Build Future Initiative is dedicated to address challenges of our community spanning from; Healthcare, Governance, Human Rights, Entrepreneurship & Innovation.
Tumejivunia kushiriki kikamilifu katika Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania jijini Dodoma – tukijadili ajira, elimu & ushiriki wa vijana katika ujenzi wa taifa.
Tunaamini katika ushirikiano na wadau ili kuijenga kesho bora kwa vijana wa Tanzania! 💪🇹🇿
#TYDF2025
BFI imeshiriki kugawa taulo za kike kwa mabinti mkoani Pwani kama sehemu ya juhudi za kuondoa vikwazo vya kielimu vinavyotokana na hedhi.
Tunaamini kila msichana anastahili mazingira salama, heshima, na usaidizi kipindi cha hedhi.
#MenstrualHealthDay#BFI#AfyaYaMsichana
Leo vijana kutoka Build Future Initiative (BFI) wameungana na East Africa Radio kupitia kipindi cha Drive Show kwa mazungumzo maalum kuelekea maadhimisho ya Siku ya Hedhi Duniani. Kupitia programu ya Binti Salama, wamezungumzia umuhimu wa elimu ya hedhi salama.
TZS 2,000 tu inaweza kumpa msichana staha kwa mwezi mzima.
Hii siyo haki, na wewe unaweza kuwa sehemu ya suluhisho.
Changia leo. Toa pedi, badilisha maisha.
Michango yote inapatikana kupitia:
Bank: Equity Bank
Jina: Build Future Initiative
Akaunti Na.: 3007211912604
Asilimia 30 ya wasichana wa shule nchini Tanzania hukosa masomo kila mwezi kutokana na changamoto zinazohusiana na hedhi. Maumivu, ukosefu wa vifaa vya usafi, na hofu ya kudhalilishwa vinawazuia kutimiza ndoto zao.
*BFI Yashiriki Kuwafunda Vijana Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025*
Katika kuunga mkono juhudi za kuimarisha ushiriki wa vijana katika mchakato wa kidemokrasia, Build Future Initiative (BFI) kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji, @PhilipMulashan, imeshiriki kikamilifu katika kutoa elimu hiy
Imani potofu zinaua ndoto za wasichana!
Ni uongo kwamba huwezi kwenda shule ukiwa kwenye hedhi.
Ukweli ni huu: Ukiwa na pedi na elimu sahihi, kila msichana anaweza kufanikwa!
Tuvunje miiko na tuhamasishane kwa pamoja!
UKWELI: Hedhi si uchafu ni mchakato wa kawaida wa kibaiolojia unaoashiria afya ya uzazi kwa wasichana na wanawake.
Hapa Tanzania, bado kuna unyanyapaa na ukosefu wa uelewa kuhusu hedhi. Tafiti zinaonesha kuwa:
- Takribani 25% ya wasichana hukosa masomo kila mwezi
BINTI SALAMA PROGRAM
Leo BFI yazindua rasmi mpango wa kila mwaka wa kutoa elimu ya hedhi salama na taulo za kike kwa wasichana wenye uhitaji.
Kauli mbiu: "Hedhi salama inaanza na mimi"
Kwa heshima, usalama na hadhi ya binti!
Uongozi wa BFI leo tumepata fursa ya kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mama Ongea na Mwanao, ambapo tulijadiliana kwa kina juu ya ushirikiano wa kimkakati kati ya taasisi zetu kwa lengo la kuinua ustawi wa vijana na jamii ya Kitanzania.
#BFI#MamaOngeanaMwanao#KijanaChangamka
🎙️ FURSA YA KIPEKEE!
Je, wewe ni kijana mwenye sauti ya kipekee, uelewa wa masuala ya vijana, na uwezo wa kuwasilisha kwa mvuto na weledi kwenye redio?
📌 Maombi yanapokelewa sasa!
⏰ Deadline: Tarehe 08/05/2025
📩 Jinsi ya kutuma: (eleza kwa kifupi au weka link kwenye bio/post)