Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akicheza Wimbo wa Hamasa ya maendeleo pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 10 Juni 2020 kabla ya kuanza kwa Kikao hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. @SuluhuSamia akizungumza na Viongozi na Watumishi waandamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Baaraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)leo katika ukumbi wa Mikutano wa Kambarage Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi mara baada ya Kwaya ya Chama cha Walimu CWT kutumbuiza katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa @MagufuliJP akizungumza na viongozi pamoja na wawakilishi mbalimbali wa Chama cha Walimu CWT kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CWT uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo tarehe 5 Juni 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
@MagufuliJP akipiga makofi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu wakati Kwaya ya CWT ilipokuwa ikitumbuiza.
"Tuliambiwa tujifungie ndani yaani hata misikitini na Kanisani tusiende, hii ni kufuru kubwa. Yaani wakati wa shida ndio wa kumkimbilia Mungu sisi tunamkimbia Mungu na kujifungia ndani huko ni kumpa ushindi Shetani" Mhe. Rais Dkt.
@MagufuliJP
"Baada ya suala la kuzikwa kushindwa, wakaja na madai kwamba Tanzania kuna Ebola, kwamba wakisema hivyo walilenga kuwa tutapoteza watalii, na wakaeneza propaganda watu wanakufa tu barabarani, sisi tukawaambia hatuna Ebola" Mhe. Rais Dkt.
@MagufuliJP
''Tulipoingia madarakani tukatangaziwa kuna homa ya Zika, nikamfukuza kazi aliyetumwa kutangaza, baada ya siku chache akateuliwa na waliomtuma wakampa ukurugenzi, tangu hapo hatujawahi kupata kesi ya zika'' -
@MagufuliJP
“Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali imeongeza nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka 53,302 hadi nyumba 57,541,”-
@MagufuliJP
'Ili kuepuka udanganyifu, Serikali kwasasa inaandaa mfumo wa kielektroniki wa kuhakiki madai ya watumishi wakiwemo walimu, ambao utaanza kutumiwa kwa majaribio mwezi huu hapa Dodoma na endapo utaonesha mafanikio utatumika kwa nchi nzima'' -
@MagufuliJP
"Tangu tulipoingia madarakani tumeshalipa madeni ya malimbikizi ya mishahara bilioni 115.3 kati ya hizo bilioni 38.3 walilipwa walimu 35,805 hii ni kutokana na taarifa ya jana kutoka wizara ya fedha, madeni ya likizo na yasiyo ya mishahara tumelipa bilioni 358.1"Rais @MagufuliJP
"Kada ya Ualimu ndio inayongoza, kati ya watumishi wa umma 524,295 walimu wako 266,905 sawa na 51% ya watumishi wote, serikali inafahamu upungufu wa walimu ya sayansi, hesabu na lugha, na mwaka huu wa fedha unaomalizika tunatarajia kuajiri walimu 13, 526"Mhe. Rais Dk.@MagufuliJP
"Tangu tulipoingia madarakani tumeshalipa madeni ya malimbikizi ya mishahara bilioni 115.3 kati ya hizo bilioni 38.3 walilipwa walimu 35,805 hii ni kutokana na taarifa ya jana kutoka wizara ya fedha, madeni ya likizo na yasiyo ya mishahara tumelipa bilioni 358.1"Rais @MagufuliJP
''Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita miongoni mwa mambo makubwa tuliyoyafanya ni kutoa elimu bila malipo, jumla ya kiasi cha Sh Trilioni 1.01 tumekitoa kwaajili ya kugharamia elimu kati ya Disemba 2015 na Februari 2020'' -
@MagufuliJP
"Ufaulu wa kidato cha nne umepanda kutoka asilmia 69.8 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 80.65 mwaka 2019, hongereni sana walimu kwa kazi nzuri" Mhe. Rais Dkt.
@MagufuliJP
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mwenyekiti wa @ccm_tanzania Mhe. Dkt. @Magufuli akizungumza jambo na Rais wa #Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein Ikulu ya Chamwino Dodoma leo.
Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akizungumza na wajenzi kutoka JKT mara baada ya kukagua kazi za Ujenzi wa Ofisi za IKULU
Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiangalia kibao cha jiwe la msingi la Ujenzi wa Uwekaji Ofisi za Ikulu ya Chamwino.
Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mohamed Ali Shein akiweka udongo katika jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi za Ikulu na kukagua maendeleo ya kazi ya ujenzi wa ofisi hizo inayofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia shirika lake la Suma JKT.