BUNGE LAPITISHA KWA KISHINDO BAJETI YA WIZARA YA NISHATI 2026/2027
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha kwa kishindo shilingi trilioni 2.53 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati 2026/2027.
BUNGENI: Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius J. Ndejembi (Mb.), akizungumza wakati akijibu hoja na michango ya Wabunge na kuhitimisha mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2026/2027, leo Aprili 23, 2026, Bungeni jijini Dodoma.
Akiwasilidha hotuba yake bungeni jijini Dodoma, Mhe. Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2026/27 wizara itaweka mkazo katika kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika mijini, vijijini na vitongojini pamoja na kuongeza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.
WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali itaendelea kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya ndani na ziada kwa ajili ya kuuza nje ili kuongeza mapato ya fedha za kigeni.
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikishwaji Wazawa na Wadau kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Charles Nyangi, amesema uwezo wa kuzalisha gesi katika kisima B5 katika kitalu cha Mnazi Bay mkoani Mtwara umekuwa zaidi ya mara mbili ya ilivyotarajiwa.
Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayohusisha Wizara ya Nishati na Taasisi zake yameanza katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma huku yakilenga kutoa elimu ya nadharia na vitendo kuhusu Sekta ya Nishati.
Waziri wa Nishati, Deogratus Ndejembi, amewahamasisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, yaliyoanza rasmi leo Aprili 20, 2026.
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi akipata maelezo kuhusu mfumo wa Kidigitali wa Kupanga na kusimamia miradi ya REA *(REA Digital Platform)* wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Picha mbalimbali katika Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Felchesmi Mramba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akigawa mitungi ya gesi kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Mama na Baba Lishe katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dsm tarehe 21 Aprili 2026.