@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
#TANZANIA: ALIYEWAKEJELI VIJANA WA GEN Z ATAKIWA KUOMBA RADHI
"Nakutaka utuombe radhi kwamba hatujui tunachokitaka, sisi Young generation (Gen Z) tunajuwa tunachokitaka, ndio maana hawa wanaofanya wanayoyafanya wanajuwa kwamba hawawezi kutupa tunachokitaka kama vijana wa Gen Z" - Rukaya
Zaidi: https://t.co/1WOZ4QSppc
Serikali ipunguze kodi kwenye Mafuta kwa muda wa miezi sita kuondokana na azma hii
Kasumbalesa Zambia umbali wa km 1980 kutoka Dar port bei ya Mafuta iko chini Sababu kuna tozo wamepunguza.
Hatuwezi endesha nchi namna hii mfumuko wa bei utakuwa Mkubwa zaidi.
Baada ya kukabidhi Ripoti by necessary implication tume inakuwa imekufa kwani inakuwa imemaliza kazi. Ndio maana baada ya kukabidhi ripoti kinachofuata ni hatua za kuchukuliwa na mteuzi.
TUNACHOONA HAPA NI TUME KUPOTEZA MUDA hawana mamlaka kisheria kufafanua ripoti iliyotolewa
@HildaNewton21@Oleshangay Nadhani siasa za namna hii hazina mvuto jina lako umetumia nguvu sana kulitengeneza hivyo usifanye hivi utajiharibia tujikite kwenye kutoa hoja na kujibu hoja nakutoa elimu kwa watu wako
Uadilifu na kujiheshimu ni tunu kubwa sana! Pale mtu mzima unapojitoa ufahamu, ukakosa haya hata kuuza utu wako kwa vipande thelathini vya fedha kama Yuda Iskariote, unakuwa umejidhalilisha na kupoteza hadhi yako. Je, kweli unapata usingizi wa amani?
#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 6
Anaendelea Wakili wa Said Issa na wenzake
Suala la amri ya zuio inamuhusu nani?
Record yenyewe ya Revision inajieleza nani inamuhusu. Page 153 imewaeleza wanaouzuiwa. Wametajwa bodi ya wadhamini na katibu mkuuu.
O.XXXVII ya CPC inasema kuwa order ya bodi ya wadhamini itawahusu wahusika pekeee. Sasa ukiitaja bodi ya wadhamini maana yake ni Chama chote.
Jaji kwani order inaposema na waliopo chini yake Katibu Mkuu ni chini hadi wapi?
Jaji mwingine anasema walisema kuwa servants na wengine wote wanaofanya kwa niaba sasa je kuna yeyote ambae angeweza kufanya shughuli nyingine?
Wakili naomba niendeleee
Jaji kabla hujaendelea sasa tusaidie mahusiano ya madai ya mali na kufanya shughuli za Chama?
Wakili anajibu waheshimiwa madai hapa sio mgawanyo wa mali lakini kweli mgawanyo wa Mali ni madai ila kitu cha msingi ni kifungu cha 6 cha Political Party Act.
Jaji hebu kisome halafu tuambie kinasemaje na maana yake.
Anakisoma hapa.
Anasema sasa matendo ya viongozi wa Chama yaliwakera wananchi wa Zanzibar.
Jaji wananchi wa wapi?
Wakili Mhe. Jaji namaanisha wakazi wa zanzibar.
Jaji una hakika wakazi wa zanzibar hawakufurahia
Wakili ni wanachama tu.
Jaji unajua kanuni za kutoa interim order hilo zuio?
Jaji mwingine na utuambie nani angepata athari zaidi kwa mfano nyie mmgeshindwa hiyo petition yenu kati yenu na respondents nani angeathirika zaidi?
Wakili sasa waheshimiwa majaji naona kama mnazungumzia kesi ya Attilio vs Mbowe
Bila kuzuia wasitumie hizi property basi wote wasingetumia na zingekuwa salama kwa wote.
Pia kufanya political activities lilikuwa ni zuio la muda tu, zingeachwa zingeendelea kutengeneza friction baina ya members.
Jaji sasa tuambie irreperable loss ni ipi?
Wakili tulisema sera za Chama zinaenda kuwa damaged.
Jaji tena anamuuliza Marijan kwahiyo unasemaje kuhusu kilichoombwa kwenye main case ni kama kilishatolewa kwenye ombi la zuio?
Wakili ni kama vinafanana lakini vinatofautiana.
Jaji huoni amri ya kwenye maombi madogo inaweza kuwafanya waleta maombi wakaona wameshamaliza kesi yao wakaanza kuchelewesha kesi ya msingi au wakaona haina msingi?
Wakili washemiwa nafikiri hakuna mwenye nia ya kupoteza muda kwenye shauri la msingi hivi.
Majaji wanatabasamu na kucheka ki kituristi kidogo halafu wanaandika kwa umakini mkubwa.
Jaji sasa mlisema hii kesi ni ya aina gani?
Wakili sisi tunasema haki zilikuwa infringed
Jaji hizo haki zipo wapi si Article 30?
Wakili ndio ni Article 30.
Jaji sasa kama ni Article 30 ya Katiba ndio zimevunjwa. Swali letu hii ni kesi gani? Ya Kikatiba au sio ya Kikatiba.
Jaji mwingine anasema sasa hapa una address jambo gani hebu tuambie maana kila kitu kina utaratibu wake sasa tueleze.
Anasimama Wakili Kiharuzi kuwa applicants hawahangaiki na haki za kikatiba.
Ila wanachosema ni maombi ambayo yanawaomba ku comply na matakwa ya kisheria hii ni CIVIL Case. Inawalazimisha
Jaji hebu subiri kwanza hoja hapa ni kwamba order ya zuio inaathiri haki zingine za Kikatiba, unasemaje?
Wakili sisi tunasema hayo ndio matokeo ya kosa walilolifanya.
Jaji kwahiyo unasema ni sahihi kuwa constitutional right zimekuwa infringed au vipi? Usituambie mambo ya inawezekana. Tujibu kuwa haki za kikatiba za wanachadema zimenyimwa au hazijanyimwa kwa maoni yako sasa?
Je haki ya kufanya siasa ni haki ya kikatiba au sio? Je mtu akizuiwa ni sahihi?
Sisi hatukufika kwenye Katiba anasema Wakili.
Jaji ndio tunawauliza hii kesi yenu ni Civil Case?
Wakili ndio hii ni Civil Case.
Jaji sasa kwanini hamkuiita Plaint na iwe ni Civil Case.
Jaji mwingine kwahiyo hii mnasema kuwa ni Suit under Civil Procedure na haikuletwa kwa njia ya Plaint? Unasemaje hapa.
Wakili, Mheshimiwa Jaji hii ni Civil Case.
Anakaaa anasimama tena Manywele Waheshimiwa Majaji kuhusu suala amri ya zuio inadumu kwa miezi sita tu.
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MGAWANYO_MALI_ZA_CHADEMA
Part 1
Mahakama imeanza!
Mawakili wa pande zote mbili wapo.
Anaanza Wakili wa upande wa waleta maombi Mzee Mpale Kaba Mpoki @MpaleMpoki
Kuhusu hoja ya Cause of action ilianza lini yani madai ya akina Said Issa na wenzake yalianza lini wao wanasema ni mwaka 2016.
Kwa Mujibu wa Sheria ya Law Limitation Act kipindi cha mwisho kwa kesi ambazo hazijaelezwa na sheria itakuwa ni miaka 6 lakini wao wameleta kesi hii baada ya miaka 9.
Na jambo hili hawajalisema kwenye kesi yao ya msingi hata hiyo ya kuwa cause action ilianza mwaka 2016.
Wamekuja kuisema baadae kwenye pingamizi lao kuwa Mwenyekiti wa Chama asiunganishwe kwenye maombi yao ya msingi.
Sasa sisi tunasema kwenye shauri/maombi ya msingi hawakusema cause of action ilianza lini lakini hata hili la 2016 walilolisema liko nje ya muda.
Labda ingekuwa kesi ya Kikatiba wangeweza kuruhusiwa maana hakuna limitation of time.
Lakini hii kesi yao sio ya Kikatiba kwasababu kwanza imesikilizwa na Jaji mmoja na hakuna kesi ya Kikatiba inasikilizwa na Jaji mmoja.
Sasa Effect ya kutokuweka Cause of Action O. VI r.11 ya Civil Procedure Code katika hali ya kawaida hii kesi ilipaswa kuwa rejected na Court kwasababu haikuonesha ni lini Cause of action arouse.
Eneo lingine ni Failure to raise the value of the property. Takwa la ku disclose cause of action pia iko O. VII r. 1(i) ya CPC. The value of the subject matter of the Suit is of paramount importance for the case to be admitted.
Sheria inasema tunaweka value ya subject matter ili kuonesha pecuniary jurisdiction lakini kuisaidia mahakama kujua inacharge kiasi gani ili kuilipia gharama za kusajili kesi husika.
Sasa Ukurasa wa tano wa bando tulilowapa. Mara nyingi tungeona wamesema value ya subject matter lakini hawajasema.
Madai yao yaliyopo ukurasa wa nne wanadai distribution un even distribution of party asserts na pia paragraph 7 inasema tuna nyumba mikocheni yenye thamani ya milioni 726, landed property zenye thamani ya bilioni 2 na usheee, kulikuwa na magari 8 yenye thamani ya 576 milioni, Pikipiki 478.
Sasa hawajasema thamani ya wanachokidai ni shilingi ngapi?
Tumeangalia kwenye filing system imelipiwa kama fees ya shilingi elfu 50.
Sasa naomba niwapeleke kwenye GN. No. 247/2018 Court Fees Rules ambayo inasema inazidi kiwango cha juu zaidi inapaswa kulipiwa milioni 5.
Receipt ambayo tumeiona ni ya elfu 50, mtu ambae anaamua walipe shilingi ngapi angesema walipe milioni 5 na sio elfu 50.
A case has been deemed proper filed once the proper fess has been paid accordingly and as it is required by the law. Sasa ni wasilisho letu ni kwamba order ya injuction haikuwa sahihi kutokana na hakukuwa na kesi iliyofailiwa Mahakamani. Na tunaona lilikuwa ni pungufu kubwa sana.
Sasa naomba Dr. Rugemeleza Nshala aendeleee.
Dr. @rugemeleza anaanza. Nawashukuru sana kwa nafasi.
Naomba nizungumze hoja moja kwanza ukurasa wa 4 wa petition yao. Kwenye hoja ya Kikatiba.
Anasoma maneno yao ambayo wanasema viongozi wakuu wamekuwa wakisema maneno dhidi ya Zanzibar ambayo yanatishia Muungano na utendaji kazi wao kama wazanzibari.
Sasa Maneno haya yanaonesha madai yao ni ya Kikatiba. Na kesi hii ilipaswa kuwa ya Kikatiba. Lakini kesi hii imesikilizwa na Jaji mmoja na haikuwa kabisa kesi ya Kikatiba.
Jaji alipelekewa suala hili akasema mambo ya Kikatiba tuachane nayo. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ilikuwa ni hatari sana kwa Jaji mmoja kujivika madaraka ambayo hana.
Kesi za Kikatiba yanaletwa chini ya BRADEA au kwa mujibu wa ibara ya 108 ya Katiba. Hawajafanya hivyo.
Haya Madai yao yana UVUNDO sina Lugha nyingine ya kutumia Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Sasa Dr. Nshala anaendelea hapa.
Wafungua maombi wa 2 na 3 wamesema wao ni member wa Board of Trustees ya Chama.
Sasa sisi tunasema hawawezi kufanya hivyo kwasababu wanapingana na Trustee Incorparation Act.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
TAHADHARI! TAHADHARI! TAHADHARI! Vigelegele kwa Samia ni too premature. Tulipiga vigelegele Magufuli alipoingia ofisini. Tulifanya kosa hilo hilo kwa Kikwete 2005; na kwa Mkapa 1995. Tuache vigelegele; tudai vitendo zaidi. Actions speak louder than words! Tujifunze tulikotoka!
Unajua kwanini Mungu ataingilia kesi yetu hivi karibuni?? ni kwa sababu kule mbele kuna giza zaidi ya hili. Kuna mtu ananyemelea kule juu. Ni mbaya sana, ni Shetani-mwanadamu, kwa nje kama mkristo, mpenda watu, mtoaji. Ila hatutafika huko. Mungu ameshamuona, ameshamzuia.