SIASA NI WATU
NYASA inayoundwa na Iringa,Njombe,Mbeya,Songwe na Rukwa itakua Ikumbilo,Ileje.
Ninapokea na kuzitunza baraka za safari Mpya toka kwa watu wema wa NYASA.
#Leadership_without_tittle.
#ILEJE_2025.
Nikiwa Dar mlianza na Noah ya Silver, mkajua ninalolala na mizunguko yangu ya siku nzima. Nikiwa Dodoma mkanifuatilia na Toyota Corrolla nyeupe na leo ni Land Cruiser nyeusi isiyokuwa na plate number. Bahati nzuri nilitaarifiwa haya hili mapema na watu wanaonipenda. SINA HOFU.
“Kwa aina ya bunduki walizokuwa nazo hao watu waliokuja kumchukua (Mzee Ally Mohamed Kibao ambaye ni mjumbe wa sekretarieti ya chama taifa (CHADEMA)) kwenye basi si bunduki ambazo kwa kawaida hutumiwa na Jeshi la Polisi, ni bunduki ambazo hutumiwa na Idara ya Usalama wa Taifa.Wakati tukifuatilia taarifa zaidi na wakati tukijiandaa kuchukua hatua zaidi kuja kwenye vyombo vya habari kueleza tu kwamba kiongozi wetu na mwenzetu ametekwa na vyombo vya ulinzi na usalama, nitoe wito kwa IGP wa Jeshi la Polisi Mkuu wa Jeshi la Polisi kueleza iwapo Ally Kibao ametekwa na Jeshi la Polisi, waeleze sababu za kumteka, yupo wapi, na ana hali gani. Kwa kawaida huwa tunajizuia sana kuzungumza kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa lakini kwa sheria ya idara ya Usalama wa taifa kuna mtu mmoja tunaweza tukamtaja na tunaweza kumzungumza, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa natoa wito kwake ajitokeze aeleze iwapo idara ya usalama wa taifa imemteka Mzee Ally Mohammed Kibao, yuko wapi? - Mnyika.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika akizungumza na wanahabari mchana wa siku ya Jumamosi Septemba 7, 2024 Makao Makuu ya CHADEMA, Dar es Salaam.
Maisha ni mafupi sana. Ila watawala wanataka kutuuwa mapema watawale bila bugdha.
God is this what you meant for us?
Hatukuja duniani kuwa kondoo.
And we reject all attempts to make us apologists.
Release Deus Soka & all the boys, NOW.
‼️🚨 ANOTHER ABDUCTION BY PEOPLE CLAIMING TO BE POLICE‼️🚨
#Tanzania
Ali Mohammed Kibao a member of the opposition @ChademaTz secretariat was taken by unidentified men from the bus he was travelling on at night!
This is too much @SuluhuSamia
Stop #EnforcedDisappearances ❌
Hii ni panic ya CCM kuhusu uchaguzi! Tusipofanya jambo kubwa la ku push back watateka wengi hadi #TutaelewanaTu
Meko alimuweka SHASHA lockup mara kadhaa alipotaka kujiuzulu. Uzoefu huo haujamsaidia.
SASHA anaona sawa watoto wa w/wake wenzie watekwe & kuteswa kwa siku 18 sasa.
Anyways, furahia mamlaka, asubuhi yaja.
Stay stronger, young G.
Katibu Mkuu CHADEMA @jjmnyika akieleza jinsi Mzee Ally Mohammed Kibao, mjumbe wa Sektretariati ya CHADEMA alivyotekwa ndani ya basi la TASHRIF linalofanya safari zake Dar es Salaam - Tanga, eneo la Kibo, Tegeta, DSM. Hadi sasa hayupo kituo chochote cha polisi. #zuiautekaji
UONGO WA IGP MAHITA KWA CUF; UONGO WA POLISI KWA CHADEMA.
POLISI kupitia Msemaji wake DCP David A. Misime limetoa tuhuma kwa CHADEMA katika taarifa kwa umma kwamba viongozi wa CHADEMA kupitia kikao cha ZOOM, wamepanga kuvamia vituo vya polisi kwa wakati mmoja katika makundi ya watu 20.
CHADEMA wamewaita waandishi wa habari na kuwaeleza taarifa ya Polisi ni uongo na uzushi yenye lengo OVU zaidi kwa CHADEMA. Hii imenikumbusha mwaka 1995, IGP akiwa ALHAJI OMARI IDDI MAHITA alipowazushia uongo CUF.
Kila nyakati za kuelekea uchaguzi mkuu, Jeshi la Polisi wanatoa tuhuma nzito kwa chama kikuu cha Upinzani, ambacho kinakuwa na nguvu na ushawishi wa kisiasa. Jeshi la Polisi wanatoa tuhuma nzito ambazo ni ngumu kuthibitisha sehemu yoyote.
1995 Omari Mahita akiwa RPC kilimanjaro, Augustine Mrema alikwenda Moshi kufanya mkutano wa hadhara na baadae kufanya maandamano. Mahita aliamuru Mrema achakazwe na mabomu yaliyopelekea Mrema kuugua macho, muda mrefu.
RPC Alhaji Omari Iddi Mahita akajitapa mbele ya vyombo vya habari …., “kama (Mrema) ulikuwa bosi wangu ni zamani sio sasa”, kitendo hicho kilimpa ujasiri ndani ya CCM na kupandishwa cheo kuwa INSPECTOR GENERAL OF POLICE (IGP).
Augustine Lyatonga Mrema alikuwa mwanachama wa CCM, waziri wa mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu kabla ya kuhamia NCCR-Mageuzi na kuwa mgombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995. Mahita akajichukulia pointi tatu kwa gwiji..
Chama cha Wananchi (CUF), chenye ofisi zake Buguruni ,Dar es Salaam, kilikuwa ni chama cha upinzani chenye nguvu, ushawishi na Polisi iliyokuwa chini ya (IGP), Omari Mahita ilielekeza nguvu zake kupambana na wafuasi wa CUF.
Wafuasi wa CUF walikuwa wakikaidi amri haramu za polisi ambazo zilikuwa zikipiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara iliyokuwa inapangwa kufanya na chama hicho siku ya Ijumaa baada ya ibada ya waumini wa dini kumalizika.
Mara nyingi maandamano ya CIVIC UNITED FRONT - CUF ambayo yalikuwa yanapigwa marufuku na Jeshi la Polisi yalikuwa yakianzia Buguruni (yalipo makao makuu ya CUF) kuelekea Uwanja wa Kidongo Chekundu Dar Es Salaam katika kusanyiko lao.
CUF ya enzi zile kati ya 1999-2005 kilikuwa ni Chama chenye wanachama ambao walikuwa na umoja na ujasiri na na baadhi ya wanachama wake walikuwa na ujasiri wa kukaidi amri za Jeshi la Polisi na kuamua kuingia barabarani kuandamana.
Walifanya mikutano ya hadhara, katika mikutano, matokeo yake yalikuwa ni kupokea vipigo, kurushiwa mabomu ya machozi na Polisi na wengine kufunguliwa kesi za jinai mahakamani. CUF waliitaabisha serikali ya Benjamin Mkapa ipasavyo.
Maandamano mengi ya CUF yalitaabisha jeshi la polisi ambayo waliyapiga marufuku kupitia aliyekuwa msemaji wa Jeshi la Polisi enzi za IGP - Omari Mahita, Aden Mwamunyange na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar Es Salaam Enzi hizo, Alfred Gewe.
2005 kuelekea uchaguzi mkuu, katikati ya joto kali la Uchaguzi Mkuu, baada ya kubanwa na (Civic United Front - CUF), serikali ya Benjamin W. Mkapa ilimtumia Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Omari Mahita, kutisha wapiga kura.
Kulikuwa na wimbi kubwa la ujambazi. IGP Mahita na jeshi la polisi wakatuhumu CUF walikuwa nyuma ya ongezeko la vitendo vya ujambazi. Kwamba CUF walikuwa wakiendesha kwa siri UJAMBAZI ili kuikomoa Serikali ya Benjamin W. Mkapa,
Lengo kuu la tuhuma za Mahita zlikuwa kuiharibia haiba ya CUF mbele ya jamii, akaongeza pia, ajenda nyingine ya CUF ilikuwa kumchonganisha Mahita na Rais Mkapa ili aonekane hafai, kwamba ameshindwa kudhibiti ujambazi, au anaihujumu serikali.
Mahita aliwatuhumu CUF kwa kueneza uvumi mitaani kwamba anashirikiana moja kwa moja na majambazi. Akaweka wazi uhasama wote huo ni kwa vile CUF inamtuhumu yeye kuwa atachangia kwa kiasi kikubwa katika kushindwa kwao uchaguzi.
Mahita akaweka wazi kwamba angeondoka madarakani kwa nguvu za Mungu pekee na kuwa haogopi mtu yeyote, tena akashindwa kujizuia akisema kwamba CUF kamwe haitaweza kuingia Ikulu hata kama yeye hatakuwepo Polisi. Aliweka nadhiri.
Baada ya hotuba hiyo ya kushtusha, sio CUF pekee waliotoa misimamo, hata wanasiasa wa vyama vingine vya upinzani waliingilia kati na kuitaka Serikali kuunda tume kuchunguza tuhuma hizo ili sheria ifuate mkondo wake dhidi ya mkuu wa polisi.
Kwa upande wao CUF waliibuka kwa nguvu na kufanya maandamano makubwa wakimtaka Rais amtimue kibarua IGP Mahita mara moja. Kadhalika waliahidi kwenda mahakamani kufungua kesi dhidi yake kwa kuchafuliwa jina mbele ya jamii.
Serikali haikusema lolote zaidi ya kukana kuhusika na maneno ya Mahita kupitia Waziri wa mambo ya ndani, Omari Ramadhan Mapuri. Ikafuatia mikanganyiko ndani ya Polisi. Utajiri binafsi wa Mahita na jinsi alivyoupata, umri wake na tarehe ya kustaafu.
Msemaji wa jeshi la Polisi, SACP Aden Mwamunyange, akasema Mahita alimuandikia barua Rais tangu 2005 akiomba kustaafu. Mwamunyange akaitaja tarehe rasmi ya kustaafu kwa bosi wake akitoa vielelezo vya umri na tarehe yake ya kujiunga na jeshi.
Tarehe ya kustaafu IGP Omari Iddi Mahita ilikuwa iwe 04 Mei 2006 hata hivyo tarehe hiyo ikabatilishwa na Mahita akastaafu kabla. Haikuwahi kuelezwa au kujulikana sababu za msingi za kwanini alistaafu kabla ya tarehe yake rasmi ya kustaafu kufika.
Je, Omari Mahita alistaafu chini ya shinikizo fulani. Je, ni sakata lake na CUF? Je, ni tuhuma zilizokuwa zikimkabili juu ya kuushindwa uhalifu. Je, Serikali iliamua kumaliza mizozo kwa busara ya kuung’oa mzizi wa fitina? Yote yanawezekana!
Sakata hili lilipamba moto katikati ya simanzi ya ongezeko la ujambazi nchini, lililoitia Serikali hasara ya mabilioni na kupoteza roho za watu wengi wakiwa vilema, yatima au wajane. Katika kutafuta mchawi ndipo wakubwa hawa walipoanza kutajana.
Minong’ono ikaenea IGP Omari Mahita yuko nyuma ya uhalifu huo. Mahita akajitokeza na kusema anawajua wanaoeneza minong’ono hiyo na sababu zake. IGP Omari Mahita akataja Civic United Front - CUF kwamba ndio wahusika wakuu wa ujambazi
Tuhuma hizo hatari zikawashtua watu hata waliokuwa serikalini. Serikali ilikana kuhusika nalo. Pamoja na historia yake ya kijeshi na sifa lukuki na nishani, Mahita anatajwa kuwa na tatizo kubwa la kuzungumza kwa hisia kali, hasira na kukosa utulivu.
Mara nyingi alionyesha kushindwa kuzuia jazba yake na kujikuta akiropoka mambo yaliyomtia mara kadhaa katika mizozo na migogoro na wanasiasa, hata kama aliyoyasema yalikuwa na ukweli ndani yake, hakuweza kuyawasilisha kwa utulivu na utimamu.
Alahaji Onari Mahita aliingia katika mzozo na wabunge ambao aliwataka wakatwe posho zao wakalipwe askari Polisi, Mahita hakupenda kuonekana mwoga huku akitumia nguvu ambazo mara nyingi zilimfanya anase kirahisi katika mitego ya wanasiasa.
Hoja ya wabunge ilikuwa Jeshi la Polisi lilistahili kuvunjwa ili liundwe upya. Wabunge wakatoa mfano wa Jeshi la kikoloni la King African Rifles (KAR), lilivyovunjwa baada ya maasi ya 1964 na kuundwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hoja ya wabunge ilitokana na ongezeko la ujangili na mauaji. Kwamba, Polisi wameshindwa kazi. IGP Mahita alijibu mapigo kwa kusema kama wabunge wanataka kuona utendaji kazi wa Polisi, basi wawe tayari kuwalipa vizuri kama wao wanavyolipwa.
Mara nyingi alisimama kama Omari Mahita na siyo IGP. Sikiliza hotuba zake za mgogoro wake na (CUF) hadi kujiita ‘ngunguri’ baada ya CUF kujiita ‘ngangari’. Hii ilimfanya Mahita wakati mwingi awe Katika mizozo ,iwe na taasisi au mtu binafsi,
IGP Omary Mahita akavaa mabomu kumfurahisha RAIS Mkapa. Akaibukia kwenye TV akiwa na majambia visu vilivyopakwa rangi za bendera ya CUF, akisema wamekamata kontena la visu ambavyo CUF walikuwa wanakusudia kufanyia ugaidi.
Kisanga hicho kilikuwa ni 2005, mbele ya maafisa wa Polisi katika ukumbi wa bwalo la Polisi, Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam. Mkononi ana visu na majambia, vikiwa vimepakwa au kufungwa vitambaa vye rangi za bendera ya CUF.
Hadi leo polisi na serikali ya Mkapa hawajatueleza visu hivyo vilipelekwa wapi. Kontena liliishia wapi. Hatujasikia mtu au kiongozi wa CUF amekamatwa kwa ugaidi. Hakuna kesi dhidi ya viongozi au wanachama wa CUF kutokana na tukio hilo.
Ni wazi lilikuwa tukio la kupika na kuichafua CUF mbele ya umma. Ilikuwa mbinu ya ushindi mchafu. iliwasaidia kuipiku CUF na kuidhoofisha mbele ya macho ya wapiga kura. Na hizo zimekuwa mbinu chafu za CCM nyakati zote ukifika uchaguzi.
Visu 20 vilivyotengenezwa SIDO vikatumika kuchafua taswira ya CUF. CUF ndiyo walikuwa chama kikubwa cha upinzani Tanzania wakati huo. CCM kupitia IGP Omari Mahita wakajenga hofu kwa jamii kwamba CUF ni chama cha kigaidi, wasiichague.
Ukazuka mjadala mkubwa. Kwa kuwa ujambazi umekithiri na IGP Mahita anatuhumiwa kushirikiana na majambazi na kwamba anawatuhumu CUF. Je, ni kweli benki na maduka na magari barabarani yanavamiwa na visu vya CUF na siyo bunduki?
Vilelezo (visu vyenye rangi ya nyeupe na nyekundu - rangi ya bendera ya CUF) vilikataliwa. Visu hivyo aliwahi kuvionyesha Waziri wa mambo ya ndani, Omari Mapuri wakati wa kampeni na kusema ni maandalizi ya CUF ya kuchafua amani ya Tanzania.
IGP Omary Mahita akaingia katika mgogoro mkubwa na wafuasi wa CUF. February 19, 2006. Wanachama na wafuasi wa CUF wakaandamana kushinikiza IGP, Omary Mahita apigwe chini baada ya kuwatuhumu Civic United Front - CUF kwa ujambazi.
Jakaya Kikwete hakumuondoa kama matakwa ya CUF yalivyokuwa. IGP Omari Mahita akastaafu mwezi uliofuatia. Alistaafu Machi 4, 2006 akiwa na miaka 60, wadhifa alioutumikia kwa miaka 10 tangu mwaka 1996 akaingia Said Ally Mwema.
Ujio wa IGP Said Mwema ukawa wa ahueni kwa wananchi. Polisi walipata vitendea kazi vya kutosha. Wakapambana na ujambazi. Uporaji fedha ulioshamiri kwenye benki, ukapungua na hata kukoma. Je, Mahita alishirikiana na majambazi?
Said Ally Mwema akahudumu kwa miaka nane. Akateuliwa Ernest Jumbe Mangu ambaye alihudumu kwa miaka minne tu. Akateuliwa Simon Nyakoro Sirro. Omari Mahita alitanguliwa na Haroun G. Mahundi ambaye alihudumu kwa miaka 12.
Baada ya kustaafu, Mkuu wa Polisi, Alhaji Iddi Omary Mahita alijiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kufanya kazi za CCM hadharani. Hii ikadhihirisha wazi vita yake na CUF akiwa IGP ilikuwa ni kwa manufaa ya CCM na serikali ya Benjamin Mkapa.
Hizi chokochoko za Polisi sasa kwa CHADEMA, zinaturejesha nyakati hizo. Tanzania inarudi nyuma hatua nyingi katika demokrasia. Jeshi la Polisi limeshindwa kuacha vyama vya siasa vya Upinzani vishandane kisiasa na CCM kutafuta DOLA.
PS; Pamoja na hayo, nashauri, CHADEMA wasiache hizi tuhuma zibaki hivyo kwa sababu siyo tuhuma za kisiasa, zimetoka Jeshi la Polisi. Hivyo, CHADEMA washtaki Polisi mahakamani, Polisi wapeleke ushahidi wa tuhuma zao. CHADEMA ni mali ya UMMA.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
Hodi hodi @SuluhuSamia acha tuje hapohapo ili tuje tukuulize kwanini kijana wetu hutaki kumuachia? Kwanini umekuwa mtekaji? Kwanini umekuwa muoga hoja unajibu kwa bunduki? Tanzania ni Jamuhuri na Rais ni kibarua tu anayewajibika kwa wananchi wala Rais sio mfalme.
Hivi mnataka kumuua huyu mtoto kwa sababu gani ? Kwa nini mnamtesa bila sababu ? Mnamshikilia kwa kosa lipi ? Pls kama mkifanikiwa kumuua na Mimi naomba mniue .You will definitely pay the huge price one day. STUPID.
Hivi @TuliaAckson unamtoto/watoto?
If Yes, hivi ingekuwa aliyetekwa ni mtoto ako ungeongea huu utumbo unaoongea hapa?
Hivi unaelewa maumivu ambayo wanapitia familia ya @DEUSDEDITHSOKA, Jacob Mlay, Chaula na @DIONIZKIPANYA25 baada ya wapendwa wao kutekwa
Mh Rais unamuona kijana wako Abdul mlivyopendeza. Huyu kijana Soka pia ana wazazi na ndugu. Kabla haujalala leo assume hawa vijana na watu wanaotekwa ni watoto wako wa kuwazaa.
‼️SHAME❌‼️
Speaker Tulia Ackson refusee to discuss enforced disapperances in #Tanzania claiming she is not informed enough
Mi ndo maana haya mambo kutetea masuala ya gender bila qualifications huwa nakataa! Sasa tunaonekana wanawake ni makatili kwa kuzingatia ukatili wa Bi Chura Kiziwi na Rango 😫
Eniwei #TutaelewanaTu
Bunge MFU. Bunge KIBOGOYO. Bunge LIMEKEKETWA. Bunge haliwakilishi wananchi. Bunge limekuwa ni mtetezi wa Serikali. Bunge limejinasibisha na WATEKAJI. Bunge limekuwa genge la WAHUNI. Bunge linafanya kazi ya mbogamboga. RANGO hafai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji. RANGO ni MZIGO.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema leo Jumatatu Aug 19, 2024 namba ya simu ya Deusdedith Soka ambayo inashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu September 2023 imetumika kutuma ujumbe wa simu kwa Mwenyekiti wa Chama Wilaya ya Temeke wenye maudhui kuwa Deusdedith Soka ameamua kwenda nje ya Nchi sababu ndani ya Chama kuna migogoro hivyo anaondoka hadi baada ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakapokamilika na kuwa amesitisha Maandamano
ya Aug 26, 2024.
Taarifa iliyotolewa leo Aug 19,2024 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema imesema “Tunalaani kukamatwa na kuendelea kushikiliwa kwa Viongozi wa Chama Wilaya ya Temeke kinyume cha sheria , tangu jana Viongozi wa Wilaya ya Temeke ambao ni Jacob Mlay - Katibu wa Jimbo la Temeke, Deusdedith Soka - Mwenyekiti wa Bavicha, Wilaya ya Temeke, Frank Mbisa - Mwendesha Bodaboda ambao walikamatwa jana Jumapili Aug 18, 2024 wakiwa eneo la Buza, Mkoa wa Temeke na wameendelea kushikiliwa kusikojulikana na Jeshi la Polisi”
“Tunalitaka Jeshi la Polisi liwaachie mara moja bila masharti na kama wametenda kosa lolote wafikishwe mahakamani mara moja, aidha Polisi ieleze inakowashikilia ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria na mahitaji muhimu ya kibinadamu”
#MillardAyoUPDATES