Baada ya video zangu za jana, nimeambiwa tatizo sio kwamba wanaharakati wanaona uvivu kuondoa comments za ku demoralize wananchi na mwishowe kuharabu harakati, nimeambiwa tatizo ni kwamba wanaharakati wengi wanataka engagement na followers.
Dah, basi tatizo ni kubwa kuliko nilivyodhani. Nilidhani labda ni uvivu tu ila ndo nimeleeweshwa kuwa wengi ni hawajali kama harakati zao zinaleta manufaa yoyote, wao wanataka engagement na followers regardless hata kama harakati zinaharibika na zinakuwa hazina mashiko kutokana na comments wanazoacha kwenye post zao.
Basi kazi ipo!!!!!
Wanaharakati, haswa mnaoposti Instagram na Tiktok tunawaomba mzingatie comments kwenye posti zenu.
Posti zenu zinakosa ushawishi sababu mnaruhusu comments za maboti wa wauwaji.
Wao wauwaji especially muuaji mkuu ana control comments kwa page yake sababu anaelewa uzito wa comments. Haya yule msemaji ana control comments, hata page ya CCM wana control comments.
Mnaharibu harakati zenu wenyewe kwa kuruhusu comments za kuvunja watu moyo. Mtu akiona posti cha kwanza ni kufungua comments ili kujua mawazo ya wengine. Ni kazi yako mwanaharakati kuhakikisha comments zoote kwenye posti zako zinatoa moyo wa maandamano.
Wananchi kutoka kuandamana is a psychological issue, msiruhusi comments zinachozesha na psychology ya binadamu.
Kama huwezi ku control comments ni bora hata usiposti harakati maana haina maana unapoteza muda. You have to control the comments.
Baada ya video ya kwanza kuhusu kenge waliovamia msafara wa Mamba mwaka jana,nimepata message nyingi whatsapp Watanzania wakijilaumu sana.
Msijilaumu, we made a mistake. Cha muhimu tusirudie tena kosa la kuamini kenge….
Tusiwaongelee tena. Hata mimi siwaongelei tena maana najua wanatamani hata niwataje kwa majina ili wa trend. Tusiwape umuhimu. Tuendeleee kudai
Hi guys, I need a huge favor. Naomba msaada wenu mkubwa.
Hili tangazo ni la maana sana, siwezi kuelezea kwa kina sasa hivi ila baadae nitawaelezea. Ila ni process ya kupata account zangu za meta (instagram na Facebook)
Naomba mnitumie posti yoyote ile ya Mmarekani yoyote yule, mweusi au Mzungu ambae kawahi kuandika posti yoyote ile akiikosoa serikali ya Tanzania na posti hiyo haikufutwa au kuchukuliwa hatua na meta, posti lazma iwe kwenye mitandao ya instagram au facebook sio humu X.
Sio lazma awe Mmarekani au mzungu, hata awe mweusi ila sio Mtanzania ila awe anaishi hapa Marekani au hata nje ya Marekani.
Yani kwa kifupi posti za foreigners haswa wazungu wakiikosoa serikali ya Tanzania.
Naomba mnitumie kupitia whatsapp +1 424-537-3057
Nina swali, wale wapuuzi waliokuwa wanapush maridhiano kati ya Watanzania na wauwaji wa CCM wana la kusema kwa sasa????
Wanaharakati tulipokuwa tunayakataa maridhiano tulijua wauwaji hawako tayari kwa maridhiano ya kweli, wanachotaka kwenye maridhiano ni legitimacy na uwezo wa kuwazodoa international community kwa kuwaambia, msituingilie sisi tumeshafanya Maridhiano na tume heal.
Things are getting worse in Tanzania.
@Europarl_EN@SenTedCruz@SenatorShaheen@SenateForeign@SecRubio
The government has now banned political rallies after the main opposition party drew massive crowds across the country.
When a government responds to overwhelming public support for the opposition by banning political rallies instead of respecting the democratic process, it should alarm everyone.
Alafu wanawanyooshea vidole wananchi kuwa wanataka kuharibu amani na wao watalinda amani…..
Waharibifu wa amani wanadai wao ndio wanalinda amani…..
. @jmkikwete@SuluhuSamia Mnawanyima Watanzania haki ya kuunga mkono chama chao wanachokiamini kwa kuzuia mikutano ya hadhara.
Mnataka wananchi wapambane kwa njia zipi kama njia zote halali zinazuiliwa?
Ni mpaka mzalishe rebel groups Tanzania ndio mtaona raha?
JAKAYA KIKWETE NI KANSA KWENYE TAIFA LA TANZANIA. HUYU NDIO CATALYST WA MAUAJI YANAONDELEA TANZANIA NA VITENDO VYOTE VYA UMINYAJI HAKI.
Mwaka jana kipindi cha uchaguzi, kuna speech mbili aliongea Kikwete ambazo zilituumiza mioyo Watanzania wengi na pia speech hizi zilituonyesha Watanzania ni nani anaemdanganya Samia Suluhu kuendelea na unyanyasaji wa Watanzania, utekaji na uuaji wa Watanzania.
Video ya kwanza, Kikwete alisema kuwa sheria za uchaguzi Tz sio mbaya, ziko sawa tu na kwamba ni kundi dogo la watu ndio linadanganya wananchi.
Imagine nchi nzima inavyolia na sheria za uchaguzi ila Kikwete anakwambia hizi ndo sheria zinafaa Tanzania.
Video ya pili Kikwete anasema kuwa bunge zima la Tanzania linatakiwa kuwa CCM tupu maana hawataki kuchanganya pumba na mchele, kwamba wao na familia zao ni mchele sisi wananchi tunaolilia haki ni pumba.
Downfall nzima ya demokrasia Tanzania ameileta Kikwete na mpaka sasa yeye ndio anazidi ku drive machafuko ndani ya nchi kwa kuhakikisha Watanzania hawapati haki.
Yes, Samia ana deserve lawama zote ila inabidi Watanzania waelewe Samia anapewa nguvu na Kikwete. Hata Samia tufanikiwe kumuondoa ila as long Kikwete bado yuko involved the siasa za Tanzania basi Watanzania tutaendelea kuuliwa nafasi CCM.
Na kinachoumiza zaidi @_AfricanUnion imempa Kikwete position ya kudeal na siasa tata nchi za Afric. Imagine master mind wa siasa tata Tanzanka ndio anapewa cheo za kusawazisha siasa tata Tanzania.
Huyu Mzeehatakiwi kupewa nafasi in any room ya uongozi popote pale. Ana damu za Watanzania kwenye mikono yake.
Siku nzima ya leo magari mawili ya polisi na polisi wakiwa wameziba nyuso zao na silaha kubwa kubwa, wamenifuatilia tangu nikiwa Urambo kwa kupokezana mpaka nafika Kigoma.. njiani nimesimama mara mbili kuwauliza shida yao ni nini kwangu hawakuwa na majibu ya maana.
Nimefika hapa Kigoma kila ninakopita na hapa Hotelin kwangu wamejaa maafisa wakiwa na nguo za Kiraia..
Mimi ni Mwanasiasa wa upinzani ninaetimiza wajibu wangu wa kikatiba… Chama chetu ni chama cha siasa ambacho kimesajiliwa na chenye haki zote katika Nchi hii.
Nimepokea taarifa nyingi kwa watu wema wakitaka niwe makini, wengine wanasema mimi na familia yangu tumetolewa maelekezo mabaya.
Nitatimiza wajibu wangu bila uoga wala hofu, hakuna mtu anaweza kuniondoa kwenye haki na wajibu wa kutetea Nchi yangu na watu wetu.
Ninawashauri watawala dhalimu kuacha kucheza na utulivu huu uliopo . Hofu haijawahi kuzaa amani, hofu huzaa hofu zaidi.
Hakuna siku nitakimbia Nchi yangu.
Serious question, hivi kweli CCM wanaangalia hii hali na bado wanadhani kuna possibility ya wao kuendelea kushikilia nchi bila ridhaa ya Watanzania??
Kweli Kikwete anaangalia hii hali na anaendelea kumdanganga kimama kuwa waendelee tu kung’ang’ania nchi kinguvu??
Mtanzania mwenye akili timamu akiona hii anajua kuwa kama haki isipopatikana haraka basi October 29 ITAJIRUDIA, ITS ONLY A MATTER OF WHEN, NOT IF!!!!!!!!!
Hatuko hapa kukatishana tamaa ila tunaambiana ukweli.
Nilichoona juzi na jana baada ya posti yangu ni kwamba kuna watu wengu walidhani sisi wanaharakati tuna belong kwa chama flani, hapana, most of us hatupo na chama chochote, sisi tuko na wananchi.
So, kama jinsi tunavyowakalia kooni CCM bila uwoga wowote na Chadema pia tukiwa na wasiwasi nao tunaongea vile vile…..
Don’t get it twisted, we are not loyal to any party, we are only loyal to the people.
Na tunaongea coz we want the best for opposition sababu a strong opposition is good for the public, hatutaki tufike December tuwaulize wameachieve nini mwaka mzima, alafu jibu liwe ni picha za nyomi. We want concrete results!!!!!!
Kama mnamaanisha haya anzeni kwanza kwa kuonyesha good faith kwa wananchi kwa kuanza kutoa haki kabla ya maridhiano kuanza kwa:
1. kutoa katiba mpya
2. Kumwachia Tundu Lissu
3. Kuvunja bunge na kulirudisha kwenye uchaguzi ili angalau wananchi wapate bunge la wananchi kabla ya 2030 na sio hiki kikao cha chama kinachojiita bunge la Tanzania ili roho za wananchi ziwe na hope kuwa 2030 uchaguzi utakuwa wa haki na kwamba Maridhiano yana dhamira ya kweli ha kuleta haki…
Mbali na hapo hizi porojo zenu na sinema za good cop na bad cop hamtupatiiiii, tuna akili zaidi yenu…… Sasa hivi mtaongea yote ili tu kuwahadaaa Chadema waingie maridhiano kwa niaba ya Wananchi, maridhiano ambayo yatawapa wauwaji legitimacy internationally na yatawapa control of the situation internationally. Huu mtego Watanzania hawatoingia.
Kabla hatuja wapa maridhiano tuonyesheni kuwa kweli mnamaanisha kuleta haki kwenye nchi.