo wa lishe 1977 na Baadaye maadui wakawa Mafuta/cholesterol na Chumvi.
.
Adui mkubwa ni SUKARI
Huwezi kula Chumvi zaidi ya Kipimo ikitokea mwili huhangaika hapohapo Kuipunguza chumvi.
Sukari ina bei kubwa kuliko chumvi Lakini ndiyo inayopendwa sana na watu kwa sababu Sukari ni Kiburudisho.
Kinacho nishangaza Adui Mkubwa Sukari HATAMKWI Tuhuma zina Elekezwa kwenye CHUMVI.
Kiwango salama za Chumvi kwenye damu ni gramu 3 katika Lita ya damu na kama una Lita 5 za damu mtu mzima Chumvi itakuwa gramu 15. Sukari ni 100mg/dl sawa na gramu 5 kwenye Lita 5 za damu. Chumvi huwa nyingi kwenye damu kuliko Sukari.
-Chumvi ina bei ndogo kuliko Sukari
-Sukari huleta utegemezi chumvi hapana
-Chumvi ni nyingi kwenye damu kuliko sukari
-Kila lita ya damu ina chumvi gramu 3 kwa lita tano ni gramu 15 wakati sukari ni Gramu 5 katika lita 5
-Teja wa Sukari akiugua Husingizia “Ameuguzwa na Chumvi”
Ukiona Huduma au Biashara yako
-Mteja anajisikia Fahari kuwa na Bidhaa yako.
-Mteja anajivunia kuwa na bidhaa
-Bidhaa au Huduma yako inagusa na Kuamsha Hisia za Mtu
Mfano Kwako Unajisikiaje Kumiliki German Car? Apple device?
Wateja hununua BRAND na sio BIDHAA
Daaa! Jamaa mmoja hapa Hotel ameshangaza watu. Kagoma kunywa supu kwa sababu ni nyeupe tu haina “Mafuta juu”. Akamuagiza Mhudumu achukue Mafuta ya Juu aje aongeze Ubora Supu yake.
Mwisho Kasema “Sisi wamasai Bila Mafuta Juu ya Supu hayo ni Maji sio Supu ya Kitoweo” 😀
Gari siku hizi inasababisha kitambi? Unaacha gari unatembea kwa Mguu ili uondoe Kitambi?
.
Watu hawana gari wana Kitambi. Ni hivi Kitambi ni matokeo ya Muundo wa sahani yako Unaweka 95% chakula cha Burudani na asilimia 5 Vyakula vyenye Virutubisho.Badili Sahani kabla ya Mazoezi.
Kwa nini watu wa kale Hawakuwa na Kitambi?
-Nafaka haikuwa lishe Kuu kwao sababu ya nyenzo duni za Kuchakata.
-Waliishi kwa Uwindaji na Ufugaji
-Walikula matunda sio Juisi wala soda
-Hawakuwa na Mafuta ya Mbegu
-Mlo Ulikuwa 1-2 tu/Siku
-Hawakukaanga Chakula
-Kazi zao ni Mazoezi
Hebu Fikiri na Wewe
ASUBUHI
-Mtori wa Ndizi,Chapati na Soda
MCHANA
-Ugali dagaa,Maharage, Energy
USIKU
-Chips Kuku, Soda
Unakula hivyo Miaka 5-10 unafikiri utaachaje kuja kuwa Goigoi Kitandani? Badilisha SAHANI urudishe UANAUME WAKO. Utakuja Nishukuru Shortcut ZITAKUFIRISI.
Mazoezi ya tumbo ukiwa na Kitambi unapoteza muda.
-Mafuta ya nyama uzembe hutunzwa Juu ya Misuli.
-Mazoezi yatumbo huwa ni kukaza misuli ya tumbo.
-Mafuta Yaliyo Juu ya Misuli huzuia Kufikia misuli.
“Anza na Lishe bora toa kwanza mafuta juu ya misuli halafu kaza misuli mazoezi”
Kuhusu Kitambi na Lishe
-Kitambi tiba sio mazoezi magumu
-Kitambi ni tatizo la Homoni sio Ulafi wala Uvivu
-Ulafi na Uvivu sio vyanzo vya Kitambi ni dalili za Kitambi Kilicho kithiri
-Kuna Uhusiano Mkubwa kati ya Homoni,Chakula na Kitambi. Kutokujua ni sababu ya Kumiliki Kitambi.
Nimeangalia Video Ya Bibi Harusi wengi wanafanana Kifuani. Wanafunga nini tumboni mbona kama wanahemea Juu Juu.
Mkanda bana tumbo? Kwani harusi ni jambo la dharura? Kwani kwa miezi 4 Unaweza Kukata nyama uzembe kilo takribani 20.
Sogezeni Ndoa Mbele Watakuja Kutapika ukumbini.