Mabibi na Mabaunsa, Wadai kwa Wadaiwa, Wenye nyumba na wenye vyumba, habari zilizonifikia kwenye chumba cha habari jioni hii ni kwamba Kamati ya Maandalizi ya Matamasha ya Miaka 30 ya Bongofleva imefikia makubaliano rasmi na Rapper wa Marekani Mr. Cheeks kuja kutumbuiza katika tamasha la Arusha tarehe 19 September.
Na kwa tangazo hilo basi Mashabiki wa Mr. Cheeks wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania ikiwemo Kenya, Rwanda, Zambia, Uganda, South Africa na kwengineko tutakutana katika Viwanja vya General Tyre, Arusha Tanzania tarehe 19 September. #MillardAyoUPDATES