Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri wakikagua ujenzi wa chumba cha Maabara cha Sekondari ya wavulana ya Muungano iliyopo kijiji cha Rubambangwe kata ya Muungano
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri leo imetembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri, Kamati hiyo imemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha anakamilisha miradi yote ambayo haijakamilika ikiwemo mradi wa kituo cha Afya cha Katete
Halmashauri ya Wilaya ya Chato leo imeibuka mshindi tatu kwenye kundi la Halmshauri kwenye maonesho ya 5 ya Kitaifa ya Teknolojia ya Dhahabu yaliyohitimishwa leo mjini Geita na waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
Mbunge wa Geita mjini mhe. Constantine Kanyasu ametembelea banda la Chato kwenye Maonesho ya 5 ya kitaifa ya Teknolojia ya Dhahabu yanayoendelea mjini Geita. Mhe. Kanyasu amewashauri wajasiriamali wa Chato kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinaenda sambamba na bei halisi ya soko
Wananchi wa kata ya Bwongera wilayani hapa wamechangishana fedha kiasi cha shilingi milioni 6 kwa lengo la kutengeneza barabara inayounganisha kata hiyo na kata jirani ya Nyamirembe ili iweze kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka shambani
Mikopo ya asilimia 10 ya vijana, wanawake na wenye ulemavu, kikundi cha akina mama kilichopo kijiji cha Msilale Kata ya Chato chenyewe kimenufaika na mikopo na kujikita kwenye uuzaji wa Dagaa na Samaki kutokana na mikopo hiyo isiyokuwa na riba inayotolewa na Halmashauri
Mikopo ya asilimia 10 ya vijana, wanawake na wenye ulemavu, kikundi cha vijana cha Mpogoloni Chato chenyewe kimenufaika na mikopo ya Pikipiki (bodaboda) kutokana na mikopo hiyo isiyokuwa na riba inayotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Chato
DC CHATO AHESABIWA
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi akizungumza na karani wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Consolatha Chrispine, wakati alipokuwa akihesabiwa katika makazi yake kijiji cha Mlimani leo tarehe 23.08.2022 kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wa ndugu Mandia Kihiyo akizungumza na karani wa Sensa ya Watu na Makazi Bi. Consolatha Chrispine, wakati alipokuwa akihesabiwa katika makazi yake kijiji cha Mlimani leo tarehe 23.08.2022 kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
Mkuu wa Mkoa wa Geita mhe. Martin Shigela leo amefanya ziara ya siku moja yenye lengo la kujitambulisha wilayani hapa.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ametembelea pia hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato ambapo ameipongeza serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya umaliziaji