#Cotton provides employment to 500 000 rural households and is the source for both direct and indirect benefits to more than 40% of the #Tanzanian livelihood.
E A R L Y H A R V E S T in Central #Tanzania. Early harvesting of seed #cotton contribute to a substantial improvement in cotton lint's color grade and possibly other quality parameters, such as a reduction of leaf content in the fiber.
Cotton farming communities in Tanzania benefiting from Build a Better Tomorrow #BBT initiative which among many benefits they are assured of delivery of effective and timely #extensionservices. #WHITEGOLD#cotton#AGENDA1030
Bei ya kilo moja ya pamba mbegu kwa msimu wa 2024-25 imetangazwa na serikali kuwa ni shilingi 1,150/= kwa pamba Daraja A na shilingi 575/= kwa pamba Daraja B ikiwa ni ongezeko la asilimia nane (8%) kutoka bei ya shilingi 1,060/= ya msimu uliotangulia wa 2023-2024.#dhahabunyeupe
Tukio hilo limefanyika wakati wa shererehe za uzinduzi wa msimu wa ununuzi wa pamba kitaifa zilizofanyika wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya pamba wakiwemo wakulima na wanunuzi kutoka mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani.
FURUSHI LA KWANZA MSIMU WA 2024-2025
Mzigo wa kwanza wa furushi la pamba kwa msimu wa 2024-2025 ya Mkulima Bw. Abel Masanja wa Kijiji cha Ndoleleji ukipimwa kwenye mzani katika AMCOS ya Butalijalala kuashiria kuanza rasmi kwa msimu wa ununuzi wa pamba wa 2024-2025.
Watumishi wa Bodi ya Pamba Tanzania ofisi ya Makao Makuu wakipatiwa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo wa Ofisi-Kielektroniki kutoka wa wakufunzi toka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma yenye lengo la kupunguza gharama za uendeshaji na kurahisisha mawasiliano
WADAU WA TASNIA WANENA
Mchango wa Mhe. Dkt Hamis Kigwagangalla
@HKigwangalla kwa sekta ya pamba kuweza kulitumia vema soko la nje wakati wa Mkutano wa 17 wa wadau wa sekta-ndogo ya pamba uliofanyika hivi karibuni jijini Dodoma #mkutano17wadauwapamba
MAMBO MANNE (4) KUONGEZA TIJA
Mhe. Stanslaus Nyongo akielezea namna tija katika zao la pamba inavyoweza kuongezwa kwa kuzingatia mambo makuu 4 wakati wa mkutano wa 17 wa wadau wa pamba.Maswa ni miongoni mwa wilaya vinara wazalishaji pamba hapa nchini
#mkutano17wadauwapamba
Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wote wa Bodi ya Pamba Tanzania tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake tangu aingie madarakani. Tunamtakia kheri katika Utumishi wake na#kaziiendelee
KNOWLEDGE SHARING FROM BEGINNING.....
Cotton lead farmer (left) exchange critical information on good agricultural practices in growing cotton with fellow cotton growers in Geita region in northwestern Tanzania.
#cotton#farming#KnowledgeIsPower
DESEMBA TUKIMALIZIA KUPANDA
PICHANI: Mkulima wa kijiji cha Gusui wilaya ya Serengeti,mkoani Mara akivuta kamba wakati akiendelea na upandaji wa zao la pamba katika shamba lake msimu wa kilimo 2023-24
#pamba#dhahabunyeupe#kilimo#tija#ajenda1030
Pamba!!! Dhahabu Nyeupe…
Ni wito wetu kwa wadau kupata taarifa sahihi toka kwa vyanzo vya kuaminika na ukashiriki katika kufikisha taarifa sahihi kwa Watanzania kwa nia njema ya kuwaletea maendeleo
SEKTA YA PAMBA NINI KINACHOCHEA MABADILIKO YA BEI
Pamba nchini inalimwa katika mikoa 17 na wilaya 56na wakulima wadogo wadogo kati ya 350,000 hadi 600,000, wenye mashamba ya ukubwa wa wastani wa ekari 2.5 hadi 5
Burundi bei ni shilingi sawa na shilingi za kitanzania 700 kwa kilo, Zambia ni shilingi za kitanzania 780-800 kwa kilo, Zimbabwe ni shilingi za Kitanzania 900-1000 kwa kilo.