Mwenyekit Tundu Lissu amehukumiwa kifungo cha miaka minne kwa kosa la uchochezi ambalo, kwa mtazamo wangu, ni la kutengenezwa. Safari sasa ni kwenda Mahakama ya Rufaa, lakini tusisahau kwamba hata Mahakama ya Rufaa haiwezi kuwa mbadala wa dhamiri ya umma katika kutetea haki na kupinga matumizi mabaya ya mifumo ya dola.
Mahakama ya rufaa ya Lissu haipaswi kuwa Mahakama ya Rufaa pekee. Inapaswa kuwa umma wote tunaohofia kwamba kesi hizi zinatumika kama njia ya kuwanyamazisha na kuwadhibiti wanasiasa wakosoaji.
Hatari kubwa zaidi si kifungo cha Lissu pekee. Ni uwezekano wa kifungo kutengeneza mazoea hatimaye kuwa sehemu ya mfumo wa kawaida wa kudhibiti upinzani. Hapo ndipo tunapopaswa kuwa na wasiwasi.
Leo hukumu imetolewa, lakini nchi inaendelea na shughuli zake kana kwamba hakuna jambo kubwa lililotokea. Kana kwamba ni mtu mwingine wa kawaida tu aliyefungwa. Hii ni ishara inayopaswa kutufanya tutafakari kwa kina kuhusu hali ya dhamiri ya jamii yetu.
Watu wengi, wakiwemo wanachama wetu, tayari wako mahabusu. Tusipojiuliza kwa pamoja tunakoelekea, tunaweza kuamka siku moja na kukuta magereza yamekuwa sehemu ya kawaida ya maisha ya kisiasa ya nchi yetu.
Uonevu hauzuiliwi na nguvu ya waliouonewa pekee, bali pia na dhamiri ya jamii inayokataa kuuzoea.
Kukaa kimya mbele ya jambo linalogusa haki za msingi za binadamu kunaweza kuifanya jamii izoeane na hali ambayo kesho inaweza kumkuta yeyote kati yetu.
Hakikisha unamuoa/unaolewa kabla hajajua madhaifu yako yote.
Binadamu tunaweza kuvumilia madhaifu yetu tu.
Kwa nini unaachwa, kwa sababu amefahamu madhaifu yako yote. Umejianika kila kitu kwake.
Ila pia kumbuka, akikutongoza tu basi ni sawa kawasha maigizo ndani yako.
Kuwa mjinga ni gharama, ila gharama inayoingiwa huijui kwa hiyo hakuna maumivu ya Moja kwa Moja..
Mtu mjinga anaahueni, kwa sababu kila kitu anaamini kipo kwa sababu alizopata kichwani, haijalishi ni sababu zisizo na mashiko kwa mtu mwingine kwake zina mashiko...
Muangalie kiongozi mwenye hasira, maamuzi anayofanya.
Waangalie Wana ndoa/familia waliokasirika, utagundua changamoto katika maamuzi Yao...
Akili hurejea pale hasira ikipoa.
@godbless_lema Watanzania ni ngumu sana kuelewa kuwa Kuna wakati unampaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa...
Ndugu zangu, Kuna wakati kinachoandikwa sio maana halisi, napataga shida sana binafsi nikiandika fumbo lenye kufikirisha,
Wengi huanza kutafsiri kwa Yale maneno, Hadi utakapo chambua ten
M/kiti Lissu anakupa pole sana kwa kufiwa na mume wako kipenzi. Tukiwa mahakamani takribani mara mbili, amesisitiza salamu zake zikufikie pamoja na pole zake kwako, watoto na ndugu zako wote.
Lissu ni mtu mwenye upendo mkubwa kwa watu na anayesimamia haki. Ninaamini kama angekuwa nje ya gereza, angefika Unguja mwenyewe kutoa pole na faraja. Kwa bahati mbaya, akiwa bado yuko gerezani, hawezi kutoka na kufika mwenyewe kukupa pole katika kipindi hiki kigumu.
Nami nikupe pole sana kwa kumpoteza mume wako mpendwa. Jipe moyo na uimarishe imani yako katika tumaini la Mungu. Mungu awape nguvu, faraja na uvumilivu wewe, watoto na familia nzima.
Let’s Love Lead, Mama! Get Lissu out of the prison walls!
We are still filling our pen with ink so as to write our history..
Tulipoandika karamu zetu hazikuwa na wino mwing japo bahati mbaya, kuna sehemu tumeandikia historia yetu kwa Penseli
@MariaSTsehai Namuona kwa miaka miwili atajifunza na yeye atabadilika kabisa. Tatizo sio alikotoka na alivyo,
Uongozi wa Awamu hii hubadilisha kila mtu no matter what tutegemee anarudi kule kule kwa kina Mipango na Sera....
Ukweli huwa haupotei ndani ya mtu. Haki huinua Taifa.
@Jaxon__tz Makonda sio mtu mwepesi, alihamishwa kutoka Katibu mwenezi kwenda mkuu wa mkoa, maana alikuwa ni mkubwa kuliko Waliojuu yake...
Alikua anapanda juu zaid katika maamuzi yake
Angellah Kairuki
Ashatu Kijaji
Dorothy Gwajima
Hamad Yusuf Masauni
Deogratius Ndejembi
Joel Nanauka
Juma Homera
Kuna mmoja atatoa hapo..
Makamu wa Rais au aliyeachwa kwenye nyazifa za uongozi, mawaziri wa Awamu zilizopita
Dkt. Mwigulu Nchemba
Prof. Palamagamba Kabudi
Dkt. Dotto Biteko
George Simbachawene
Paul Christian Makonda
Ridhiwani Kikwete
Prof. Kitila Mkumbo
Mahmoud Thabit Kombo
Patrobas Katambi
Anthony Mavunde
Adolf Mkenda
Khamis Mussa Omar
Mohamed Mchengerwa
Hapo