Serikali yaanza kukusanya pesa za CHF kwa mfumo wa Kielektroniki. Kuanzia sasa pesa za CHF zitaanza kukusanywa kwa njia ya kuomba Control number nakufanya pesa kufika kwenye akanti ya CHF na wanachama kupata huduma. Pia njia huwa epusha wandikishaji kukaa pesa muda mrefu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino A. H. Masasi (kulia) akijiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mapema leo hii.
Mwisho wa kujiandikisha siku ya Jumatatu tarehe 14 Oktoba, 2019.
Leo tarehe 9 Oktoba, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Vumilia Nyamoga ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama kutembelea vituo vya uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kabla ya 14.10.2019 saa 12 jioni.
Leo tarehe 9 Oktoba, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Vumilia Nyamoga ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama kutembelea vituo vya uandikishaji kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kabla ya 14.10.2019 saa 12 jioni.
Leo tarehe 20/9/2019 Mkurugenzi Chamwino Ndugu A.H.Masasi amefanya kikao na watumishi wa kada zote za Halmashauri, asikiliza kero na kuzitolea majibu ya ufumbuzi. Awataka watumishi kutekeleza maagizo yanayotolewa na viongozi na kufanya kazi kwa uzalendo.
"Ukiachilia mbali CHF kuwa mfuko wenye gharama nafuu zaidi nchini, CHF hurudisha fedha kwenye Zahanati na Vituo vya Afya kulingana na idadi ya wananchi waliojiandikisha katika eneo husika. Fedha hizo zinasaidia ununuzi wa dawa na vifaa tiba" Dkt Kessy-Mganga Mkuu Wilaya Chamwino
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndugu A.H.Masasi anawatakia kila la kheri wanafunzi wa Darasa la Saba wilayani Chamwino na nchi mzima kwa ujumla katika mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi itakayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 11 Septemba 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndugu A. H. Masasi anawatakia kila la kheri wanafunzi wa Darasa la Saba wilayani Chamwino na nchi mzima kwa ujumla katika mitihani ya kuhitimu Elimu ya Msingi itakayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo 11 Septemba 2019.
Tarehe 06 Septemba 2019, Mkururugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Ndugu A. H. Masasi amewasainisha Mikataba Watendaji wa Kata ikiwa ni makuliano ya kwenda kusimamia utoaji wa elimu ya lishe katika maeneo yao.
Leo tarehe 04 Septemba 2019, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge anafanya ziara ya kikazi Wilayani Chamwino kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Tembelea https://t.co/obFgNZKmwQ kujua yote yanayojiri.
TAARIFA KWA UMMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Athumani H. Masasi, anautaarifu umma hususani wa Wilaya ya Chamwino kuwa tarehe 29-30/08/2019 kutakuwa na Kikao cha Baraza la Madiwani kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa Kijiji cha Chamwino Ikulu kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Vumilia Nyamoga, ameupokea Mwenge wa Uhuru asubuhi hii tayari kuukimbiza .
tembelea https://t.co/UxgyMUIOU7 kujua yanayojiri.