Wanaanga wa Artemis II wameweka rekodi mpya wakisafiri zaidi ya maili 200,000 kutoka Dunia—mbali kuliko safari yoyote ya mwanadamu tangu Apollo 13.
🎙️ Brenda Karegi
#Artemis2#Moon#Sayansi#NASA#BrainsetSwahili
Serikali ya Iran imetangaza dau nono la takriban dola elfu sitini kwa raia yeyote atakayefanikiwa kumkamata hai rubani wa jeshi la Marekani.
🎙️Arinota Ainsworth
#marekani#israeliranwar#israelwar
Iran na Israel zilikuwa washirika wa kimkakati hadi Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979, ambapo Ayatollah Khomeini aliigeukia Israel na kuiita “Shetani Mdogo.”
🎙️ Ibrahim Jodia
#IranVsIsrael#Mossad#Iran#Israel#BrainsetSwahili
Ndege Common Swift (Teleka/Mbayumbayu) hutumia karibu maisha yake yote angani na anaweza kusafiri zaidi ya km 22,000 wakati wa uhamiaji.
🎙️ Allan Wetungu na Mariam Swalehe
#Wanyama#Ndege#Mbayumbayu#BrainsetSwahili#AWetungu
Serikali ya Tanzania imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kuanzia Aprili 1, 2026, kufuatia ongezeko la bei kimataifa kutokana na mzozo wa Mashariki ya Kati.
Zaidi na mwandishi wa Brainset Swahili, Arinota Ainsworth
#Tanzania#Mafuta#Iran#IranVsTrump#BeiyaMafuta
Iran imeingia siku ya 32 ya kukatika kwa mtandao. Kulingana na mtandao wa NetBlocks watumiaji wengi wamekosa mawasiliano ya nje kwa zaidi ya saa 744
Wengine wamejaribu kutumia huduma za satelaiti kama Starlink, ingawa ni ghali
🎙️Arinota Ainsworth
#IranVsIsrael#InternetInIran
Ulimi wa kigong'ota, au kigogota hulinda ubongo wake dhidi ya athari mbaya ya kugongagonga bila kukoma. Ulimi wa kigogota ni mrefu sana kiasi kwamba huzunguka fuvu lote
🎙️ Allan Wetungu na Brenda Karegi
#Wanyama#Ndege#Kigogota#BrainsetSwahili#Awetungu
Serikali ya Uingereza inasema inalinda maisha ya raia wake, maslahi ya taifa na washirika wake. Hata hivyo, Waziri Mkuu Keir Starmer amesisitiza kuwa Uingereza itaendelea kushirikiana kimataifa kulinda usafirishaji, hasa katika Mlango Bahari wa Hormuz.
#IranIsraeUsWar#Trump
Mchwa aina ya Carpenter hufanyiana “upasuaji” kwa kukata mguu ulioumia wa mwenzao ili kuzuia maambukizi na kuokoa maisha.
🎙️ Swinny Jangara na Brenda Karegi
#Wanyama#Wadudu#Mchwa#Swahili#BrainsetSwahili
FIIDIA AU VITA? Sharti Jipya La Iran Linaloiumiza Kichwa Marekani.
Marekani na Israel zadai kuidhoofisha Iran kijeshi kwa mashambulizi ya kihistoria, huku Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth akisisitiza kuwa "mabomu ndiyo njia ya mazungumzo."
#GlobalConflict#PeteHegseth#DonaldTrump
Rais wa Bassirou Diomaye Faye amebadilisha picha yake ya wasifu na kuweka kombe la AFCON ambalo Senegal ilishinda. Hii inajiri wakati serikali ikitaka uchunguzi dhidi ya CAF kufuatia madai ya kuvuliwa taji kwa upendeleo wa Morocco.
🎙️ Arinota Ainsworth
#Senegal#AFCON#Morocco
Iran imetangaza kuendelea kulenga miundombinu ya nishati ya Marekani, ikiwa Marekani itashambulia sekta yake ya nishati. Rais Trump amesema Iran ina chini ya masaa 48 kufungua njia ya bahari ya Mlango wa Hormuz, la sivyo, watapokea kipigo kikubwa.
-
#IranIsraelWar#IranVsTrump
Watu zaidi ya 4,560 wamejeruhiwa na kulazwa katika mashambulizi ya Iram dhidi ya Israel, imesema wizara ya afya ya Israel.
Majeruhi 124 bado wanapata matibabu, na mmoja ni hali mahututi.
Allan Wetungu 🎙
#Iran#IranIsraelWar#IranVsTrump#IsraelUsIranWar#BrainsetSwahili