#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 261
Mhe. Tundu Lissu anaendelea kusema kuwa shitaka dhidi yangu linahusiana na kauli yangu niliyoitoa Aprili 3, 2025 kuhusiana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025
Nataka nisema kwamba mimi nina uzoefu mkubwa sana na masuala ya uchaguzi wa Tanzania. Nilipiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 1985 kwenye uchaguzi mkuu nikiwa na miaka 18. Kati ya mwaka 1985 na mwaka jana (2025) nimeshiriki katika uchaguzi mkuu either kama mgombea au mpiga kura katika chaguzi zote isipokuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 na yale maafa ya mwaka jana
Watu wanacheka ๐๐๐๐๐
Mwaka 2000 sikuwepo Tanzania nilikuwa nafanya kazi Marekani na mwaka jana nilikuwa gerezani.
Waheshimiwa majaji kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 nikiwa mwanafunzi chuo kikuu cha Warwick Uingereza nilirudi Tanzania kuja kugombea Ubunge jimbo la Singida Kusini, nilisimamisha masomo ya masters.
Waheshimiwa Majaji ukiachilia ushiriki huo, nimeshiriki kwenye masuala ya kesi za Uchaguzi tangu mwaka 2005, ninaamini kabisa kwamba kwenye kesi za uchaguzi mimi ni mjuaji sana na nimjuaji kweli kweli kwasababu nimeshiriki sana kuliko Mawakili wengi wa nchi hii.
Ninaamini kuna Majaji wengi wa Mahakama hii na Mahakama ya Rufani wamejifunzia kwangu kesi za uchaguzi (wala kusema hivi sijitapi)
Waheshimiwa Majaji nje ya huo ujuzi wa kuwa wakili, kuanzia mwaka 2021 hadi nakamatwa mwaka jana nimefanya utafiti mkubwa sana kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi sio tu sheria, mfumo mzima tangu kipindi cha ukoloni, ningekuwa sipotezewi Muda Ukonga ningekuwa nimeshachapisha kitabu kuhusu mfumo wa uchaguzi wa nchi hii na uchafu wake.
Jaji Ndunguru anauliza hivi sasa ni saa kumi na moja vipi tuendelee au tuahirishe hadi Jumatatu?
Jaji Ndunguru anamuuliza wakili wa Serikali unasemaje? Anajibu kinyonge sana kuwa ndio nilikuwa naelekea huko tuahirishe hadi jumatatu.
Tundu Lissu anasema naomba nimalizie ili tuahirishe hadi Jumatatu.
Kwasababu ya uzoefu huo waheshimiwa majaji nimekuwa mstarinwa mbele kabisa kupigania mfumo mpya wa uchaguzi hapa nchini. Hakuna hoja yoyote ya uchaguzi ya CHADEMA kwa miaka hii kumi ambayo haijapitia kwenye mikono yangu. Tutaendelea jumatatu waheshimiwa majaji.
Majaji wanaahirisha kesi hadi Jumatatu saa tatu kamili asubuhi na Jaji Ndunguru anasema mshtakiwa tunaamini Jumatatu utamaliza ushahidi wako hivyo summons zitolewe kwa mashahidi
Tundu Lissu anasema hapana waheshimiwa majaji siwezi kumaliza Jumatatu bado kuna kazi.
Majaji wanahirisha kesi hadi jumatatu tarehe 24 Agosti saa tatu kamili asubuhi ambapo Tundu Lissu ataendelea kutoa ushahidi wake.
Kwa namna anavyotoa ushahidi na anavyojua vitu nadhani tumtegemee kutoa ushahidi kwa siku mbili za wiki ijayo.
Inapigwa High Courrrrrrrrrt
Majaji wanatoka sasa
Lissu anaagana na Mawakili wake na wananchi.
Wananchi kwa vibe sana wanaimba Katiba Mpyaaaaaaaaaaa
Wengine wanaitikia FreeTundu Lissu.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 260
Mhe. Tundu Lissu anaendelea kutoa ushaidi wake
Anasema nilikuwa Msemaji Mkuu wa masuala ya katiba na sheria ya kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Masuala ya Muungano na nilikuwa shadow Attorney General.
Naomba Mahakama irekodi kwamba nilifanya kazi yangu kwa uaminifu mkubwa na umahiri mkubwa sana.
Waheshimiwa majaji katika kipindi cha 2011 hadi 2014 nilikuwa mjumbe maalumu wa Bunge la Katiba kwa kipindi hicho cha 2011 hadi 2015 niliongoza harakati za kupigania Katiba Mpya na mfumo huru wa uchaguzi, niliongoza hayo mapambano bungeni na kwenye Bunge la Katiba kwa uaminifu na umahiri mkubwa sana, hivyo ni ushahidi wangu kwamba kilichotuleta hapa ni mgogoro wa kisiasa, ni vita ya kisiasa na sio Uhaini.
Waheshimiwa Majaji nje ya ubunge nimekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kuanzia Machi hadi Septemba 7, 2017 na huwi Rais wa TLS kama wewe ni mtu wa hovyo hovyo mhaini mhaini.
Nje ya uongozi wa mawakili wenzangu hapa nilipo ni Makamu Mwenyekiti wa Internationa Democrats Union (IDU).
IDU ni muungano au shirikisho linalojumuisha vyama karibu 80 kutoka dunia nzima.
Mimi pia ni mjumbe wa International Executive Committee ya IDU, mimi ni Makamu Mwenyekiti ninayewakilisha bara zima la Afrika
Waheshimiwa majaji ni ushahidi wangu kwamba mimi ni mtu wa heshima ndani ya nchi hii na kimataifa na heshima niliyonayo ni kutokana na msimamo wangu wa kupigania Demokrasia, Haki za binadamu na Utawala wa sheria sio kwasababu nyingine.
Waheshimiwa Majaji mwezi Mei 2011 nilipewa tuzo ya heshima ya kuwa mwenza wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Bridgeport (International Fellow) jimbo la Connectcut lilipo nchini Marekeni, walisema ni kwasababu ya kupigania haki za binadamu, mazingira na demokrasia katika nchi ya Tanzania na Barani Afrika.
Mwezi Desemba 2020 nilitunukiwa heshima nyingine na IDU tuzo inayoitwa Bush Thatcher Award Freedom (kwa jina la Rais wa 41 wa Marekani) sababu yake au citation yake ilisema Tundu Lissu umekuwa ni kielelezo cha msimamo thabiti wa kupigania Haki, Demokrasia na Utawala bora katika nchi za Afrika.
Ni muhimu vilevile iingie kwenye ushahidi kwamba pamoja na kukaa gerezani kwa muda wote, heshima yangu ndani na nje ya nchi haijapungua in fact imeongezeka.
Taasisi nyingi sana za kitaifa, kikanda na kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Madola zimesema haya mashtaka ni mashtaka ya kisiasa hakuna jinai yoyote na wamedai niachiliwe huru bila masharti yoyote.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limeeleza sio tu kwamba niachiwa bali nilipwe pia fidia kutokana na usumbufu wote uliojitokeza tangu nilipokamatwa.
Waheshimiwa Majaji naomba iingie kwenye ushahidi kwamba nchi za Jumuiya ya ulaya zimesimamisha misaada kwa Tanzania kwasababu ya mashtaka haya, takribani dola million 700 nchi ya Marekani imesimamisha kwa Serikali ya Tanzania kwa takwimu nilizonazo kwasababu ya mashtaka haya.
Bunge la Marekani linajadili muswaada wa kuiwekea serikali ya Tanzania na Viongozi wake vikwazo kwasababu ya mashtaka haya.
Waheshimiwa majaji dunia haiwezi ikakupigania hivi kama wewe ni mtu wa hovyo hovyo
Watu wanatabasamu sana na kucheka ๐๐๐๐๐๐
Mhe. Lissu anaendelea kusema Dunia inaweza kukupigania hivi kama wewe ni mtu wa heshima.
Part 261 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 259
Baada ya Mapumziko mafupi Tundu Lissu amepata angalau nusu saa ya kuzungumza na Mawakili na mashahidi wake ambao ni Makamu Mwenyekiti John Heche, Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa na Brenda Rupia.
Mawakili wake ambao alikuwa nao kwenye mashauriano ni Dr. Nshala Mwanasheria Mkuu wa Chama, Deogratias Mahinyila, Paul Kisabo na Edward Heche.
Inapigwa Courrrrrt
Majaji wanaingia
Mawakili wa Serikali wanasema wako tayari na Mhe. Lissu anasimama anasema Waheshimiwa majaji kabla hatujaendelea ninaomba maelekezo ya Mahakama kuhusu mashahidi wangu wa Chama maana wote wamo humu ndani je watoke nje au wabaki?
Jaji Ndunguru anajibu kuwa wanatakiwa watoke nje wataitwa wakihitajika kutoa ushahidi.
John Heche, John Mnyika , Amani Golugwa na Brenda Rupia wanatoka nje
Jaji Ndunguru anamwalika Tundu Lissu kwenda kwenye kizimba cha mashahidi maana alichokaa ni cha watuhumiwa
Tundu Lissu anahamia kizimba cha mashahidi wakati anaenda namuona anashikana mkono na dada ake na wapendwa wake huku akitabasamu, lakini akiwa anasindikizwa na maaskari magereza wa kutosha wasiopungua 8.
Jaji Ndunguru anamuuliza Lissu majina yake, umri wake miaka 59 na dini yake ni Roman Catholic
Jaji Ndunguru anamwambia tunaamini unatoa ushahidi wa kiapo?
Mhe. Lissu anajibu ndio Mhe. Jaji ila sijawahi kutoa ushahidi ingawa nimeshtakiwa mara nyingi sana ila sijawahi kufikia hatua hii
Watu wanacheka๐๐๐๐๐๐
Anaongozwa kuapa na ameapa.
Mhe. Tundu Lissu anaendelea kuhusu kazi yake amesema ni wakili na kiongozi wa kisiasa, ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.
Nilichaguliwa na kutangazwa kuwa Mwenyekii wa CHADEMA Taifa Januari 22, 2025.
Kabla ya hapo Mimi nimekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbunge wa vipindi viwili na nilishambuliwa kwa risasi Septemba 7, mwaka 2017 lakini pia nimewahi kuwa Mkurugenzi wa Sheria CHADEMA, Ex Official Member wa Chama,
Mwaka 2010 nilichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (siku hizi linaitwa Ikungi Mashariki) na nilichaguliwa kwa tiketi ya CHADEMA, na mwaka 2015 hadi 29 Juni 2019. Sasa ilikuwaje nikaishia 29 June 2019??
Nawarudisha Septemba 7, 2017 ambapo nilifuatwa kwenye makazi yangu Dodoma na kushambuliwa kwa risasi na watu ambao Serikali ya Tanzania inawaita watu wasiojulikana.
Waheshimiwa majaji nilikimbizwa kwa ndege hadi Nairobi hospital hadi Tarehe 4 Januari 2018 na baada ya hapo nilipelekwa Ubeligiji kwa Matibabu zaidi katika hospital ya chuo kikuu cha Leuven. Nilitibiwa hadi Januari 2022.
Kati ya Nairobi na Leuven nilifanyiwa operation 25 (operation 17 Nairobi Hospital, 8 Leuven). Waheshimiwa majaji mkiona navuta mguu ni kwasababu ya matukio hayo.
Nikiwa hospital tarehe 29 June 2019 aliyekuwa Spika wa Bunge Job Ndugai (marehemu sasa) alinifuta ubunge kwasababu alisema nilikuwa mtoro, alikuwa hajui niliko.
Licha ya kuwa Mbunge na kuumizwa vibaya sana nikiwa kazini Bungeni, Bunge na Serikali ya Tanzania ilikataa kulipa gharama ya matibabu yangu, sikupewa hata senti moja, licha ya Sheria ya Bunge inayosema kwamba mbunge akiugua atatibiwa kwa gharama za bunge lakini mimi kwangu walikataa katakata kabisa.
Nikiwa Bungeni kipindi chote nilikuwa Mnadhimu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni yaani ni kiongozi wa pili kwa viongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.
Part 260 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 258
Anasimama wakili wa serikali na kuomba ahirisho kwaajili ya health break au tuahirishe hadi jumatatu.
Anasimama Tundu Lissu anasema mimi nina wasiwasi sana na ahirisho maana gerezani sio sheraton hotel, hivyo naomba tupate muda wa health break nifanye consultatikns na mashahidi wangu then tuendelee.
Jaji Ndunguru anatamka kuwa Mahakama inaahirisha kesi hadi saa tisa na nusu, Mahakama inaruhusu ufanye consultations na mashahidi wako bila kuathiri taratibu zingine za kiusalama hivyo Mahakama inaangalia sehemu ya kufanyia consultations.
Inapigwa High Courrrt
So tukutane hapa saa tisa na nusu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 257
Mhe. Lissu anaendelea kujibu pingamizi la Wakili wa Serikali.
Tatu, Waheshimiwa majaji naomba msimamie maamuzi yenu, mlitaka niwatajie majina na niliwatajia mkaandika sasa imefika wakati wa kutekeleza hicho mlichokiandika.
Mashahidi wangu ni watu wakubwa sana ndio, lakini kwa nafasi zao ndio wanaohusika na masuala hayo.
Kwenye sheria za nchi hii watuhumiwa wa makosa ya jinai wana haki ya kutendewa fair trial, Fair trial ni pamoja na haki ya kuwezeshwa na Mahakama mashahidi kuitwa, msipowaita kwasababu ya hofu za Mawakili wa Serikali hakutakuwa na fair trial. Na kama hakuna fair trial God knows. Kwahiyo lindeni right to fair trial, nimemaliza waheshimiwa majaji.
Wakili wa Serikali Katuga amesimama na kuanza kujibu hoja za Lissu kuwa sisi Jamhuri tumeialika Mahakama kuangalia kifungu cha 314 na 281 cha CPA.
Sisi msisitizo wetu ni kuwa mashahidi waliotajwa leo hawakutajwa kwenye committal.
Records zinaonyesha hawakutajwa, mahakama ipo kwaajili ya kutafsiri sheria na sio kwa huruma, Lissu aliitishia Mahakama, Katuga anaongea kwa dharau sana kama vile sio afisa wa Mahakama, ni kama mtu asiye na malezi kutoka kwenye familia.
Watu wanamsonya katuga sana, Jaji Ndunguru anasema tulieni jamani.๐
Mhe. Lissu anasimama na kusema wakili Katuga hajibu hoja zangu, hayo maneno kuwa nionewe huruma, kuitisha Mahakama naomba yaondolewe kwenye records otherwise nitaomba kumjibu.
Jaji Ndunguru anatoa mwongozo kuwa jamani tulieni anayeshindwa kuhimili mihemuko bora akae nje naongea kwa mara ya mwisho tutawachukulia watu hatua.
Katuga anaendelea kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 281 kuna hatua mshtakiwa alitakiwa kuchukua kama mashahidi wake hawakutajwa. Mashahidi kutajwa wakati wa Preliminary hearing (PH) sio takwa la kifungu cha 281. Hatukupinga wakati wa PH kwasababu tulisubili wakagi huu.
Lissu alisema msikane maamuzi yenu, tumeangalia records inaonyesha hakukuwa na amri ya Mahakama isipokuwa kulikuwa na orodha tu ambayo aliita ya mashahidi.
Sisi msimamo wetu ni kuwa hao mashahidi anaowataka wa serikali tuomba mahakama itumie mamlaka yake kuwa ushahidi wa mashahidi hawa sio muhimu kwasabau suala la kutishika au kutokutishika is immaterial kwenye kesi hii
Waheshimiwa majaji waliotajwa kama vile DG wa TISS, CDF na IGP sisi Jamhuri tunasema ushahidi wao umeshatolewa na wasaidizi wao kwasababu kauli za mshtakiwa zililenga kuvunja amani.
Mhe. Lissu anasimama na kusema nitaomba nijibu hilo la kuwa kauli zililenga kuvunja amani kwasababu hilo ni kosa tofauti kabisa.
Katuga anajitetea kuwa maana yetu ni ushahidi wao umeshatolewa hivyo nao wakiitwa itakuwa ni sawa na kuwauliza maswali ya Dodoso dhidi ya ushahidi uliokwishatolewa tayari.
Waheshimiwa majaii mahakama ikitoa summons ya witness kwa mujibu wa kifungu cha 145 na 146 cha CPA na enforceability yake haitekelezeki. Lissu alitaja kesi ya Mahalu kisutu kuwa the late President Mkapa alienda kutoa ushahidi, huo ulikuwa ni utashi wa Mkapa mwenyewe. Hatujaelezwa kama mahakama iliangalia relevance ya ushahidi wake kwahiyo mahakama haiwezi kuiga.
Sisi tunasema kwakuwa hukuwataja wakati wa committal? Mahakama ina descretion ya kuwaita au vinginevyo. Tunaomba vifungu vilivyotumika kuipiga kesi ya Jamhuri huko nyuma basi walau na sasa vitumike. Katuka amemaliza na kumuita Mwinuka aendelee
Wakili Mwinuka sijui mwinuko anasimamama na kusema kuwa Lissu alisema kifungu cha 9 na cha 10 cha Presidential Affairs Act vinaweza kusomwa kwa pamoja. Sisi tunasema haviwezi kusomwa kwa pamoja kama alivyosema Lissu. Sisi tunaona kwamba Mahakama haiwezi kumtumia wito Rais. Ni hayo tu, waheshimiwa majaji.
Baada ya mawasilisho ya pande zote mbili majaji wamechukua muda kadhaa kujadiliana ni zaidi ya dakika 20 wametumia. Kiongozi wa jopo Mhe. Jaji Dunstan Ndunguru anayeongoza jopo anafanya consultations na wenzake Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.
Part 258 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 256
Anaendelea Mhe. Lissu
Waheshimiwa majaji kwa mujibu wa kifungu cha 192 cha CPA mahakama inaweza kukitumia kuamuru proceedings to be held in camera kama ushahidi utakuwa ni prejudicial to the public interest. Huo ndio utaratibu uliotumika hata kwenye kesi ya Mataka na Hatibu Ghandi
Kuna hoja imeletwa na wakili wa serikali Katuga kuwa eti mashahidi wa jamhuri wametoa ushahidi kwaniaba ya Serikali kwasababu tu ni watumishi wa serikali, hoja hii haina msingi wowote wa kisheria au kimantiki.
Kama ingekuwa ni kweli kwamba wafanyakazi wa serikali wakitoa ushahidi wanatoa kwaniaba ya serikali, simply sheria ingesema hivyo. Hii dhana kwamba watumishi wa umma wakitoa ushahidi ni kwamba Rais anakuwa ametoa, maana yake ni nini?
Wakili wa Serikali Katuga amesema mara kwasababu watumishi wa serikali wametoa ushahidi Rais hatakiwi kutoa ushahidi, Mara anasema Rais hawezi kutoa ushahidi, so which is which?
Mahakama kicheko๐๐๐
Mhe. Lissu anaendelea kusema kuwa hao mashahidi na viongozi wa serikali wanakuja kutoa ushahidi kama wajumbe wa Baraza la Usalama wa Taifa na hawaji hapa kama wateule wa Rais bali kama Wakuu wa hivyo vyombo
Mkuu wa Jeshi la Polisi atatoa ushahidi kama mtu ambae jeshi lake limenikamata na mjumbe wa sekretarieti ya Baraza la usalama wa Taifa.
Majaji Katuga anasema msiite mashahidi blindly kuna siku atamuita Samia Mungu na Rais sio Mungu hivyo anaweza kuja kutoa ushahidi, kama nyie mawakili wa Serikali mnadhani Rais ni Mungu kama alivosema yule Profesa basi ni nyie na sio sisi.
Marehemu Rais Mkapa alitoa ushahidi kwenye kesi ya Costa Mahalu kama Mkapa alitoa ushahidi kama Rais kwanini MPANGO asije.??
Katuga anasimama tena anasema waheshimiwa majaji Lissu analeta vitu vipya kama hivyo vya Mkapa basi na sisi tupewe haki ya kujibu
Mhe. Lissu anasema wewe huna unachokielewa. Mimi najibu pingamizi lako na wewe kama unataka kufanya rejoinder utaomba nafasi.
Katuga anasimana anasema wewe ndio huelewi.
Mhe. Lissu anamuuliza Katuga nyie mnasoma sheria wapi?
Jaji Ndunguru anamwambia Katuga babu tulia, mwenzako amalize na nyie mtakuja kujibu anachoongea Lissu.
Watu wanacheka ๐๐๐
Mhe, Lissu anaendelea kuwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, hakuna utaratibu wa kutoa ushahidi kwa niaba ya mtu mwingine, hakuna utaratibu wa ushahidi wa Rais kutolewa na mtu mwingine kwaniaba ya Rais. Hivyo hakuna vicarious testmony katika sheria za Tanzania. Ushahidi wa Mapolisi akina Amin Mahamba na wengine ulikuwa wao personally na sio kwaniaba ya mtu mwingine.
Kuna kesi wakili Mrema wa serikali aliitaja hapa (kesi ya Jacobo) inahusu mahakimu, sasa nyie ni majaji yeye ameleta kesi ya mahakimu , nyie inawahusu nini?
Watu wanacheka๐๐๐๐๐
Mhe. Lissu anaendelea, kanuni iliyopo kwenye hiyo kesi ni kuwa hakimu anaweza kukataa ushahidi ambao hauna uhusiano na kesi husika. Sasa swali kwenu waheshimiwa majaji mashahidi na viongozi wa serikali ushahidi wao hauna uhusiano na kesi ya uhaini????
Hii ndio hoja ya mawakili wakuu wa serikali. Kesi ya Jacob haina uhusiano na kesi hii, sababu mashahidi niliowataja wana uhusiano wa moja kwa moja na kesi hii.
Kuna hoja aliisema wakili Mrema eti nataka taarifa, jibu langu ni jepesi tu kuwa nataka ushahidi na sio taarifa kama kweli kuna kesi ya uhaini hapa na sio ya kutunga tunga kama alivyosema JajiChande kwenye ripoti yake.
Waheshimiwa majaji naomba nimalizie kuwa hakuna sheria inayozuia mashahidi kupelekewa summons hata Rais anaweza kupelekewa summons akikataa ni jambo jingine
Pili ushahidi wao ni muhimu katika kesi hii, kama kweli kulikuwa na hayo matishio yanayodaiwa Rais, Makamu na Waziri Mkuu lazima wawe wanajua.
Part 257 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako,
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 255
Anaendelea Mhe. Lissu
Hoja imeletwa hapa ya kipumbavu kwamba kuna mashahidi ambao hawawezi kulazimishwa kuja mahakamani. Hawawezi kuwa compelled kuja mahakamani.
Who is a compellable witness? Utaratibu huo upo kwenye sheria ya ushahidi sect. 135 kwamba mashahidi wote ni compellable.
Kifungu cha 9 cha Presidential Act kinasema kama kuna haja anapelekewa kupitia kqa Katibu Mkuu Kiongozi au Personal Secretary wa Rais na kumuomba huyo Katibu Mkuu aisaidie Mahakama kumfikishia Rais hiyo summons.
Halafu yeye, huyo Rais ataamua aheshimu wito wa Mahakama au asiuheshimu. Maamuzi ni yake.
Section 10 ya Presidential Affairs Act inapaswa kusomwa pamoja na kifungu walichosema cha 9.
Katuga anasema msiite mashahidi ambao hawawezi kuja. Ni sawa na kusema kuwa mawakili wa serikali wanasema msiwaite kwasababu hawatakuja, kwamba Samia hatokuja.
Wakili wa serikali Katuga amesimama kupinga hayo maneno ya Lissu, na anasema hiyo itakuwa contempt kwa mahakama,
Mahakama nzima imenongโona huyu wakili wa serikali, watu ni Kama wanamshangaa huyu jamaa vipi ๐๐๐
Mhe. Lissu anasema hawa mawakili wa serikali nimewasikiliza kwa zaidi ya mwaka nina wasiwasi kama wanajua maana ya contempt.
Jaji Ndunguru anatoa muongozo kwa Katuga kuwa hiyo ni tafsiri ya Lissu hatuwezi kumzuia kutafsiri mlichokisema hivyo kaa Katuga.
Mhe. Lissu anaendelea kuwa hawa mawakili wa serikali wanaanza kuwasemea mashahidi kuwa hawatakuja, kwanini wanawajibia??
Hiki Kiherehere hiki wamekitoa wapi? Hoja kwamba mkiwaita hawawezi kuja ni ya hovyo. Muwaandikieni tuone.
Sasa hiyo inamuhusu Samia, sasa vipi kuhusu Philip Mpango nae? Majaliwa je? Nao wana tatizo si wastafu hao?
Kwa taarifa zangu ni Emmanuel Nchimbi na Mwigulu Nchemba ndio wako ofisini sasa hawa wa Mwaka jana hawako ofisini, hawamsaidii Rais sasa hivi.
Na vipi kuhusu IGP? DCI? na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa je?
Kwenye hoja hii hakuna mtu yeyote wala afisa yeyote ambae hawezi kupelekewa summons sio Rais sio Makamu wa Rais Mstaafu na mkuu wa Majeshi na wote niliowataja. Wote hao they are subject to court process.
Sasa mmeambiwa mashahidi hawa hawana ushahidi mzito au ushahidi wao hauna umuhimu wowote kwenye kesi hii, Waheshimiwa majaji, mtu ambaye kosa linamlenga kama Rais inawezekanaje ushahidi wake usiwe relevant? Unapomzungumza Rais ndio serikali kwa mujibu wa ibara ya 151 ya Katiba.
Ninachokiona hapa ni jitihada kuwa Rais yuko juu ya Sheria, asionekane ameenda Mahakamani. Jaji Mkuu mstaafu Barnabasi Samata aliwahi kusema kwamba dhana tu kuwa Rais yuko juu ya sheria inakiuka Katiba. Kwa nature ya kosa la uhaini na kutengeneza nia ya kuitishia serikali, Rais anawezaje asiwe na ushahidi ambao ni relevant???
Rais ambae ni Chief Executive wa Serikali na ni serikali ana ushahidi relevant wa kosa la uhaini la kutengeneza nia ya kuitishia serikali yake.
Mhe. Lissu anaendelea kumwaga madini
Anasema kuwa Rais ni Mwenyekiti wa National Security Council, wajumbe wake ni DGIS, IGP, Mkuu wa Majeshi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu. Hawa watu wote ushahidi wao unaachaje kuwa relevant? Ni namna tu ya kutaka hawa wasije kutoa ushahidi.
Waheshimiwa majaji ni kweli kuwa hamuwezi kutoa arrest warrant kwa Rais, lakini hiyo haina maana kuwa hamuwezi kutoa summons kwa Rais. Makamu wa Rais, Waziri Mkuu Mstaafu, IGP, DG wa TISS, Mkuu wa Majeshi wakikataa kuja kutoa ushahidi wanapelekewa polisi na amri ya Mahakama waje waeleze kwanini wasishughulikiwe??
Mahakama kicheko๐๐๐๐๐๐
Part 256 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 254
Anasimama Wakili wa Serikali Ignas Mwinuka anasema Presidential Affairs Act kifungu cha 9 kinasema wito wa summons maana yake unamlazimisha shahidi kufika.
Kifungu hicho cha 9 kinasema anakisoma. Kwahiyo kwa mujibu wa kifungu hiki Mahakama haina mamlaka kutoa wito wa ku compell Rais kufika Mahakamani.
Naomba kuwasilisha.
Anasimama Wakili mwingine wa Serikali Job Mrema nae, anasema naomba kuunga mkono hoja.
Jaji Ndunguru : achana na mambo ya kuunga mkono hoja, Nenda kwenye hoja
Mrema anasema Section 24 ya TISS CAP 406 kinasema kuhusu protection of source of information.
Yaani usiri wa taarifa kwa kuzingatia mshitakiwa ametaja baadhi ya mashahidi mfano DGIS yaani Mkuu wa Usalama wa Taifa aje hapa Mahakamani. Anataka kupata taarifa kwa mashahidi hawa ili apate kujitetea.
Sasa kwa cheo cha shahidi huyu anafungwa na masharti ya sheria hii hata akija hapa hataweza kusema kila kitu. Na sio sahihi kabisa. Kuna limitation kwa mujibu wa sheria.
Kifungu hicho kimeweka penal sanctions yaani kutoa ushahidi huo ni kosa kubwa la kisheria.
๐๐ Lissu alisema mmeyataka mtayapata. Ngoja tuendelee.
Job Mrema anaendelea kusema naomba kufanya marejeo kwenye shauri la criminal appeal Jacob Tiifunga vs Republic Criminal Appeal No. 185/1980. HC Tanzania at mwanza. TLR.
Mahakama ilisema a trial magistrate has descretion to call witness yaani Mahakama ina uwezo wa kukataa shahidi kuitwa. Lakini kwa mujibu wa msingi uliotengenezwa kwenye kesi hii ni kuweka sababu. Sasa sisi tunasema sababu tulizotoa kuanzia shahidi namba moja SAMIA hadi namba 7 mashahidi wasiitwe kwenye shauri hili kwa sababu tulizozieleza na ni hoja yetu kuwa mnayo mamlaka ya kukataaa. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama anacho cha kusema
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji kabla sijaanza naomba kidogo kufanya consultation na Mawakili wangu kabla sijaanza, 5 minutes its enough...
Mawakili wa Lissu wakiongozwa na Dr. Nshala, Jebra, Matata, Paul Kisabo, Deogratias Mahinyila, Madeleka namuona Wakili Kisabo amesimama akimuonyesha Mhe. Lissu sheria kwenye laptop, Lissu anasoma na wanaendelea kujadiliana.
Wamemaliza kujadiliana
Mhe. Lissu anasema
Kuhusu hoja ya mimi kuwataja mashahidi wangu ninaotegemea kuwatumia kwenye kesi hii. Katuga amesema hoja hii na ukweli ni kwamba toka Kisutu hoja hii ilikuwa na shida.
Mgogoro specific ni kwamba Hakimu Mkuu Mkazi Franco Kiswaga baada ya mtuhumiwa kumwambia kuwa ana mashahidi na kuanza kuwataja akakataa kuwarekodi hao mashahdi.
Na hoja yake ilikuwa ni hao utaenda kuwataja Mahakama kuu. Mimi siandiki utaenda kuwataja Mahakama Kuu.
Baada ya shauri kuletwa hapa Mahakama Kuu Waheshimiwa Majaji nilileta hoja kwamba utaratibu mzima wa committal proceddings ulivurugwa kwa makusudi na nikawaambia majina ya mashahidi wangu wa utetezi yalikataliwa.
Nililileta mbele yenu na mkasema wenyewe kuwa utakapofika wakati wa kujitetea utaapata fursa ya kuandaa utetezi wako. Na mkasema niawatajie majina mnaotaka niwaite.
Nikawatajia na Mkaandika kwenye rekodi.
Katuga akasema ukurasa wa 186 wa proceedings orodha ipo na mliwaandika wenyewe Majaji.
Jambo hili sio la leo. Lipo kwenye rekodi za Mahakama hii, anachotaka Katuga mfanye ni mjikane wenyewe.
Anataka mjioneshe kuwa hamna akili sasa hiyo ni juu yenu sio kwasababu majina ya mashahidi hayajawahi kutajwa.
Yalitajwa Kisutu, yakatajwa kwenu na leo nimerudia tena.
Amueni mtanipa haki hiyo ya kupata mashahidi au mjikane.??
Mimi napendekeza msijikane, msikubali huo mwaliko wa kujikana. Vinginevyo kosa kubwa kuliko zote Mahakama hii itathibitisha kuwa haina uwezo wa kutenda haki tena kwenye Kesi ambayo adhabu yake ni kifo, mtaonesha kuwa hamna uwezo wa kutenda Haki na mtageuzwa Kangaroo Court. A court of star Chamber Court.
Hoja ya kifungu cha 281 na 314(2) mlishaandika majina ya mashahidi last year. Has already been taken by your own order.
Part 255 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 253
Hii nchi ina maajabu sana.๐คง
Wakili wa Serikali Katuga amesimama anasema kwa mujibu wa kifungu cha 313 na 381 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai vyote vinasema mashahidi wa mshitakiwa au mtuhumiwa wanapaswa kutajwa kipindi cha committal yaani kule Kisutu.
Watu wanacheka.๐๐๐๐
Watanzania wanakumbuka Mh. Lissu aliwataja mashahidi wake kule Kisutu na wote tulisikia. Leo Katuga anasimama hapa anasema Mshitakiwa au mtuhumiwa hakumtaja Samia, Majaliwa na hao wengine kule Kisutu.
Katuga anasema pia tunaitaka Mahakama iangalie mashahidi wanaoitwa wanahusika na hii kesi?
Jaji: Sasa usiende huko tuambie kwanza mashahidi ambao hutaki waje ni akina nani?
Katuga: Ni mashahidi wote kabisa.
Relevance ya mashahidi lazima aiseme ni ipi?
Lakini kipekee tunapinga mashahidi wanaotoka Serikalini na nitaeleza kwanini?
Watu wanacheka na kushangaaa nini kinatokea? ๐๐๐
Pale Mahakama itakapotoa wito kwa mujibu wa kifungu cha 146 cha kutoa wito basi kinaelekeza mahakama kutoa hati ya UKAMATAJI. Kutokana na mazingira haya Mahakama haiwezi kutoa hati ya wito bila kujiridhisha kama shahidi huyo ni muhimu, compellable na competent.
Mahakama inapaswa kujiridhisha hivyo vitu vyote, haiwezi kumuita mtu ambae yuko aware na fact in issue lazima awe anajua kinachoendelea.
Mahakama haiwezi kutoa wito ambao haiwezi kuenforce sasa Rais hajaja Mahakamani itatoa arrest warrant?
Haya ni maneno ya Katuga.
Anaendelea hapa naomba niende kwa mashahidi watatu wa mwanzo, Samia Suluhu, Philip Mpango na Kassim Majaliwa kama tumemuelewa mshitakiwa kuwa hawa ni Viongozi wa Serikali anaotuhumiwa kuwatishia. Ibara ya 43 ya Katiba. Rais atakuwa Mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu.
Ibara ya 47 ya Katiba inasema Makamu wa Rais atafanya kazi zote za Rais kama hayupo nchini au atakazoagizwa na Rais.
๐๐๐๐ Yaani Jamhuri wamemshtaki Mhe. Lissu kwa Uhaini halafu wanaweka mpira kwapani hawataki kuja kutoa ushahidi
Katuga anaendelea
Mashtaka yetu ni kuwa mshtakiwa ametengeneza nia ya kuitishia Serikali regardless kama serikali imetishika au haijatishika na mashahidi wetu 17 walitoa ushahdi kwaniaba ya serikali, kwa maneno mengine Rais ameshatoa ushahidi
Watu wanacheka๐๐๐๐๐
Kama mshtakiwa anamalengo kuwa mashahidi waje waeleze kama walitishika au hawakutishika ushahidi huo sio wa muhimu hapa kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Ushahidi wa mashahidi anaotaka kuwaita Lissu sio material, pia sio lazima kuwaita mashahidi hawa kwasababu ni descretion ya Mahakama. Kwa namna Lissu alivyosema waitwe, ni kama anataka kuja kuwauliza maswali ya Dodoso dhidi ya ushahidi uliotolewa na mashahidi wa serikali ambao wameshatoa ushahidi kwaniaba yao kinyume na malengo ya kifungu cha 155 na 156 ya Sheria ya Ushahidi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 209 Mshtakiwa anaweza kuomba Mahakama iite shahidi kama ushahidi wake ni wa muhimu kuisaidia Mahakama.
Sisi tunaona kuwa Lissu amekiuka vifungu vya sheria na hawa mashahidi sio material na hivyo mashahidi waliotajwa kuanzia namba moja hadi 7 tunaomba wasiitwe, hao wengine wa CHADEMA hatuna shida nao ila utaratibu ufuatwe. Ni hayo tu naomba kuwaalika wenzangu.
Part 254 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 252
Jaji Ndunguru anaendelea kusoma uamuzi.
Mahakama hii baada ya kupitia hoja za pande zote mbili Mahakama inajiuliza je jamhuri kwa ushahidi wao kama wame establish endapo kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au lah
Hakuna ubishi kuwa maneno hayo yalitamkwa kwenye Mkutano na mbele ya vyombo vya habari na ushahidi unamzungumza, mshtakiwa na shahidi wa 17 alieleza kuwa maneno hayo yalitolewa na mshtakiwa na yeye alikuwepo na mbele ya watu wengine.
Hivyo Mahakama hii haingalii uzito au kuaminika kwa ushahidi, na kwasasa mahakama hii imeona kuwa kuna kesi imekuwa established na hivyo Mshtakiwa ana kesi ya kujibu dhidi ya ushahidi ulioletwa na upande wa mashtaka.
Jaji Ndunguru anaeleza zaidi kuwa Mshtakiwa ana haki kwa mujibu wa kifungu cha 312 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jiani , ana haki ya kutoa ushahidi wake mwenyewe; haki ya pili ni kuita mashahidi wake au pia mshtakiwa ana haki ya kukaa kimya.
Mhe. Lissu anasimama na kueleza kuwa nitajitetea mimi mwenyewe kama shahidi wa kwanza, nitaita wafuatao ambao Mahakama naomba iwapelekee summons;
1. Samia Suluhu Hassan (popote alipo apelekewe summons) maana ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama wa Taifa tunataka tujue kama wana taarifa za uhaini unaodaiwa.
2. Philip Isdor Mpando mwaka jana alikuwa Makamu wa Rais na Mjumbe wa Baraza la Usalama wa Taifa naamini anaushahidi kuwa haya maneno ni ya kutunga tunga tu.
3. Kassim Majaliwa ambaye wakati matukio haya yanatokea alikuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa shughuli za serikai na mjumbe wa Baraza la Usalama wa Taifa;
4. IGP Camillius Wambura na Mjumbe wa Sekretariati wa Baraza la Usalama wa Taifa,
5. General John Mkunda Mkuu wa Majeshi na mjumbe wa sekretariati ya national security counsel,
6. DG wa Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi (Mkuu wa TISS) tunataka DG aje aseme kama hili kosa kubwa katika Jamhuri ya Muungano lilifanyika au maneno tu,
7. DCI Ramadhani Kingai nataka aje anitetee maana alitajwa tajwa na mapolisi mashahidi
Naona sasa Lissu anaihamishia serikali Mahakamani.๐๐๐
Wengine waheshimiwa majaji naomba wafuatao pia wapelekewe summons
8. John Mnyika, katibu mkuu wa CHADEMA,
9. Amani Sam Golugwa huyu ni naibu katibu mkuu wa CHADEMA,
10. John Heche Makamu Mkt CHADEMA na vilevile alikuwepo kwenye mkutano wenyewe ni shahidi wa kuona na kusikia;
11. Brenda Rupia ushahidi ulitolewa hapa na watu wa jambo tv kuwa ndiye aliyealika waandishi, hawa ndio mashahidi wa kuanzia ila kukiwa na haja ya kuongeza nitawaomba mniruhusu niongeze mashahidi.
Kabla sijakaa naomba niongeze jambo hapa kuwa nimekuwa na matatizo makubwa sana ya mimi kukutana na Mawakili wangu na mashahdii wangu; hawa viongozi wa CHADEMA niliowataja tangu Novemba mwaka 2025 wamepigwa marufuku kunitembelea gerezani.
Hili suala Waheshimiwa Majaji nililileta kwenu mapema sana na mliniahidi kuwa wakati ukifika nitapata nafasi ya kuonana na kuzungumza nao, hivyo naomba mtoe amri kuwa mazungumzo yangu na mashahidi wangu yasisikilizwe na watu baki , watu baki ni maafisa Magereza na watu wote wa Serikali tofauti na hapo hii itakuwa sio Mahakama itakuwa ni kangaroo court.
Waheshimiwa majaji naomba mtoe amri hiyo vingenevyo hii habari ya fair trial vinginevyo itakuwa ni maneno tu.
Mhe. Lissu anasema niko tayari kuanza utetezi wangu kwa muda ambao na nyie mtakuwa tayari
Mahakama imepoa sana kiukweli baada ya uamuzi, huzuni imetawala hapa ndani ya chumba cha Mahakama.
Part 253 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 21, 2026
Last time tuliishia part 250 so leo tunaendelea na -;
Part 251.
Majira ya 09:50 Mhe. Lissu anaingia Mahakamani kwa vibe sana kama kawaida yake, ameuliza kwa huku anacheka anasema mbona leo humu ndani pamejaa sana???
Watu wanaitika kwa kicheko cha furaha๐
Mhe. Lissu anasalimia kama ambavyo huwa anasalimia siku zote ๐ช mara inapigwa
High Cooooooooooort ya kikakamavu.
Majaji wanaingia na kuketi kwenye maeneo yao.
Karani anaita kesi ya uhaini namba 19605 ya Mwaka 2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu
Wakili wa Mkuu Serikali anasimama na kutambulisha jopo lake anaongea sauti ya chini sana, leo Katuga ni junior kuna senior wake wa kike anaongoza jopo na anasema wako tayari kupokea uamuzi.
Jaji anasema Mshtakiwa?
Mhe. Lissu anasimama na kusema, Waheshimiwa Majaji mimi niko tayari
Tunasubili majaji wasome uamuzi wao.
Jaji Ndunguru anaanza kusoma uamuzi kama Mhe. Lissu anakesi ya kujibu au la!
Mshtakiwa anashtakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na kifungu namba 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu.
Jamhuri wameeleza kwenye hati ya mashtaka kuwa April 3, 2025 akiwa mwenye utiifu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitengeneza nia ya kutenda kosa la jinai na alitamka na kuchapisha maneno yafuatayoโฆโฆโฆ. hapa Jaji amerudia maneno ya kukinukisha kama yalivyo kwenye hati ya mashtaka.
Upande wa mashtaka uliita mashahidi 17: DCP George, Insp Kaaya, Insp Elibariki, Shahidi wa kificho ni P4 na P5, P7 na P8, Asp Geofrey, P4, P7, P3, P9, DC Amani, ACP Mahamba na shahidi wa 17 alikuwa ni P. Namba P zote ni mashahidi wa kificho.
Mashahidi wote wa Jamhuri walieleza kuwa mshtakiwa alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi kwa nia ya kuitisha Serikali.
Baadhi ya mashahidi wa kificho walieleza namna walivyohamasika na maneno ya Lissu ya Aprili 03, 2025. Shahidi wa 17 alieleza kuwa alikuwepo siku ya Mkutano siku maneno yalipotamkwa.
Jamhuri walifunga ushahidi wao na Mahakama iliandika kuwa Jamhuri wamefunga ushahidi na Jamhuri walionyesha nia ya kujibu kueleza kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu na Mshtakiwa alikuwa wa kwanza kutoa hoja zake kuwa hana kesi kabisa ya kujibu
Mshtakiwa alikanusha kabisa kuwa hakuna kesi ya kujibu na aliielekeza Mahakama katika kanuni na maamuzi mbalimbali kama vile shauri la Rabat Vs Jamhuri ya mwaka 1937, Mrimi vs Jamhuri ya mwaka 1967 na kesi nyingine zilizoandikwa au kutumiwa na Mahakama.
Jaji anaeleza kuwa hata Jamhuri walikubaliana na kanuni hizo na Mahakama inaunga mkono kanuni hizo.
Kimsingi kanuni inasema kwamba Mahakama inapaswa kujielekeza kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka endapo hautajibiwa na mshtakiwa unatosha kumtia hatiani mshtakiwa?
Mahakama ilijielekeza kwenye kesi ya DPP dhidi ya Morgan, Mahakama ilieleza kuwa katika kutoa uamuzi wake Mahakama ilieleza kuwa je ushahidi uliotolewa unaweza kujenga kosa au hata kosa dogo linalotokana na kosa kubwa ambalo mshtakiwa anashtakiwa nalo???
Mahakama iliangalia pia kesi ya Ntonda dhidi ya DPP ambapo Mahakama iliamua kuwa Mahakama inatakiwa ione connection ya ushahidi uliotolewa bila kwenda kwa undani kabisa
Mahakama pamoja na maamuzi ambayo mshtakiwa aliiambia Mahakama, alitaja kesi nyingi za kutoka Kenya ambazo zinaeleza nini Mahakama inapaswa kuzingatia kabla ya kutoa uamuzi.
Part 252 itaendelea kwenye post inafuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 250.
Anaendelea Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji tuliattempt kuitoa hiyo video lakini by technicalities haikupokelewa,
Kuna aina tatu za ushahidi, ushadi wa maneno wa maandishi na maneno na (nimesahau kidogo mtanikumbusha) in the absence of evidence video that doesn't means all evidence collapse.
๐๐๐๐ Kwahiyo hapa Jamhuri inataka Mahakama iamini maneno tu, halafu Katuga ni mkavu hata aibu haoni, Mawakili wenzake wameinamisha vichwa vyao chini maana submission ya No case to answer aliyofanya Mhe.Lissu imewavuruga sana.
Haya tuendelee
Katuga anasema Ushahidi wa maneno ni sahihi kama unaaminika kutumiwa bila kutumia documentary evidence...haya si maneno yangu yapo Kwenye case ya Abas Kondo Gelbe Vs Jamhuri , CAT 472/2017, Tanzlii 12/08/2020
Kitu kizuri zaidi, kwenye case ya Goodluck Kiyando vs Jamhuri, No. 118/2013 inasema kuwa kila shahidi ana haki ya kuaminiwa, haisemi mpaka uwe na documentary evidence.
Pw1 alisema ni mtuhumiwa aliyechapisha kupitia Jambo Tv, pia Pw17 alisema kupitia sisi wewe ndiyo ulichapisha.
Waheshimiwa majaji kupitia hoja hizi mashahidi wanasema kupitia kitendo cha kuongea na vyombo vya habari, kitendo kilikusudia maneno yako (mtuhumiwa) yaufikie umma ili umma uchocheke.
Umma ni kina nani? Kifungu cha tano cha Kanuni ya Adhabu ya sheria iliyotumika kumshtaki mtuhumiwa
Tumezungumza Publication, Publication ...Publication ni kitu gani? Black Law dictionary inatafsiri nini maana ya kutangaza, taking into account that it was live streaming
Hivyo kupitia viini vyote vya Uhaini Jamhuri imevithibitisha hivyo tunaona mtuhumiwa anapaswa kupewa nafasi ya kujitetea kutokana na mazingira ya kesi yake.
Pw1 anasema Mtuhumiwa wakati anahojiwa alisema maelezo yake/ ushahidi wake atakuja kuutolea Mahakamani,
hivyo kwakuwa Jamhuri imethibitisha viini vya kosa tunaona ni haki ya mshtakiwa kujitetea kwa mujibu wa kifungu cha 312 (1) cha sheria ya makosa ya jinai.
Kwa upande wetu ni hayo tu waheshimiwa majaji tunaomba kuwasilisha.
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema, Hoja zilizotolewa ni nyingi na mashahidi ni wengi hivyo tunaomba tupate muda wa kupitia na kutolea uamuzi, kesi inahairishwa mpaka tarehe 21/08/2026
Saa tatu kamili asubuhi.
Imepigwa High Cooooourt
Majaji wanatoka pamoja,
Mawakili wa serikali wananyanyuka
Mhe Lissu anamalizia kupanga vitabu na sheria zake huku akisemezana na viongozi wenzake wa chama.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 249
Wakili wa Serikali Katuga anasema pia case ya DPP MorganMalk vs 2013 ambapo ilisema Mahakama ya rufani iliendelea mbele kwa kuifafanua hii principle ya primafacie case kwa kuangalia ushahidi uliotolewa, unajitosheleza kumtia hatiani mshtakiwa kwenye shtaka dogo au kosa analoshtakiwa nalo, ukiangalia kiini cha kosa kwenye mashtaka
Je mshtakiwa ni mwenye utii?
Je mtuhumiwa alitengeneza nia?
Je alidhihirisha nia yake kwa kufanya kitendo?
Waheshimiwa majaji, viini vya kosa ya uhaini vilishaainishwa kwenye case Grey Likungi Matata , elements zilizoainishwa ni kama zile alizoanisha mtuhumiwa tofauti ya viini ni kidogo ukilingqnisha na mazingira ya kosa
Aina ya kwanza, mshtakiwa awe mwenye utii, ya pili mshtakiwa awe ameonyesha nia, ya tatu amedhihirisha nia yake kwa kuchapisha.
Kiini cha tatu cha kudhihirisha kina utofauti kidogo kwakuwa kimechaguliwa kimoja cha kufanya, imebaki na manifestation of deed, kwahiyo upande wa Jamhuri walipaswa kuthibitisha manifestation of deed, siyo overt act siyo kuchapisha. Section 13 ya Interpretation Act inaonyesha kuwa maneno haya hayako similar unless kuwe na neno similar mbele ya hayo maneno.
Mtu hatokuwa sahihi kama mtu ataonyesha neno moja likatumika kati ya hayo, au mtu akatumia neno lingine lisitumike, hakuta kuwa na nyingine litakaloladhimisha Jamhuri lithibitishe overtact na siyo deed.
Upande wa Jamhuri kupitia mashahidi wake 17 unathibisha kuwa umeonyesha viini vya kosa la uhaini, nikianza na kiini cha kwanza; kuhusu kiini kuwa yeye ni mtiifu na raia wa Tanzania ambapo mtuhumiwa alikiri ye ni raia hoja hii tunaiweka pembeni kiini kimekuwa proved.
Ukija kiini cha pili, cha kutengeneza nia, naomba tuangalie maneno yaliyotumika "ALITENGENEZA NIA"
Case ya Mahendra KCV Vs KarmaTaka, 1238/20 (case ya India)
Inasema uchochezi ni kushawishi, kushauri na yaweze kusababisha consequences kwa tafsiri hii maneno yaliyotumika kwenye hati ya mashtaka bila ya kufanya hajitetee yanaonyesha wazi yana suggest consequences, kwahiyo Mahakama kutompa mshtakiwa haki ya kujitetea yanaweza yakamtia hatiani.
Maneno yamethibitishwa na mashahidi wote akiwemo PW17 ambaye yeye alisikia kwa ukaribu kabisa.
Maneno ya kutishia serikali yanaweza kuthibitishwa kwa vyombo mbalimbali; Kutishiwa/ vitisho imetafsiriwa kwenye Oxford dictionary 2nd Edition (anasoma)
Kwa mujibu wa kifungu cha 39 2 (d) mtu yeyote atakae tengeneza nia kwa nia ya kuitisha Serikali basi utakuwa umetenda kosa.
Hivyo, upande wa Jamhuri kiini cha nia ya kuitishia serikali tunasemq kimethibitishwa na ushahidi wa Pw1, Pw16 & Pw3.
Ambapo Pw1 na Pw16 wamesema maneno yaliyochapishwa yalikuwa na lengo la kuitishia Serikali na wakasema kuitishia Serikali ni kuvunja sheria ambapo serikali ni kwa ajili ya kutimiza majukumu kwa mujibu wa sheria. Pw3 anasema walipanga kupiga watu mawe.
Hoja kuwa Serikali imetajwa au la, serikali imetajwa constructively kupitia hoja ya constructively kilichotajwa ni serikali, halijatishwa Bunge wala Mahakama kwahiyo tunasema primafacie imekuwa established, kupitia hoja hiyo ya to intimidate ambayo imekuwa proved.
Waheshimiwa Majaji, upande wa Jamhuri umeleta mashahidi wengi ambao wanaonyesha walichocheka na uchochezi wa mtuhumiwa.
Kitendo cha kuyatoa na kuchapisha ndo kinaonyesha manifestation with deed, unlike case ya Agrey likungi matata, unlike case ya Khatibu Gandi na hapa ndiyo utaona kila kesi inaamuriwa kutokana na mazingira yake.
Cross examination haikupinga maneno ilijikita kuhoji je maneno yale ni uhaini?
Mashahidi wamethibitisha kuwa mshtakiwa alitoa maneno yale, hivyo upande Jamhuri inaona imethibitisha kwa kuwa haijawa crossexamined.
Waheshimiwa suala la kuchapisha limezungumzwa na mashahidi upande wa Jamhuri, kwamba waliona You tube kwenye account ya Jambo Tv
Part 250 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 248
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji ni muhimu kukumbuka kuwa, mimi ni mshtakiwa pekee katika kesi hii na ikumbukwe katika kesi ya Khatibu Gandi inasema maneno ya mtu mmoja, hayatengenezi uhaini, kwa ushahidi uliotolewa haujathibisha nia ya kutenda kosa la uhaini then on the basis kuwa kusipokuwa na primafacie case nitaitwa nijitetee kwa kipi?
Ni ushahidi gani nisipojitetea utanitia hatiani? Ushihidi ukoje kuhusu publication ya reasonable act?
Lazima kuwe na ushahidi wa machapisho au matendo ya wazi wakati wa pre trial Upande wa Mashtaka wanasema mimi nilichapisha maneno kwenye mtandao wa Jambo TV, hivyo uthibitisho wa haya maneno ulitakiwa uwepo Jambo Tv.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwaelekeze ukurasa wa 185 wa record za Mahakama, upande wa mashtaka ulionyesha ushahidi wa nyaraka 9 na aina 2 za vielelezo ikiwemo Video clips, hawajaleta hata moja.
Shahidi PW 17 ni shahidi pekee wa eye witness aliyenishuhudia kwenye mkutano, testimony ya mashahidi, shahidi PW 17 ndiyo shahidi mwenye ushahidi mzito, alisema yeye na wenzake watano ndiyo waliorecord na kurusha, amesema kwa maneno yake na kwa maandishi kupitia kielelezo D16 na ni shahidi wao, Kwahiyo kama ni tuhuma ya publication siyo yak wangu, aliyepublish ni PW 17 na amesema mpaka leo vipo kwao.
Ushahidi wa nani aliyechapisha hawajaujibu.
Waheshimiwa Majaji, walidai ooh wewe ndiye uliyeitisha Mkutano, shahidi wao PW 17 amesema mwaliko waliupata kwa afisa habari wa Chadema anaitwa Brenda Rupia, na nikamuuliza uliniona mimi nikifanya maandalizi nikipanga viti akasema, hakuna.
Kwenye hili suala la tatu hawajathibitisha kabisa kosa la kuchapisha maneno.
Naomba nimalizie,
Kama hakuna proof ya kucommint treason act, hakuna intention maana yake ni kuwa hakuna primafacie case, na kama hakuna primafacie case mkiruhusu nijitetee mtakuwa mnafanya makosa ya kisheria.
Sasa Waheshimiwa majaji msipokubali mnafanyaje? Mnafanya kile ambacho sheria imewataka mfanye kwa mujibu wa kifungu cha 312 (1) kufanya finding ya kuwa hakuna case ya kujibu.
Waheshimiwa Majaji naomba kama mtatoa huo uamuzi muutoe leo, kama mnaridhika na hoja hii, reason ruling mtatupa baadae, hakuna haja ya mimi kurudishwa Ukonga leo. Hili ni la pili;
La 3 lipo kwenye kifungu cha 367 cha CPA (Sheria ya Makosa ya Mwenendo wa Jina), kama mashtaka ni ya uonevu ya kusingizia mnaweza kuamuru mtuhumiwa alipwe fidia, haya maumivu yangu na familia yangu nani atafidia?? mashahidi wote 17 mmewasikia.
Hivyo naomba iamriwe kuwa sina kosa la kujibu pia ipangwe tarehe nije kuthibitisha madai/ fidia yangu.
Naomba niwape Waraka wa kikosi kazi wa Umoja wa Mataifa, uamuzi wa tarehe 23/2/2026 unaosema niachiwe mara moja na kulipwa fidia. Hivyo Waheshimiwa Majaji msimamo ni kuwa hakuna primafacie case na kwakuwa hakuna Primafacie case, sheria inawataka muandike findings ya NO CASE TO ANSWER
Waheshimiwa majaji ya kwangu ni hayo tu.
Mhe. Lissu anamaliza na kuketi.
Jaji Ndunguru : Ehee Jamhuri ?
Wakili wa serikali Katuga anasimama anasema Upande wetu kwanini tunaona mshatikiwa ana kesi ya kujibu ni kutokana na makosa aliyoshtakiwa nayo kwa mujibu wa kifungu cha 39 (2) (d)
Anasoma kosa kama lilivyoainishwa katika hati ya mashtaka na anaainsha maneno ya uhaini...
"WANASEMA KITU KIMOJA SAHIHI HAPA, WANASEMA TUTAHAMASISHA UASI, NI KWELI TUTAHAMASISHA UASI, TUTAKINUKISHA VIBAYA......"
Waheshimiwa DPP Vs Philipo Joseph Mtonda, 217 Rufaa ya jinai, Tanzlii 2021.... case hii ili cite case Tambaklal na ikarudia maneno ya hiyo Landmark cases ya Tambklal case.
Part 249 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 247
Mhe. Lissu anasema Katika kifungu cha 546 cha criminal procedure code ambacho kwasasa ni kifungu cha 312 (1).... kwamba masharti ya kifungu cha 246 ambacho saa hizi ni 312 (1) ni cha lazima , wajibu wa kuthibitisha mashtaka upo kwa Upande wa Mashtaka, na sheria yetu imeweka wazi kwamba endapo utashindwa kuthibitisha basi Mahakama itapaswa kumwachia mtuhumiwa.
Maamuzi yote haya yanasema kama Mahakama itamwita mtu ajitetee wakati asipojitetea hakutwi na hatia hii ni makosa kwa mujibu wa case ya Murini vs Republic.
Mahakama ya rufaa Kenya, katika case ya Antony Njuwe Njeru Vs Republic 2006 EKLR, Na yenyewe ilikubali msimamo wa case ya East Africa ya Trambklal
Case ya Republic Vs Benard Ruwangu Ingubu, 2025 KHC 11026 ( KLR) pia imekubali msimamo huo, case nyingine ni case ya Republic Vs James Ogwagwa Nyakina & another, 2025 KEHC 11403 (KLR)
Mahakama ilikuwa ikijadili kifungu ambacho kinaendana na kifungu chetu cha 312 (1)
Waheshimiwa baada ya kuweka huo msingi, naomba nizungumzie kesi ya uhaini inayonikabili, hii siyo kesi ya kwanza katika nchi yetu ni kesi ya tatu, kesi mbili zilizotanguliwa ziliamliwa finally, case ya Grey Likungu Matata na wenzake Vs Jamhuri, (1971) EA496 Mahakama ya Rufani ya Afrika Mashariki, na case ya Khatibu Gandi na wenzake TLR.
Katika kesi ya Grey Likungu Matata, Mahakama iliweka masharti matatu ya kuthibitisha uhaini;
i) utiifu kwa Jamhuri/ Raia
ii)Nia ya kutenda kosa
iii)Nia ithibitishwe kwa maandishi au matendo
Waheshimiwa majaji msimamo wa Mahakama wa case ya Grey Likungi Matata ulikubaliwa wote katika kesi ya Tanzania ya Khatibu Gandi katika ukurasa wa 13 wa kesi ya Khatibu Gandi na Wenzake, ambapo iliongeza mengine kwa kujiuliza.... Je maneno matupu yanatengeneza Uhaini? Na majibu yapo ukurasa wa 55, kuwa maneno matupu siyo matendo ya wazi kwenye kosa la uhaini isipokuwa hayo maneno yaelezee kitendo cha uhaini, lakini kusema tu tunataka kuipindua Serikali...hayo ni maneno tu.
Ukurasa wa 67, ijapokuwa ni sahihi kuwa maneno ni maneno matupu, ikiwa ni maneno yanayotumiwa na mtu mmoja, yanaweza kuwa uhaini yakitumiwa na watu zaidi ya mmoja.
Ushahidi unasemaje kuhusiana na nia?
Ushahidi haujathibitisha kama kulikuwa na kosa la kutenda uhaini,
Waheshimiwa majaji kifungu cha 39 (2) (d) kinasema; lazima kuwe na nia ya kuitishia serikali, au bunge au mahakama, shitaka ambalo liko mbele yenu Waheshimiwa majaji linasema maneneno yafuatayo " Tundu Lissu akiwa chini ya utiifu wa Jamhuri ya muungano alionyesha nia ya kutenda kosa uhaini........."
Sheria inasema kosa lazima uitishie Serikali, Bunge au Mahakama, kwa hayo maneno Bunge, Mahakama wala Serikali havijatajwa hata mara moja, swali ni je Serikali imo haimo kwenye hati ya mashtaka? Haimo.
Serikali ni nini Waheshimiwa majaji ? Serikali ni neno la kikatiba siyo maneno ya kuokotwa na Mapolisi mtaani. Serikali imetafsiriwa katika Ibara ya 151 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ooh ooh uchaguzi, ooh Serikali, Serikali haindeshi uchaguzi, uchaguzi unaendeshwa na Tume ya uchaguzi, ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jambo la pili Waheshimiwa majaji, hayo maneno " TUTAZUIA UCHAGUZI" " TUTAKINUKISHA" na mengine yote..... siyo kosa kisheria.
Sheria ya Uchaguzi wa Rais wabunge na Madiwani, 2024 Cap 7 imeanisha makosa kibao ya jinai...ambapo hayo maneno hayamo, sasa hili ni kosa la aina gani? Hakuna.
Infact, hakuna ushahidi wa kutenda kosa lolote la jinai kwa sheria za Tanzania zinazoainisha makosa yanayotokana na hayo maneno waliyoainisha kwenye hati ya mashtaka na kama siyo kosa hakuwezi kukawa na nia ya kosa la uhaini.
Part 248 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 246
Wakili wa Serikali - Katuga amewainamia mawakili wa serikali ni kama kuna jambo wanajadili.
Wakili wa Serikali Katuga anainuka anasema Waheshimiwa Majaji, Mtuhumiwa amewalika kwenye kifungu 312(1) hii inahusu no case to answer, mimi nimewaalika kwenye case to answer, Waheshimiwa hicho kifungu alichokitumia inasema statement iliyotumiwa, itatuleta tafsiri tofautitofauti kwa nature ya case hii, halafu kinazungumzia Mawakili wa pande zote mbili hakizungumzii mtuhumiwa ambaye hajawakilishwa, ndo maana nikasema hakuna kifungu mahususi, hii inabaki kuwa discretion ya Mahakama.
Upendeleo wetu tunaichia Mahakama, kuna written submission na kuna oral, ambapo bado Mahakama hii haijaamua.
Waheshimiwa at this instance hatuthibishi guilty ni primacie case to answer.
Anasimama Mhe Lissu anasema Waheshimiwa Majaji hili jambo ni dogo sana, halitaki majadiliano makubwa hivi. Kifungu No. 312(1) inaipa wajibu Mahakama na siyo discretion. Kifungu kinazungumzi no case to answer, hakuna mahali inaonyesha case to answer
Wakili wa Serikali - Katuga anasimama nakusema kuwa Waheshimiwa majaji mimi sijasema hayo naona mtuhumiwa anajielekeza kwenye mambo mengine, labda kama ni off record.
Mhe. Lissu : Waheshimiwa naomba mniache nimalizie.
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema, aah sasa basi mtuache sisi tuamue hilo, uzuri wote mnakubaliana kuwa mnafanya submission.
Wakili wa Serikali - Katuga & Mhe. Lissu: sawa Waheshimiwa majaji.
Wakili wa Serikali - Katuga: Naomba mshtakiwa apewe hii East Africa Law Report aliyopewa na Mawikili wake wa research.
Mhe. Lissu anakabidhiwa.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa rudia ile reference
Mhe. Lissu: Mimi nilikuwa nanukuu tu ile section 312(1) na kwa mujibu wa ile mimi ndiyo nilikuwa napaswa kuanza, hivyo naomba kuanza.
Jaji Ndunguru : eeeh prosecution?
Wakili wa Serikali - Katuga: Sisi hatuna pingamizi waheshimiwa.
Jaji Ndunguru : Case upande wa mashtaka imefungwa, na mnapaswa kusubmitt kwa mdomo.
Mhe Lissu anasema Waheshimiwa Majaji baada ya kusikiliza ushahidi wote wa upande wa mashtaka wa mashahidi wote 17, naomba kutoa hoja kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kabisa kuthibitisha kwamba kuna prima facie case ya kuiwezesha Mahakama hii kumtaka mshtakiwa ajitetee.
Sasa Waheshimiwa majaji prima facie case ni kitu gani?
Waheshimiwa majaji prima facie case/ primafacie evidence ni ushahidi wa mashtaka unaotolewa na upande wa mashtaka ambao usipojibiwa kwa ushahidi wa utetezi mtu anafungwa au analipa fine ambapo kwa case kama ya uhaini mtu ananyongwa.
Kama upande wa mashtaka umetoa ushahidi ambao hata mtuhumiwa hawezi kujibia/ kujitetea then hakuna hatia (prima facie case)
A primafacie evidence siyo ushahidi wa mwisho katika case, ushahidi wa mwisho ni ule unaojumuisha ushahidi wa utetezi, hivyo Prima facie case ni ushahidi wa upande wa Jamhuri.
Msingi wa kisheria wa primafacie case to answer ni kifungu cha 312 (1) ambacho nimeshakisoma, hiki kimefanyiwa maamuzi mengi za Mahakama za juu ambacho kimetengeneza misingi ya kisheria ( Legal principles ) kuhusiana na nini kinapaswa kufanyanyika kuhusiana na hoja ya hakuna case ya kujibu.
Kesi ya East Africa ya Raumanlal Trambaklal Bhatt v Public 332 esp 334-335 hii ina umuhimu ule wa case ya Mkisa Biscuit kwa namna ilivyoweka msingi kisheria Mhe. Lissu
(anasoma citation ya Tramnaklal case)
Mahaka imesema, haitoshelezi tu kuwa ushahidi mwingi umetolewa tu, lazima ushahidi huo mwingi uwe na uzito na credibility.
Waheshimiwa msingi huu Tramnklal ulikubaliwa na Mahakama hiyo ya rufani katika case ya Murini vs Jamhuri 1967 EA 542, Uk 544, Mahakama ilinukuu approval uamuzi wake wa miaka kumi kabla wa case ya Tramnklal.
Part 247 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 17, 2026
Last time tuliishia part 244 so leo tunaendelea na -;
Part 245
Wanaingia mawakili wa Serikali,
Then kaingia Mhe. Lissu akiwa anasindikizwa na kundi la askari magereza wapo wengi kama kawaida yao.
Mhe. Lissu kaingia na vibe la kutosha na Wanachama na Wananchi waliojitokeza Mahakamani wanapiga makofi mengi ya shangwe.
Imepigwa High Cooooooourt...
Majaji wanaingia, wapo watatu wakiongozwa na Jaji Ndunguru, wanaketi kwenye viti vyao.
Karani anasoma case no . โ- Jamhuri Vs Tundu Antipas Lissu
Anasimama Wakili wa serikali anatambulisha jopo la Mawakili wa Serikali na mtuhumiwa Mhe. Lissu
Wakili wa Serikali anasema wana maombi mawili ambayo wanaomba kuyawasilisha;
Jaji anasema tuendelee
Wakili wa Serikali anasema maombi hayo atawasilisha wakili Katuga.
Wakili wa Serikali -Katuga anasema Waheshimiwa majaji upande wa Jamhuri tunamaombi mawili
1.Baada ya kupitia ushahidi ambao umeshatolewa hapa Mahakamani na mashahidi waliobaki, baada ya kuangalia agreed facts, upande wa Jamhuri unaona ni ushahidi toshelezi, hivyo tunaitaarifu Mahakama kuwa Upande wa Jamhuri unafunga ushahidi wake na kwamba tunaomba imark kwamba upande wa Jamhuri unafunga case yake.
2. Ingawa hakuna kifungu kinaonyesha majumuisho ya no case to answer, mimi naliita kuwa ni kosa ambalo siyo kosa zoefu hasa kwajinsi tunavyomtuhumu mtuhumiwa kulicommitt, hivyo tunaomba tufanye submission ya no case to answer.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama anachokusema?
Mhe Lissu: Kwanza kuhusiana na kufunga kesi kwa upande wa mashtaka, hilo sina shida nalo nilisema toka wiki iliyopita tayari wameshakata pumzi.
Watu wanacheka ๐๐๐๐
Kuhusu ombi la pili, Wakili Katuga anasema kuwa japo hakuna kifungu, mimi nasema kifungu kipo pale ambapo ushahidi wa upande wa mashtaka umefungwa, na kwamba pale ambapo Mahakama inaona hakuna kosa ambalo mtuhumiwa ametuhumia nalo then Mahakama husikiliza pande zote mbili kama kuna kesi ya kujibu au la, kifungu cha 312 (1) cha sheria ya mwenendo wa mashtaka, naomba nikisome
(anasoma...)
Hivyo Waheshimiwa Majaji, kwa practice mtuhumiwa ndiye anayeanza kuwasilisha hoja za kama ana kesi ya kujibu au la, mimi niko tayari kuanza Waheshimiwa.
Asante ni hivyo tu.
Part 246 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 244
Majaji wanateta kwa dakika nyingi kidogo na mwingine yeye anakuna kichwa ameangalia chini.
Wameandika muda mrefu sana, nafikiri wanashauriana sababu gani watumie kulikubali ombi la Wakili wa Serikali.
Amemaliza kuongea na Jaji mwingine huyu Mwenyekiti wa jopo sasa anaongea na jaji wa kushoto kwake.
Huyu wa kushoto mara zote yeye huwa kama hanaga habari amekaaa tu anafanyaga mambo yake na kucheka.๐
Yule wa upande wa kulia ndo huwa yuko serious muda wote.
Ngoja tusubiri majibu ya Jaji.
Baada ya kujadiliana kwa dakika kadhaa
Jaji Ndunguru amewasha kipaza sauti anasema tumesikia hoja zote, kimsingi tunakubaliana na aliyosema Mshitakiwa kuwa tumetoa maelekezo ya mara kwa mara.
Mahakama imesimamia maelezo hayo kuwa Jumatatu mashahidi wote wataletwa basi tukutane Jumatatu Tar. 17/08/2026
Kesi imehairishwa mpaka Jumatatu na kwa jinsi Mawakili wa Serikali walivokuwa wanahangaika leo, sitashangaa ikifika Jumatatu halafu wakasema wamefunga ushahidi wao.๐๐๐๐
Naomba Repost yako.